Vita vya Ukraine: Putin asema Urusi kupeleka vichwa vya nyuklia Belarus ni onyo kwa Magharibi

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Rais Vladimir Putin amesema kwamba upelekaji wake wa silaha za kimkakati za nyuklia huko Belarus, jambo ambalo alithibitisha kwa mara ya kwanza tayari limetokea, ni ukumbusho kwa Magharibi kwamba haiwezi kuisababishia Urusi mkakati wa kushindwa.

Akizungumza katika kongamano kuu la kiuchumi la Urusi huko St Petersburg, Putin alisema vichwa vya kimkakati vya nyuklia vya Urusi tayari vimewasilishwa kwa mshirika wa karibu Belarus, lakini alisisitiza kuwa haoni haja ya Urusi kutumia silaha za nyuklia kwa sasa.

"Kama unavyojua tulikuwa tukijadiliana na mshirika wetu, (Rais wa Belarus (Alexander) Lukashenko, kwamba tungehamisha sehemu ya silaha hizi za nyuklia kwenye eneo la Belarus - hii imetokea," Putin alisema.

"Vichwa vya kwanza vya nyuklia viliwasilishwa katika eneo la Belarus. Lakini zile za kwanza tu, sehemu ya kwanza. Ila tutafanya kazi hii kikamilifu mwishoni mwa msimu wa joto au mwishoni mwa mwaka."

Hatua hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Moscow kupeleka vichwa hivyo - silaha za nyuklia za masafa mafupi zaidi ambazo zingeweza kutumika katika uwanja wa vita - nje ya Urusi tangu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti ilikusudiwa kuwa onyo kwa nchi za Magharibi kuhusu kuipatia silaha na kuunga mkono Ukraine, kiongozi wa Urusi alisema.

Putin aliongeza kuwa hatua hiyo inahusu "kuzuia" na kumkumbusha yeyote "anayefikiria kutushinda kimkakati".

Silaha za kimkakati za nyuklia ni vichwa vidogo vya nyuklia na mifumo ya uwasilishaji inayokusudiwa kutumiwa kwenye uwanja wa vita, au kwa mashambulizi madogo.

Vimeundwa ili kuharibu malengo ya adui katika eneo mahususi bila kusababisha athari ya mionzi iliyoenea.

Silaha ndogo zaidi za kimbinu za nyuklia zinaweza kuwa kilotoni moja au chini ya hapo (kuzalisha sawa na tani elfu moja za TNT inayolipuka).

Kubwa zaidi inaweza kuwa na kilo 100. Kwa kulinganisha, bomu la atomiki ambalo Marekani ilidondosha Hiroshima mnamo 1945 lilikuwa kilotoni 15.

Kiongozi huyo wa Urusi anatarajiwa kukutana na viongozi wa Afrika mjini St Petersburg baada ya kuzuru Kyiv siku ya Ijumaa kama sehemu ya mpango wa amani wanaowasilisha kwa nchi zote mbili.

Hata hivyo, wakiwa katika mji huo kulitokea mashambulizi ya makombora ya Urusi.

Belarus ni mshirika mkuu wa Urusi na ilitumika kama njia ya uzinduzi wa uvamizi kamili wa Bw Putin nchini Ukraine mnamo Februari mwaka jana.

Putin asema Magharibi inataka ishindwe kimkakati

Marekani imekosoa uamuzi wa Putin lakini imesema haina nia ya kubadilisha msimamo wake kuhusu silaha za kimkakati za nyuklia na haijaona dalili zozote kwamba Urusi inajiandaa kutumia silaha za nyuklia.

Hatua hiyo ya Urusi hata hivyo inafuatiliwa kwa karibu na Washington na washirika wake pamoja na China, ambayo imeonya mara kwa mara dhidi ya matumizi ya silaha za nyuklia katika vita vya Ukraine.

Putin alisema nchi za Magharibi zinafanya kila liwezalo kuhakikisha Urusi inashindwa kimkakati nchini Ukraine ambako Urusi inaendeleza vita vikali zaidi katika ardhi ya barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia baada ya kuvamia jirani yake mwaka jana katika kile ilichokiita "operesheni maalum ya kijeshi."

Lakini Urusi haikuwa na haja ya kutumia silaha za nyuklia kwa sasa, alisema Putin, akiashiria hakuna mabadiliko katika suala la nyuklia kwa Moscow ambayo inatazamia tu kuchukua hiyo ikiwa kuwepo kwa taifa la Urusi kunatishiwa.

"Silaha za nyuklia zimetengenezwa ili kuhakikisha usalama wetu kwa maana pana na uwepo wa serikali ya Urusi, lakini sisi...hatuna haja hiyo (ya kuzitumia)," Putin alisema.

Lakini aliongeza kuwa mazungumzo na nchi za Magharibi kupunguza hazina kubwa ya silaha za nyuklia za Urusi, kubwa zaidi duniani, hayakuwa ya msingi.

"Kuzungumza tu juu ya hili (matumizi ya uwezekano wa silaha za nyuklia) kunapunguza kiwango cha nyuklia. Tuna zaidi ya zile za nchi za NATO na wanataka kupunguza idadi ya kwetu," alisema Putin.

Viongozi wa Afrika Ukraine

.

CHANZO CHA PICHA,SOUTH AFRICAN PRESIDENCY

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza huko Ukraine, alitoa wito wa pande zote mbili kusitisha mashambulizi na kuwezesha mazungumzo ya amani.

"Tulikuja hapa kusikiliza na kutambua kile watu wa Ukraine wamepitia," alisema.

Lakini Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema badala ya kufanya mazungumzo ya kidiplomasia kwa Urusi, inapaswa kuzuiwa kidiplomasia ili kutuma ujumbe kwamba jumuiya ya kimataifa inashtumu uvamizi wake.

Kyiv haitaingia kwenye mazungumzo na Moscow wakati ingali inamiliki eneo la Ukrain, Bw Zelensky alisema.

Bw Putin pia alirudia madai yake kwamba Ukraine haikuwa na nafasi ya kufanikiwa katika mashambulizi yake yanayoendelea.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?