Mswati wa III wa Eswatini ndiye Mfalme wa mwisho kabisa barani Afrika.

Mahakama nchini Eswatini imewapata wabunge wawili na hatia ya mauaji na ugaidi kwa jukumu lao katika wimbi la maandamano yaliyoikumba nchi hiyo mwaka wa 2021. 

Mduduzi Bacede Mabuza na Mthandeni Dube wanakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela. 

Wawili hao walizuiliwa baada ya kushiriki katika maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika kile ambacho ni utawala wa mwisho kabisa wa kifalme barani Afrika. 

Hata hivyo, walikana mashtaka ya kuchochea machafuko. 

Amnesty International ilisema hukumu hizo ni ushahidi wa kuendelea kuwakandamiza wapinzani. 

Vikosi vya usalama vilitumia nguvu kupita kiasi katika maandamano hayo na kusababisha makumi ya watu kuuawa. 

Eswatini imekuwa ikiongozwa na Mfalme Mswati III tangu 1986 na vyama vya kisiasa vimepigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi.

Waandamanaji, waliokasirishwa na kuzorota kwa uchumi, wamezidi kupaza sauti kutaka mageuzi ya kisiasa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?