Tetesi za soka jumatatu 05.06.2023


Manchester City wanatumai kuwa jaribio lao la kushinda mataji matatu litamshawishi mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 22, kusaini mkataba wa muda mrefu zaidi na kuzuia nia ya Real Madrid kumsajili nyota huyo (Telegraph - usajili unahitajika))

Real Madrid tayari imefanya mawasiliano na Tottenham na Harry Kane kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza, 29, kama mbadala wa mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Karim Benzema, 35, ambaye amethibitisha kuondoka Real msimu huu. (Marca kwa Kihispania)

Real wanakaribia kukubali "mkataba mkubwa" wa kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz, 23, kutoka Chelsea . (Bild - kwa Kijerumani)

th

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Karim Benzema sasa anatarajiwa kujiunga na mabingwa wa Saudia Al-Ittihad kwa kandarasi ya miaka miwili. (Al-Ekhbariya, kupitia L'Equipe)

Manchester United wanapanga kutoa ofa ya pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa kati wa England Mason Mount, 24, kutoka Chelsea na wataishinikiza Tottenham kumuuza Kane - lakini wanaamini kumsajili nahodha huyo wa Uingereza "hakuwezekani". (Telegraph - usajili unahitajika)

Ofa ya Inter Miami ya kutaka kumsajili fowadi wa Argentina Lionel Messi, 35, atakapoondoka Paris St-Germain msimu huu wa joto inajumuisha mikataba na chapa kama vile Apple na Adidas, lakini ina thamani ndogo kuliko ofa yake nyingine kutoka Saudi Arabia. (Guillem Balague)

TH

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Crystal Palace wamempa Wilfried Zaha, 30, karibu pauni 150,000 kwa wiki ili kusaini mkataba mpya - chini ya kile ambacho klabu ya Qatar Al Sadd imempa fowadi huyo wa Ivory Coast, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwezi huu(Sun)

Paris St-Germain wanamlenga kocha wa zamani wa Bayern Munich , Julian Nagelsmann kuwa ili kuchukua nafasi ya Christophe Galtier kama kocha - huku mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry akiwa msaidizi wake. (FootMercato - kwa Kifaransa)

Chelsea wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Manuel Ugarte, 22, kutoka Sporting Lisbon kwa kukubali kulipa zaidi ya kifungu cha kiungo cha Uruguay cha pauni milioni 52. (Record - Kwa Kireno)

TH

CHANZO CHA PICHA, PA MEDIA

Arsenal watawasilisha ombi la kumnunua Declan Rice baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 24, kuichezea West Ham katika fainali ya Ligi ya Europa, lakini Bayern Munich pia wanavutiwa. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamepanga kuchuana na Barcelona kwa ajili ya kumsaini kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kutoka Fiorentina . (Sport - kwa Kihispania)

Mchezaji wa Brighton Moises Caicedo amekubali masharti ya kibinafsi na Arsenal , ingawa Chelsea wako tayari kulipa ada ya juu ya uhamisho wa kiungo huyo wa Ecuador, 21. (Teradeportes, via Mirror).

Everton wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst, 30, atakaporejea Burnley kutoka kwa muda wake wa mkopo Manchester United . (talkSPORT)

West Ham na Burnley wanavutiwa na mshambuliaji wa Strasbourg na Senegal Habib Diallo, 27. (Mail)

Chelsea itadai zaidi ya pauni milioni 20 ili kumuuza Ian Maatsen msimu huu wa joto, huku Burnley wakiwa na nia ya kutaka kumnunua beki huyo wa kushoto wa Uholanzi, 21, baada ya kuwasaidia kushinda taji la Ubingwa wakiwa kwa mkopo msimu uliopita. (Standard)

th

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Kocha wa Italia na meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini ni miongoni mwa wagombea kuchukua mikoba ya mabingwa wa Italia Napoli . (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Rangers wako wazi kumsajili mlinda mlango wa zamani wa England Jack Butland, 30, baada ya Crystal Palace kupitisha nafasi ya kuongeza mkataba wake baada ya kucheza kwa mkopo Manchester United . (Sun)

Kocha wa zamani wa Leeds, Jesse Marsch yumo kwenye orodha ya walioteuliwa na Monaco kuwa kocha wao mpya baada ya kumfukuza Mbelgiji Philippe Clement. (Nicolo Schira)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?