​Kiongozi wa kijeshi wa Sudan awafuta kazi magavana wa majimbo mawili

 
Image caption: Mapigano kati ya vikosi hasimu yameongezeka nchini Sudan


Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amechukua nafasi ya magavana wawili wa majimbo, shirika jipya la serikali la Suna limeripoti.

Haya yanajiri wakati mapigano kati ya vikosi hasimu vya kijeshi yakiendelea katika mji mkuu, Khartoum, na maeneo mengine.

Viongozi wawili wa kijeshi walichukua mamlaka katika mapinduzi ya Oktoba 2021 lakini sasa wanashiriki katika vita vya kuwania madaraka.

Jenerali Burhan alimfukuza kazi gavana wa jimbo la Kordofan Kaskazini Fadlallah Mohamed Ali al-Tom, na Al-Alim Ibrahim al-Nour wa jimbo la Sennar. Magavana wasimamizi wameteuliwa.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kuelezea kilichochangia kufurushwa kwao.

Maeneo ya Kordofan Kaskazini yameshuhudia vita vikali kati ya pande zinazozozana ingawa hakujakuwa na mapigano katika jimbo la Sennar.

Takriban raia 883 wameuawa na wengine zaidi ya 3,800 kujeruhiwa tangu mzozo huo ulipozuka tarehe 15 Aprili.

Pia unaweza kusoma:

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?