WANACHAMA wa Yanga wamemuangukia mwenyekiti wao aliyejiuzulu Yusuf Manji baada ya kukataa ombi la kuachia ngazi la kiongozi huyo. Wanachama wa klabu hiyo kutoka matawi 65 ya mkoa wa Dar es Salaam walikutana jana na kumtaka makamu mwenyekiti wao, Clement Sanga kuhitisha haraka kmkutano wa dharura. Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambapo kwa pamoja waliazimia kukataa ombi la kujiuzulu kwa Manji. “Wanachama hawataki Manji akae pembeni, wanataka mkutano wa dharura uitishwe siku 14 toka leo kwa mujibu wa katiba, kamati ya utendaji inakaa leo ( Jana) mchana itapitia maombi ya wanachama na kutoa maamuzi.” alisema Mkwasa. Naye Makamu Mwenyekiti wa matawi Bakili Makele alisema kuwa baada ya kutafakari barua ya Manji, ambayo inaeleza moja ya sababu ya kujiuzulu ni kutokana na afya yake, lakini wao wanasema bado wanamuhitaji. Naye Mwenyekiti wa Keko Ukombozi Joseph Kalindwa akizungumzia hilo alisema “ Manji alitukuta kipindi kigumu mno tukiwa tu...
Maoni
Chapisha Maoni