​Matumaini ya usitishaji vita siku ya Eid nchini Sudan yanafifia huku milio ya risasi ikisikika

.

Usitishaji vita wa siku moja uliotangazwa na pande zote mbili zinazopigana katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kwa ajili ya sikukuu ya Eid al-Adha, unaonekana kufifia

Mfanyakazi wa kukabiliana na dharura, Duaa Tariq, aliiambia BBC kwamba milio mikubwa ya risasi imesikika katika wilaya za kaskazini mwa jiji tangu asubuhi na mapema.

Siku ya Jumanne mkuu wa vikosi vya jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, alitoa wito kwa vijana kuungana na kupigana na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).

Lakini Bi Tariq alisema RSF ndio nguvu kubwa katika jiji hilo, ikimiliki nyumba, masoko na mitaa.

Makubaliano ya awali katika mzozo wa wiki 10 yameafikiwa vibaya vile vile.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga