Kuna uwezekano wa kuanza kupatikana tena kwa vifaru

 

  1. Image caption: Wanyama hao wameletwa kutoka Afrika Kusini (picha ya kumbukumbu)

    Vifaru 16 weupe wa kusini wamepewa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la kuwarejesha wanyama hao walio hatarini kutoweka.

    Walisafirishwa kutoka kwa hifadhi ya kibinafsi nchini Afrika Kusini hadi mbuga ya kitaifa ya Garamba kaskazini-mashariki mwa DR Congo.

    Faru mweupe wa mwisho katika eneo hilo aliuawa mwaka wa 2006.

    Afisa mmoja alisema juhudi za kuokoa viumbe hao "zimekuwa ndogo sana, zimechelewesha sana", na kuelezea faru weupe wa kusini kama mbadala wake wa karibu zaidi wa vinasaba.

    Migogoro na uwindaji-haramu nchini DR Congo umesababisha idadi ya wanyamapori kupungua.

  2. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo

  3. Vita vya Ukraine: Urusi yachukua hatua ya kudhibiti kundi la Wagner

    .

    Urusi inaonekana kuchukua hatua ya kudhibiti kundi la Wagner, baada ya miezi kadhaa ya mapigano kati ya maafisa wa ulinzi na kundi hilo la kibinafsi la kijeshi.

    Naibu Waziri wa Ulinzi Nikolai Pankov alisema Jumamosi "makundi ya kujitolea" yataombwa kutia saini mikataba moja kwa moja na wizara ya ulinzi.

    Taarifa hiyo isiyoeleweka inaaminika kuwa inalenga kundi hilo.

    Lakini katika taarifa iliyoonyesha kukasirika siku ya Jumapili, bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alisema vikosi vyake vitasusia kandarasi hizo.

    Kundi la kijeshi la kibinafsi limekuwa na jukumu kubwa katika vita vya Ukraine, likipigana upande wa vikosi vya Urusi.

    Lakini Prigozhin, ambaye anasemekana kuwa na malengo yake ya kisiasa, amekuwa katika mzozo wa hadharani na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na mkuu wa kijeshi Valery Gerasimov kwa miezi kadhaa.

    Lakini Prigozhin, ambaye anasemekana kuwa na malengo yake ya kisiasa, amekuwa katika mzozo wa hadharani na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na mkuu wa kijeshi Valery Gerasimov kwa miezi kadhaa.

    Amewashutumu mara kwa mara wawili hao kwa kutokuwa na uwezo na kwa makusudi kupunguza vitengo vya Wagner vinavyopigana nchini Ukraine.

    "Wagner hatatia saini mikataba yoyote na Shoigu," Prigozhin alisema akijibu ombi la maoni yake kuhusu tangazo la wizara ya ulinzi.

    "Shoigu hawezi kusimamia vizuri masuala ya kijeshi."

    Alisisitiza kuwa kundi lake liliunganishwa vyema na jeshi la Urusi, lakini akasema kwamba ufanisi wake utatiwa doa kwa kuripoti kwa waziri wa ulinzi.

    Ingawa tangazo la Jumamosi halikumrejelea moja kwa moja Wagner au vikundi vingine vya kijeshi, vyombo vya habari vya Urusi vilipendekeza kuwa mikataba hiyo mipya ilikuwa ni hatua ya kumdhibiti Prigozhin na vikosi vyake.

    Lakini wizara ya ulinzi ilisema hatua hiyo iliundwa ili "kuongeza ufanisi" wa vitengo vya Urusi vinavyopigana nchini Ukraine.

    Pia unaweza kusoma:

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?