Kampuni ya Johnson & Johnson yashtakiwa kwa kuwauzia Wakenya poda za watoto
Accessibility links
Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Kenya limeshtaki shirika la kimataifa la Marekani Johnson & Johnson juu ya kuuzia Wakenya poda ya ulanga.
Shirika la African Centre for Corrective and Preventive Action limesema kuwa ingawa bidhaa hiyo ilipigwa marufuku katika nchini kama vile za Bara Ulaya na India bado inauzwa nchini Kenya.
Katika ombi lililowasilishwa lenye kuangazia kulinda haki ya mnunuzi, shirika hilo linadai kuwa kampuni ya Johnson & Johnson linatumia benzene na talc kwenye bidhaa zake za poda ya watoto.
Shirika hilo linadai kuwa benzene na talc inasababisha saratani kwa binadamu na kuwa ‘’ talc yenye madini ya asbesto husababisha madhara makubwa kwa mtumiaji wake.’’
Pia unaweza kusoma:
Johnson & Johnson kutumia wanga wa mahindi badala ya ulanga kutengeneza poda
Rais Volodymy Zelensky amesema vikosi vya Ukraine "vinaongeza udhibiti" katika eneo karibu na Bakhmut kupitia ujumbe wake wa kawaida wa njia ya video.
Aliongeza "anashukuru sana" kwa hatua inayopigwa na wanajeshi wake karibu na jiji la mashariki.
Bakhmut inajulikana kama eneo ambalo limekumbwa na vita kwa muda mrefu zaidi na pengine umwagaji damu zaidi katika vita hivyo.
Wizara ya ulinzi pia ilisema jana kwamba vikosi vyake vimesonga mbele "mita 250 hadi 700" kuelekea jiji hilo.
Hata hivyo, BBC haijaweza kuthibitisha kwa uhuru madai ya yanayoendelea vitani.
Soma zaidi:
Vita vya Ukraine: Kipi kinahitajika kwa vikosi vya Ukraine kurudisha mapigo?
Mtikiso wa ndege kwenye anga umeongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa iliyofanya sayari kuwa na joto, watafiti wanasema.
Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Reading nchini Uingereza wamechunguza msukosuko wa hewa safi, ambao ni vigumu kwa marubani kuuepuka.
Waligundua kuwa msukosuko mkali umeongezeka kwa 55% kati ya 1979 na 2020 kwenye njia ya kawaida ya Atlantiki ya Kaskazini yenye shughuli nyingi.
Wanasema hilo ni kutokana na mabadiliko ya kasi ya upepo kwenye miinuko kwasababu ya hewa joto kutoka kwa uzalishaji wa kaboni.
"Kufuatia muongo mmoja wa utafiti unaoonyesha kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yataongeza mtikisiko siku zijazo, sasa tuna ushahidi unaoonyesha kwamba ongezeko hilo tayari limeanza," alisema Prof Paul Williams, mwanasayansi wa anga katika Chuo Kikuu cha Reading ambaye alishiriki katika utafiti.
"Tunapaswa kuwekeza katika mifumo iliyoboreshwa ya utabiri na ugunduzi wa misukosuko, ili kuzuia hali mbaya ya hewa kutafsiri kuwa safari za ndege zisizo na mashiko katika miongo ijayo.
"Njia za ndege nchini Marekani na Atlantiki ya Kaskazini zilishuhudia ongezeko kubwa zaidi.
Ulaya, Mashariki ya Kati, na Atlantiki ya Kusini pia ilishuhudia ongezeko kubwa la misukosuko.
Prof Williams alisema msukosuko huo ulioongezeka ulitokana na tofauti kubwa ya upepo - katika mkondo wa ndege, mfumo wa upepo mkali unaovuma kutoka magharibi hadi mashariki, takriban maili tano hadi saba juu ya uso wa Dunia.
Inapatikana kwa kiasi kikubwa kutokana na tofauti ya joto kati ya ikweta ya dunia na ncha.
Ingawa satelaiti haziwezi kuona msukosuko huo, zinaweza kuona muundo na umbo la mkondo wa ndege, na hivyo kuruhusu kuchanganuliwa.
Rada inaweza kupata misukosuko kutokana na dhoruba, lakini mtikisiko wa anga iliyo wazi hauonekani na ni vigumu kutambua.
Safari za ndege zenye misukosuko sio tu za kusumbua, lakini pia zinaweza kusababisha majeraha kwa wale walio kwenye ndege.
Msukosuko mkali ni nadra sana, lakini mtikisiko wa anga iliyo wazi unaweza kutokea wakati abiria hawajafungwa.
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 29 jela mwanamke wa Kijiji cha Lumuli, Desderia Mbwelwa (57) kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na kumsababishia magonjwa ya zinaa.
Kuingana na gazeti la Mwananchi, Siku ya tukio mwanamke huyo alimkuta mtoto ambaye ni mwathirika wa tukio hilo akiwa anachunga ng'ombe kisha akamuuliza wenzake wako wapi na alipojibiwa kuwa wenzake hawapo ndipo akambaka akiwa chini ya mti.
Kesi hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Said Mkasiwa na ilikuwa na mashahidi watano akiwemo daktari aliyempima mtoto na kuthibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa na michubuko na aliambukizwa magonjwa ya zinaa kutokana na kutokwa uchafu eneo la haja ndogo.
Mahakama ilimpa nafasi ya kujitetea, Desderia amesema yeye ni mtu mzima na kuwa ana watoto na wajukuu wanaomtegemea, ndipo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka 29 jela kwa kosa la ukatili wa kingono kwa mtoto wa miaka 8 pamoja na kumsababishia magonjwa ya zinaa.
Hata hivyo Wakili wake, Frank Mwela amesema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kuwa mteja wake hakupimwa ili kubaini kama kweli ana magonjwa hayo ya zinaa.
"Mteja wangu hakupimwa kuonekana na magonjwa hayo ambayo mteja wangu na shahidi wake wamethibitisha kuwa wao magonjwa hayo hawana kwa sababu shahidi mmoja wapo ni mume wake," amesema.
Bosi mpya wa kampuni ya mitandao ya kijamii ya Twitter, Linda Yaccarino, ameelezea mipango yake ya "Twitter 2.0.", baada ya kuchukua nafasi ya Elon Musk wiki moja iliyopita.
Anasema kampuni hiyo "iko kwenye dhamira ya kuwa chanzo sahihi zaidi cha habari za wakati halisi duniani".
Tangu Bw Musk anunue Twitter mwaka jana, imekabiliwa na ukosoaji kuhusu mbinu yake ya kukabiliana na taarifa potofu.
Katika mwezi uliopita, kampuni ilipoteza kiongozi wake wa kuaminiwa na usalama na kujiondoa kwenye kanuni za upotoshaji za EU.
Katika mfululizo wa ujumbe wa Twitter, ambazo pia zilitumwa kwa wafanyikazi, Bi Yaccarino aliunga mkono lengo la Bw Musk, kwamba Twitter lazima ilete mapinduzi ya "kitaifa".
Alisema hii itasaidia "kusogeza mbele ustaarabu kupitia ubadilishanaji wa habari usiochujwa na mazungumzo ya wazi kuhusu mambo ambayo ni muhimu zaidi kwetu."
"Watumiaji wanahitaji kujua kwamba ulimwengu hauna upendeleo," Ray Wang, afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya utafiti yenye makao yake mjini Silicon Valley ya Constellation aliiambia BBC.
Bw Musk, ambaye anajiita "mtetezi wa uhuru wa kujieleza", amekosoa sera za Twitter kuhusu kudhibiti maudhui, akisema kwamba inahitajika kuwa jukwaa la kweli la uhuru wa kujieleza.
Lakini hatua zake za kurejesha akaunti za mrengo wa kulia, ambazo maoni yake ameshiriki, na kulegeza udhibiti zimewafukuza wateja wanaotangaza biashara zao.
Mnamo Desemba, mapato yaliripotiwa kupungua kwa 40% hadi mwaka uliopita.
Ili wateja warudi, wanahitaji kujua nini cha kutarajia kuhusu maudhui ya mtumiaji na uhusika wake, Bw Wang alisema.
"Bila shaka yeye ni mtu anayeweza kumkabili Elon kwa kumueleza uhalisia wa mambo na kwenda naye unyo unyo kwa jinsi anavyomheshimu," aliongeza.
Marekani ina wasiwasi kwamba huenda Korea Kaskazini inapanga kusafirisha silaha zaidi hadi Urusi baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuapa kuimarisha uhusiano na Moscow.
Siku ya Jumatatu, Kim Jong-un, katika telegramu kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa Siku ya Urusi, "alithibitisha utayari wake wa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya DPRK na Shirikisho la Urusi."
"Comrade Kim Jong-un alibainisha kuwa watu wetu wanaonyesha uungaji mkono wao kamili na mshikamano kwa watu wa Urusi, ambao wanajitahidi kutekeleza kazi takatifu ya kulinda haki za uhuru na maslahi ya maendeleo ya Urusi, utekelezaji wa haki ya kimataifa dhidi ya utashi na jeuri ya mabeberu," Shirika la Central Telegraph la Korea linanukuu telegram ( KCNA).
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, alinukuliwa na Reuters, akisema kuwa licha ya Pyongyang kukataa kuiuzia Urusi silaha kwa vita vya Ukraine, Washington ilithibitisha kuwa DPRK ilikamilisha usambazaji wa silaha kwa Wagner PMC mnamo Novemba 2022.
"Tuna wasiwasi kwamba DPRK inapanga kuipatia Urusi vifaa vingi vya kijeshi," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema.
Mwezi Machi, Marekani ilisema ilikuwa na taarifa mpya kuhusu majaribio ya Urusi ya kupata silaha kutoka Korea Kaskazini kwa kubadilishana na msaada wa chakula.
Paris St-Germain iko tayari kumuuza Kylian Mbappe msimu huu wa joto badala ya hatari ya kumpoteza bila malipo katika muda wa mwaka mmoja, baada ya kuiambia klabu hiyo ya Ufaransa kuwa hataongeza mkataba wake.
Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa Ufaransa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.
Kulikuwa na makataa ya Julai 31 kwa Mbappe, 24, kuiambia PSG kama angepanga kusajili upya mkataba hadi 2025.
Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, ameitumia klabu hiyo barua akisema hatofanya hivyo.
Mfungaji huyo bora wa PSG atakuwa huru kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu ujao na hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya kufanya mazungumzo.
Hata hivyo, wakati mabingwa hao wa Ufaransa wakijaribu kurekebisha sera ya michezo kwa timu yao baada ya miaka mingi ya kununua wachezaji nyota bila mkakati madhubuti, PSG wameazimia kutomwacha Mbappe kwenda bure, huku klabu hiyo ikikerwa na barua ya mchezaji huyo iliyovujishwa kwenye vyombo vya habari kwanza kabla ya wao kuiona.
Ina maana kwamba wasipopata hakikisho kuhusu nia ya baadaye ya mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, watamuuza katika hatua ambayo itaweka vilabu vinavyoongoza barani Ulaya kuwa macho.
Real Madrid wanamtamani kwa muda mrefu Mfaransa huyo na alikataa kuhamia Bernabeu kusalia PSG mwaka jana.
Kuondolewa kwa Karim Benzema kwenda Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real inahitaji mshambuliaji, ingawa ilifikiriwa kuwa Harry Kane wa Tottenham alikuwa kileleni mwa orodha yao.
Mbappe, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017 kwa mkopo akitokea Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m na amefunga mabao 212 katika michezo 260.
Ana mabao 38 katika mechi 68 alizoichezea Ufaransa, ikiwa ni pamoja na mabao matatu kwa mpigo katika fainali ya mwaka jana nchini Qatar, Ufaransa iliposhindwa na Argentina kwa mikwaju ya penalti.
Mbappe alimaliza kama mfungaji bora wa Ligue 1 katika kila misimu mitano iliyopita na ameshinda mataji matano ya ligi katika misimu yake sita akiwa PSG.
PSG ilimaliza msimu wa 2022-23 kwa kutwaa taji la Ligue 1 pekee baada ya kushindwa tena kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, na kufungwa na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora.
Mbappe atakuwa mshambuliaji wa pili mwenye hadhi ya juu kuondoka Parc des Princes msimu huu, baada ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kuondoka mwishoni mwa kandarasi yake ya miaka miwili na kujiunga na Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka.
Neymar, mchezaji wa tatu wa safu ya mbele ya nyota wa PSG msimu uliopita, amekuwa akihusishwa na kuhamia Saudi Arabia kwa kitita cha pesa nyingi.
Soma zaidi:
Waombolezaji katika mazishi ya mwanamke mzee wa Ecuador walishtuka kugundua kuwa bado yu hai.
Bella Montoya, 76, alitangazwa amefariki wiki iliyopita kufuatia kile kinachoshukiwa kuwa kiharusi.
Saa tano usiku wa kuamkia Ijumaa, jamaa wakijiandaa kubadilisha nguo zake kabla ya mazishi walimpata akihema.
Bi Montoya sasa amerejeshwa hospitalini akiwa katika uangalizi mahututi, na wizara ya afya ya Ecuador imeunda kamati kuchunguza tukio hilo.
Katika taarifa, wizara hiyo ilisema kwamba mwanamke huyo alipatwa na mshtuko wa moyo – awaka hawezi kupumua na matatizo ya moyo - na hakuonyesha dalili za kuamka wakati wa majaribio ya kumsaidia kupata tena fahamu.
Daktari wa zamu alithibitisha kifo chake.
Mwanawe, Gilber Rodolfo Balberán Montoya, alinukuliwa na vyombo vya habari vya ndani akisema kwamba mama yake "alilazwa mwendo wa 09:00 asubuhi na saa sita mchana daktari aliniambia [amefariki]".
Kisha Bi Montoya aliwekwa kwenye jeneza kwa saa kadhaa hadi alipoonekana na wanafamilia akijaribu kupumua.
Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha akiwa amelala kwenye jeneza lililo wazi na akipumua kwa nguvu huku watu kadhaa wakiwa wamemzunguka.
Wahudumu wa afya kisha wanaonekana wakiwasili na kuanza kumfuatilia Bi Montoya kabla ya kumsogeza kwenye machela na kumuingiza kwenye gari la wagonjwa.
Sasa yuko katika uangalizi mahututi katika hospitali hiyo hiyo ambapo madaktari walitangaza kifo chake.
Shirika la habari la AFP lilimnukuu Bw Balberán akisema: "Kidogo kidogo ninaelewa kilichotokea. Sasa ninaombea tu afya ya mama yangu iendelee kuimarika. Namtaka awe hai na awe kando yangu."
Maoni
Chapisha Maoni