Je unajua cha kufanya mtoto wako anapokakamaa? Degedege na dhana potofu inayoizunguka

Ukuaji wa kila mtoto unatofautiana haijalishi ni wangapi umelea au uliobarikiwa nao kama mzazi.

Kila mtoto hukua kivyake na hakuna vile unavyoweza kusema kwamba aliyetangulia nilimfanyia hivi na naye huyu nitamfanyia vivyo hivyo.

Katika makala hii, tunaangazia moja ya hali ambazo zinaweza kuwa changamoto kwa mzazi wakati inapomkumba mtu wako lakini hasa kwa watoto.

Hali hii inafahamika kama degedege ambayo humfanya mtu kuanza kutetemeka mwili, kupoteza fahamu, au hata mdomo na macho kuanza kucheza cheza.

Tunachanganua hii ni hali gani? chanzo chake na tiba ya kwanza kwa mgonjwa tukiwa na daktari wa watoto na mwananurolojia yaani mtaalam wa neva Dkt. Yusuf Jamnagerwalla kutoka Tanzania.

Mara nyingi watu huchanganya degedege na kifafa lakini kulingana na daktari Jamnagerwalla ni hali mbili tofauti kama anavyosema.

“Degedege haifanani na kifafa, hapana, hiyo si kweli. Degedege zote sio kifafa lakini kifafa ni ugonjwa wa degedege”.

Anachomaanisha daktari Jamnagerwalla ni kwamba unaweza kupata degedege sababu isiwe eti ni ugonjwa wa kifafa, hapana, badala yake ikawa ni kwa sababu nyingine kwa mfano kama umepungukiwa glukosi kwenye mwili, pengine shida ya madini fulani, kama ini au figo imefeli, kama una kiharusi na sio lazima degedege hizo zitageuka na kuwa kifafa.

Visababishi vya degedege kwa watoto

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

• Kuwa na joto la kiwango cha juu (zaidi ya selsiasi 38)

• Pengine kama mtoto aliumia ubongo wakati akiwa bado tumboni

• Au kama alikosa oksijeni wakati mama anajifungua. Na hali hii inaweza baadaye kugeuka na kuwa kifafa

• Akipata maambukizi yakaingia kwenye ubongo, mfano, kupata ajali.

Dalili jumla za degedege

  • Unaweza kumuona mtoto ametoa jicho anaangalia juu tu, au ukaona shingo yake ni kama inageuka isivyo kawaida, inapinde vile
  • Mtoto anaweza kukakamaa kabisa au akageuka tu upande mmoja na akasalia hivyo
  • Mtoto anaweza kupoteza fahamu kabisa
  • Mtoto kuwa na hisia za kupitiliza kama kucheza au kulia sana, furaha isiyo ya kawaida, hofu au hata uwoga
  • Mtu anaweza kuanza kuzungumza mambo yasiyoeleweka hata ukahisi kama akili yake imeanza kuwa na matatizo
  • Kuchezesha macho, kutoa nyute, mate au hata povu
  • Misuli kukakamaa, inaishiwa na nguvu na kupelekea kuanguka
  • Lakini pia anaweza kutokewa na dalili zingine

Daktari Jamnagerwalla anasema asilimia kubwa ya watoto kuanzia umri wa miezi 5 hadi miaka 5 au 6. Wanapata degedege ya homa kali.

Na wakati joto linaongezeka kwa kasi mwilini, kuna uwezekano mkubwa mtoto akapata degedege, lakini pia huwezi kuhitimisha kwamba moja kwa moja mtoto atapata kifafa.

Daktari anafafanua kuwa: “Degedege inaweza kuwa kiwango fulani cha kifafa ikiwa tu degedege inajirudia zaidi ya mara mbili ndani ya saa 24”.

Aina nne kuu za degedege kwa watoto

Mtoto anaweza kupiga kelele na kuanza kulia na ghafla akaanza kuchezesha macho au yakaenda juu, kisha ataanza kukakamaa na kutetemeka viungo vyote vya mwili na wakati huo akapoteza fahamu kabisa.

Mara nyingi hali hii inatokea kwa dakika mbili au tatu na inapozidi dakika 5, hiyo inakuwa ni hatari kwa maisha ya mtoto. Aina hii ya degedege kwa kiingereza inajulikana kama ‘Generalized tonic-clonic seizure’.

Aina ya pili, sehemu ya nusu ya mwili wa mgonjwa aidha itakakamaa au itacheza cheza. Kwa kiingereza inajulikana kama focal seizure. Katika aina hii ya degedege, sio lazima mtu apoteze fahamu.

Aina ya tatu ya degedege, unakuta mtoto au mtu mzima ghafla anatulia, yaani kama akili inasimama kidogo. Pengine kwa sekundę 20 au 30. Daktari Jamnagerwalla anasema ‘’Mwalimu anaweza kusema mtoto hana makini darasani lakini ukweli ni kwamba kipindi hicho huwa amepoteza fahamu na hatambui kilichotokea.” Aina hii ya degedege inafahamika kama absence seizure.

Atonic seizure ni aina nyingine ambapo ghafla misuli hulegea na mtu anadondoka. Hii inasemekana kuwa hatari sana kwa watoto kwa sababu akianguka anaweza kuumia kwenye ubongo au hata kupata majeraha kutokana na vitu vilivyokaribu naye.

Hisia ya mzazi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?