Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2020

Diamond atua studio za Swizz Beatz Marekani

Picha
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania,Diamond Platnumz, ameonekana akiwa katika studio za mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz. Hilo linatokea ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtayarishaji huyo, aweke wimbo wa ‘Gere’ ulioimbwa na Tanasha Donna akimshirikisha Diamond na ile ya singeli ya ‘Wanga’ iliyoimbwa na Meja Kunta akimshirikisha Lavalava wa lebo ya WCB katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram. Kama haitoshi siku sita zilizopita mtayarishaji huyo aliweka video katika ukurasa wake ikimuonyesha  mwanamuziki Alicia Keys ambaye ni mke wake akionekana kucheza wimbo wa Wanga. Diamond katika picha hiyo ameonekana amekaa kwenye kiti akiwa amevaa fulana ya njano wakati Swizz Beatz yeye aliyejiegesha kwenye moja ya mashine ndani ya studio hiyo akiwa amevaa tracksuit ya rangi ya chungwa na kofia yenye rangi ya kaki. Katika picha hiyo, Diamond ameandika ’Kanda! Kanda! nipo na mfalme ananifanya nijisikie kama nipo nyumbani Tanzania, najisikia kama

Vita vya Syria. Wanajeshi wa Uturuki 33 wauawa katika mashambulio Idlib

Picha
Takriban askari 33 wa Uturuki wameuawa katika mashambulio ya anga ya "vikosi vya Syria" Kaskazini-Magharibi mwa Syria, amesema afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki . Wengi waliumizwa katika jimbo la Idlib, amesema Rahmi Dogan, Gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay. Taarifa nyingine zinasema idadi ya vifo ni ya juu zaidi. Uturuki kwa sasa inajibu kwa kuyalenga kushambulia dhidi ya maeneo ya vikosi vya Uturuki. Vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vinajaribu kurejesha jimbo la Idlib ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi wanaosaidiwa na wanajeshi wa Uturuki Maafisa nchini Syria bado hawajatoa kauli yao wazi kuhusu mapigano ya sasa ya Idlib, ambalo ni jimbo la mwisho lililosalia mikononi mwa upinzani. Jeshi la Uturuki lilianza kupiga maeneo ya Syria baada ya Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kufanya mkutano na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama mjini Ankara. Jimbo la Idlib Kiongozi wa Uturuki anataka vikosi vya Syria virudi nyuma kutoka kwenye maeneo ambay

Ubalozi wa Marekani waonya dhidi ya shambulio la kigaidi katika hoteli moja Nairobi Kenya

Picha
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa onyo kwamba magaidi huenda wakashambulioa hoteli moja kubwa nchini Nairobi. Kulingana na ubalozi huo, hoteli iliolengwa ni maarufu kwa kuwa hutemebelewa sana watalii na wanabiashara. ''Makundi ya kigaidi huenda yanapanga njama dhidi ya hoteli moja kubwa mjini Nairobi. Hoteli inayolengwa haijatambulishwa lakini inaaminika kuwa hoteli ilio maarufu sana na watalii na wafanyabiashara wa kigeni'', lilisema onyo hilo. Wakenya wameshauriwa kuwa waangalifu wakati wanapotembelea ama kuishi katika hoteli mjini Nairobi. ''Unapokuwa unaishi katika hoteli jifahamisheni kuhusu njia za kutorokea . Panga mapema jinsi utakavyoweza kutoroka katika hoteli iwapo kutakuwa na dharura yoyote'', liliongezea onyo hilo. Wakati huohuo Inspekta jenerali wa polisi nchini Kenya Hilary Mutyambai amewaomba Wakenya kuwa watulivu , akisema idara ya polisi imeimarisha usalama nchini kote mbali na kulinda mipaka yote. Hatahivyo amewataka

Vita vya Syria: Mashambulio dhidi ya Idlib yalenga shule na hospitali'

Picha
Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa zilikua ni shule na Hospitali ya jiji la Idlib na miji inayozingira jiji hilo, yamesema makundi ya kutete haki za binadamu Takrina raia 20, mkiwemo watototisa wameawa katika mashambulio ya anga ya jeshi la Syria katika jimbo la Idlib Jumanne, Shirika la waangalizi wa mzozo la Syria limesema. Shrika hilo ambaloi linachunguza haki za binadamu limesema kuwa shule na hoispitali zilikua miomngoni mwa maeneo yaliyolengwa. Vikosi vya serikali ya Syria vimekuwa vikiendeleza mapambano makali kwa ajili ya kulichukua jimbo la Idlib, likiwa ni eneo muhimu nchini Syria ambalo bado liko chini ya udhibiti wa waasi na wapiganaji wa jihadi Takriban watu milioni tatu wanaishi katika maisha ya shida katika jimbo hilo. Rami Abdel Rahman, mkuu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria , amesema kuwa mashambulio yalilenga jiji kuu ambalo pia linaitwa -Idlib - na maeneo mengine yanayozingira jiji hilo Mtoto mmoja wa shule na waalimu watatu pamoja

Corona Virus:Dunia lazima ijiandae kwa janga, WHO yasema

Picha
Shirika la afya duniani limesema dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona. WHO linasema ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi". Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia. Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa ya Korea Kusini , Italia na Iran ikisababisha. Hata hivyo , maambukizi mengi yanapatikana nchini Uchina, chanzo cha asili ya virusi, ambako watu zaidi ya 77,000 wamepata maradhi hayo na zaidi ya 2,600 wamekufa. Zaidi ya visa 1,200 vimethibitishwa katika nchi 30 na kumekuwa na vifo zaidi ya 20. Italia iliripoti vifo vinne zaidi Jumatatu, na kuifanya idadi ya vifo nchini humo kufikia watu saba. Masoko ya hisa yalishuka kote duniani kwasababu ya hofu ya athari za kiuchumi. Uch

Kabendera awashukuru waandishi wa habari, aanza kuomboleza kifo cha mama yake

Picha
Dar es Salaam. Mwandishi wa Habari nchini Tanzania, Erick Kabendera amesema kwa sasa ndiyo anaanza maombolezo rasmi ya msiba wa mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi. Mama wa Kabendera, Verdiana  alifariki dunia Desemba 31, 2019, katika hospitali ya Amana Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Kabendera amesema hayo, leo Jumatatu Februari 24, 2020 katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, muda mfupi baada ya kuachiwa huru na mahakama hiyo. Baada ya kifo hicho, Kabendera aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba aruhusiwe kwenda kuaga mwili wa mama yake katika shughuli ya mazishi iliyofanyika kanisa la Katoliki Temeke Dar es Salaam lakini hakuruhusiwa kwa madai Mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kusikiliza maombi yake. Katika maelezo yake leo Jumatatu baada ya kuachiwa, Kabendera amewashukuru watu wa makundi mbalimbali kwa kumpigania katika kipindi chote wa kesi yake iliyodumu kwa zaidi ya miezi saba mahakamani hapo. Ndugu wanataaluma wenzangu nawashukuru, waandi

Mtu mmoja afa kwa virusi vya Corona Italia.

Picha
Mwanaume mmoja wa Italia aliyekuwa ameathirika na virusi vya Corona amefariki dunia na hivyo kifo hicho kuwa cha kwanza kutokea barani Ulaya tangu virusi hivyo vilipozuka China na kusambaa ulimwenguni. Waziri wa Afya wa Italia, Roberto Speranza amesema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 78, alifariki siku ya Ijumaa kwenye hospitali ya mji wa Padua, alilokuwa amelazwa kwa siku 10. Speranza amesema mwanaume huyo alikuwa miongoni mwa watu wawili waliokutwa na virusi vya Corona vinavyojulikana kama COVID-19 katika mkoa wa Veneto. Madaktari watano na wauguzi pamoja na wagonjwa kadhaa wameambukizwa virusi hivyo katika hospitali ya Codogno ambako mgonjwa huyo alikuwa akitibiwa. Watu wengine watatu ambao walikwenda kwenye mgahawa mmoja kwenye mkoa wa Lombardy, walithibitika kuugua virusi vya Corona. Kuzuia mripuko Maafisa wa Italia wameamuru kufungwa kwa shule, majengo ya umma pamoja na migahawa kwenye miji 10 ya kaskazini mwa nchi hiyo baada ya visa vingine 15 kuripotiwa. Visa vyote

'Tunahofia kulima mashamba yetu upande wa Uganda'

Picha
Mkutano wa rais wa R wanda Paul Kagame na Yoweri Museveni wa Uganda kumaliza tofauti baina ya nchi zao unatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa kwenye mpaka wa Gatuna baina ya nchi hizo mbili. Mkutano huu unachukuliwa kama hatua ya mwisho ya kutathmini utekelezwaji wa makubaliano yaliyosainiwa na marais hao mwaka jana mjini Luanda –Angola chini ya upatanishi wa rais wa Angola na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Rwanda wanaoishi maeneo ya mpakani bado wana kilio kwa kuwa wamekuwa wakiitegemea Uganda kwa huduma nyingi na sasa hawaruhusiwi na serikali ya Rwanda kukanyaga kwenye ardhi ya Uganda. Wengi wana mashamba nchini Uganda na hulazimika kutumia njia haramu kwenda nchini Uganda. Mwandishi wa Newsday Swahili ametembelea wananchi hao kwenye mpaka wa Cyanika na kutuletea taarifa ifwatayo

Mmoja afariki polisi wakituliza vurugu mkoani Mwanza

Picha
Mwanza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema John Lulyeho (39) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati polisi wakituliza vurugu kwenye ranchi ya mifugo ya Mabuki iliyopo Wilaya ya Misungwi. Akizungumza leo Jumatano Februari 19, 2020 Muliro  amesema Lulyeho alifariki wakati polisi wakimpeleka hospitali ya Wilaya kwa matibabu. Amesema tukio hilo lilitokea Februari 16, 2020 saa 10 jioni. “Siku hiyo polisi walipokea taarifa kwamba shamba hilo limevamiwa na wahalifu waliokuwa wakiwashambulia  wafanyakazi wa shamba hilo waliokuwa katika hali mbaya karibu kupoteza maisha.” “Walipofika walikuta wafanyakazi wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Polisi walipofika nao walianza kushambuliwa kwa mawe na askari wetu wawili walijeruhiwa,” amesema. Amesema kundi la watu takribani  300 ilidaiwa waliingiza ng’ombe katika shamba hilo na kuanza kuwalisha kinyume na sheria, kanuni na utaratibu licha ya kupewa eneo la shamba hilo kulisha mifugo. “Wafanyakazi hao wal

Zitto Kabwe: Mahakama yamkuta na kesi ya kujibu kiongozi wa ACT-Wazalendo

Picha
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Katika kesi hiyo, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari. Hayo yanajiri siku moja tu baada ya Zitto ambaye ni rejea nchini baada ya kumaliza ziara yake katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani na Uingereza. Ziara hiyo imezua gumzo nchini Tanzania hususani baada ya Zitto kubainisha wazi kuiandikia barua Benki ya Dunia kusitisha mkopo wa elimu kwa Tanzania. Baadhi ya wanansiasa kutoka Chama tawala walitoa kauli za kutishia uhai wa mwanasiasa huyo huku yeye mwenyewe akidai kuwa kumekuwa na mipango ya "kumbambikia kesi ya uhujumu uchumi." Kesi ya uchochezi Leo Jumanne Februari 18, Mahakama ya Kisutu chini ya hakimu mwandamizi Huruma Shaidi imemkuta mwanasiasa huyo na kesi ya kujibu. Zitto sasa anatarajiwa kujitetea kwa siku nne mfu

Vita vya Syria: Serikali ya Syria itajuta kwa kuwashambulia wanajeshi wa Uturuki

Picha
Rais wa Uturuki ameionya serikali ya Syria kwamba italipa gharama kubwa kwa mashambulio dhidi ya wanajeshi wake katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria. Wanajeshi watano wa Uturuki waliuawa katika mji wa Idlib unaodhibitiwa na upinzani siku ya Jumatatu huku jeshi la Syria likiendelea kusonga mbele katika eneo la vita. Wanajeshi wa Uturuki walifyatua makombora kadhaa ili kujibu shambulio hilo , lakini rais Recep Tayyip Erdogan alisema: Tutaendelea na mashambulizi. Wakati huohuo wanajeshi wa Syria walikaribia kuikomboa barabara ya eneo la kaskazini la taifa hilo. Shirika la haki za kibinadamu lenye makao yake huko Uingereza SOHR liliripoti siku ya Jumanne kwamba wanajeshi wa Syria waliwafurusha waasi na wapiganaji wa kijihad kutoka eneo la mwisho ambalo walikuwa wakidhibiti magharibi mwa mji wa Aleppo. Hatahivyo hakuna thibitisho kutoka kwa jeshi ama vyombo vya habari vya serikali na kwamba kulikuwa na ghasia katika maeneo kadhaa ya barabara hiyo kuu siku ya Jumanne jioni

Walioko kwenye utalii sasa kufanya mitihani

Picha
SERIKALI imesema kuwa imeanzisha utaratibu wa kuwa na ithibati kwa wote walioko kwenye fani ya utalii ambapo kuanzia sasa watafanya mtihani maalumu, lengo likiwa ni kupata watu wenye viwango stahiki. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya utalii linalokutanisha wataalamu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Dk. Kigwangala alisema kuwa mbali na kupata watu wenye viwango, lakini pia wanataka kuimarisha eneo la usalama na ubora ili kuwatambua wote walioko kwenye fani hiyo. “Tumemua kwanza kuboresha kozi ambazo zinatolewa kwenye vyuo vya Serikali, lakini pia kuboresha mtaala ambao unatumika kwenye vyuo binafsi na kuanza kutoa kozi za uanagenzi, ambazo zinafundishwa kwa watu ambao walikosa mafunzo kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii na kuyapata wakiwa kazini. “Lakini pia tumeanzisha utaratibu wa kufanya ithibati kwa maana kwamba wewe soma kokote kule, lakini ukitaka kuajiriwa Tanzania kwenye ofis

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.02.2020: Grealish, Messi, Sterling, Pochettino, Coutinho, De Bruyne, Bale

Picha
Grealish angependelea kujiunga na Manchester United katika msimu wa usajili ujao iwapo ataondoka Aston Villa licha ya tetesi kwamba Barcelona na Real Madrid wameashiria kuwa na nia ya kumsajili. (Sun) Manchester City wako tayari kukubali kushindwa katika harakati zao za kumpata Lionel Messi katika msimu ujao wa ligi ya Premier baada ya kuarifiwa kwamba mshambuliaji huyo wa Argentina, 32, hana mpango wa kuondoka Barcelona. (Express) Mchezaji wa Manchester City Raheem Sterling anaamini kwamba atakuwa sawa katika Champions League kwenye mechi dhidi ya Real Madrid, ambao wanataka kumsajili mshambuliaji huyo, 25. (Telegraph) Aliyekuwa meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino bado hajafikia makubaliano ya kuwa meneja wa Manchester United ajaye msimu ujao. Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Brazil midfielder Philippe Coutinho, 27 ambaye kwasasa yuko Bayern Munich kwa mkopo, ataruhusiwa kuondoka kwa £77m ikiwa ni kiasi kidogo cha pesa huku Manchester United na iliyokuwa klabu yake Liv

Membe pasua kichwa

Picha
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe jana alifika mbele ya Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma na kuhojiwa kwa saa tano. Membe aliyepata kugombea urais ndani ya chama hicho na kuingia tano bora katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alifika ofisi ya makao makuu ya CCM jana saa 3:10 asubuhi na kutoka saa 8:43 mchana. Desemba 13 mwaka jana, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliketi na kuagiza makada watatu wa chama hicho waitwe na kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho baada ya kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali. Makada hao mbali na Membe, ni makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho tawala, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba ambao nao watahojiwa. Jana, akiwa ndani ya gari lake aina ya Range Rover Vogue baada ya kuhojiwa, Membe aliwaambia waandishi wa habari kuwa safari yake ya kuhojiwa na kamati hiyo ya maadili ilikuwa na manufaa makubwa kwake, kwa CCM na kwa taifa. Mbunge huyo wa zamani wa Mtama, alisema amekuwa mtu mwenye furaha m

Kiongozi wa Al-Qaeda al-Raymi auawa na shambulio la Marekani

Picha
Marekani imemuua kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Rasi ya uarabuni, Rais Donald Trump ameeleza. Qasim al-Raymi aliyeongoza kikundi cha Jihad tangu mwaka 2015, aliuawa wakati wa operesheni ya majeshi ya Marekani nchini Yemen, Ikulu ya Marekani imeeleza. Kiongozi wa wapiganaji wa Jihad amekuwa akihusishwa na mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maslahi ya nchi za Magharibi katika miaka ya 2000. Alichukua madaraka ya uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani. Kundi hilo la AQAP liliundwa mwaka 2009 kutokana na matawi mawili ya Al-Qaeda nchini Yemeni na Sausi Arabia, ikiwa na nia ya kuangusha tawala za serikali zinazoungwa mkono na Marekani na kuondoa ushawishi wa nchi za Magharibi kwenye ukanda huo. Tetesi kuhusu kifo cha al- Raymi kwa shambulizi la Marekani zilianza kusambaa mwishoni mwa mwezi Januari. Katika kujibu hilo kundi hilo lilitoa ujumbe wa sauti ukiwa na sauti ya al -Raymi tarehe 2 mwezi Februari ukisema kuwa wao ndi

Mwanamziki Lil Wayne asema ana asili ya Nigeria, je unakubalina naye?

Picha
Rapa - Lil Wayne - amewafurahisha raia wa Nigeria sana baada ya kutangaza kuwa amebaini rasmi kuwa ana uasilia 53 wa Nigeria . Mwenyekiti wa kamisheni ya Wanigeria wanaoishi ng’ambo bwana Abike Dabiri hata amemuita Lil Wayne ndugu yake na kusema kuwa anahamu ya kumkaribisha Nigeria.

Mahakama yatoa hati ya kukamatwa Jacob Zuma

Picha
Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka kuhusu rushwa dhidi yake. Hati hiyo itafanya kazi ikiwa atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990. Rais huyo wa zamani amefanikiwa kukwepa shutuma za rushwa dhidi yake kwa zaidi ya miaka 10. Lakini leo, sheria haikuwa upande wake. Hati ya kukamatwa kwake imetolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake. Jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka wakisema kuwa mteja wao alikuwa mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita. Jaji Dhaya Pillay alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mah

Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia

Picha
Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi afariki dunia akiwa na miaka 95, vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti. Runinga ya taifa ya Kenya (KBC), pamoja na vyombo binafsi vya Capital FM, Citizen TV na NTV vimeripoti taarifa hiyo ya msiba asubuhi ya leo Jumanne, Februari 4. Taarifa rasmi ya Ikulu ya Kenya inatarajiwa kutolewa hivi punde. Mzee Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kutoka 1978 mpaka 2002.

Mkanyagano wasababisha vifo vya wanafunzi 13 Kenya

Picha
Wanafunzi 13 wa shule ya msingi Kakamega nchini Kenya wamefariki baada ya kupata taharuki na kukanyagana shuleni. Mkuu wa kituo cha polisi cha Kakamega ,bwana David Kabena amesema kuwa wanafunzi wengine 39 walijeruhiwa na 20 wamepata huduma ya afya tayari. Inadaiwa kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Zaidi ya wanafunzi 100 wanatibiwa na wengine wako kwenye hali mbaya. Mkanyagano huo ulitokea baada ya kengele ya kumaliza masomo kupigwa na wanafunzi walikuwa wakitoka kuelekea nyumbani. Ripoti zinasema kuwa wanafunzi hao walikuwa wakitoka katika madarasa yao mwendo wa saa kumi na moja jioni wakati mkasa huo ulipotokea. Imedaiwa kwamba baadhi yao walianguka kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hilo walipokuwa wakitoka darasani. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa wanafunzi wawili wamepelekwa katika chumba cha dharura katika hospitali iliyopo kaunti ya Kakamega. Wazazi wamekusanyika hospitalini wakiwa na hofu kuwa inawezekana kuna wanafunzi wengi zaidi wamejeruhiwa.

Maswali magumu Makonda kuzuiwa kwenda Marekani

Picha
Hatua ya Marekani kumpiga marufuku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingia nchini humo imeibua maswali magumu, huku baadhi ya wachambuzi wakieleza kuwa inalenga kutoa tahadhari kwa Serikali kuelekea uchaguzi mkuu. Dar es Salaam. Hatua ya Marekani kumpiga marufuku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingia nchini humo imeibua maswali magumu, huku baadhi ya wachambuzi wakieleza kuwa inalenga kutoa tahadhari kwa Serikali kuelekea uchaguzi mkuu. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani juzi imesema sababu za kumzuia ni pamoja na kuhusika kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kukandamiza upinzani. Makonda pia amehusishwa na ukandamizaji wa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na kulenga baadhi ya makundi katika jamii. Mwandishi wetu aliyemfuata Makonda wakati akitoka katika maonyesho ya wiki ya sheria Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, hakuweza kupata maoni yake kuhusu zuio hilo. Mwandishi huyo wa Mwananchi alimu

Serikali, ubalozi watoa neno katazo la Marekani

Picha
SERIKALI imesema haijapata taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya Marekani juu ya kumzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuingia nchini humo na kuzuia Watanzania kushiriki bahati nasibu ya kupata kibali (visa) cha kuingia nchini humo. Juzi Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilitangaza kumzuia Makonda kuingia nchini humo kwa madai ya ukandamizaji wa haki za binadamu. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Emmanuel Buhohela, alisema mpaka sasa hawajapata taarifa rasmi. “There is no document’ hivyo, Serikali haiwezi kutoa kauli kwa mambo yanayozungumza kwenye mitandao,” alisema Buhoela. Gazeti hili pia lilifanya juhudi za kuwatafuta viongozi mbalimbali wa Serikali kuzungumzia suala hilo bila mafanikio ambapo simu ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Naibu wake Dk Damas Ndumbaro, zilikuwa zikita bila kupokelewa. MTANZANIA Jumap

Mapato ya ATCL yafikia Sh104.4bn

Picha
Mapato ya Shirika la Ndege ya Tanzania (ATCL) yameongezeka kutoka Sh24.7 bilioni mwaka 2016/17 hadi Sh104.4 bilioni mwaka 2018/19. Dodoma. Mapato ya Shirika la Ndege ya Tanzania (ATCL) yameongezeka kutoka Sh24.7 bilioni mwaka 2016/17 hadi Sh104.4 bilioni mwaka 2018/19. Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso juzi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo. Pia, Kakoso alisema idadi ya abiria imeongezeka kwa wastani wa abiria 4,000 kwa mwezi mwaka 2015/16 hadi 45,000 mwaka 2018/19. Alisema uwekezaji mkubwa wa Serikali umesababisha kupanuka kwa mtandao wa kutoa huduma. Kakoso alisema hivi sasa ATCL inatoa huduma ya usafiri wa anga vituo 17 kati ya hivyo, 10 ni vya ndani ya nchi. Alitaja vituo hivyo kuwa ni Bukoba, Dodoma, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro, Tabora, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Vituo saba ni vya nje ya nchi Bujumbura Burundi, Entebbe Uganda, Hahaya Comoro, Harare Zimbabwe, Johannesburg Afr

Mwanamume afurushwa kwenye ndege ya Marekani kwa kuvalia mask ya gesi

Picha
Mwanamume mmoja ametimuliwa kwenye ndege ya Marekani kwa kuvalia mask ya gesi baada ya abiria wenzake kuingiwa na hofu, Vyombo vya habari vya Texas vinaripoti. Mwanamume huyo alikuwa amevalia mask na kuabiri ndege ya shirika la ndege la Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka Houston kuenda Dallas siku ya Alhamisi. Wahudumu wa ndege hiyo walimuomba atoe mask hiyo baada ya abiria wenzake kuanza kulalamika, lakini alikataa kufanya hivyo katika hatua ambayo ilisababisha ndege hiyo kucheleweshwa kwa karibu saa moja. Mwanamume huyo alikatiwa tiketi ya kusafiri na ndege nyingine ambayo aliabiri bila hiyo mask. Nilimuona mtu akija kupanda ndege akiwa amevalia mask kamili ya gesi, hali ambayo kwa kweli si ya kawaida," abiria Joseph Say aliambia kituo cha Hauston ABC, KTRK. "Mara baada ya hapo, watu waliokuwa kwenye viti vya nyuma walianza kuhoji hatua hiyo ,"alisema. "Haungeliona uso wake. Haungeliweza kumtambua ni nani. Watu walikuwa na hofu huenda ameingiza kisir

Tanzania yapigwa marufuku bahati nasibu ya viza Marekani

Picha
Serikali ya Marekani imepiga marufuku raia wa Tanzania kushiriki katika bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani. Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya serikali ya Trump kumpiga marufuku Bahati nasibu hiyo hutoa viza kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani. Nchi ya Sudani pia raia wake wamepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo. Wakati huo huo raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani. Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan. Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa. Afisa wa ngazi ya juu nchini Marekani amesema kuwa nchi hizo sita zimeshindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa". "Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mwali zimefeli kufikia viwango vya chi