Mzozo wa Ethiopia: Ndani ya mji wa Makelle uliotengwa na ulimwengu


Wiki iliyopita Ethiopia ilifikia makubaliano ya kuruhusu kupelekwa kwa misaada eneo la Tigray Kaskazini. Kumekuwa na matumaini kuwa huenda mzozo huo wa miezi 17 ukaisha.

Eneo hilo limekosa misaada kwa miezi mingi na kusababisha mamilioni ya wakazi kukosa chakula na matumizi muhimu.

Mkazi wa mji mkuu wa Tigray Mekelle ambao upo chini ya waasi wa TPLF ameiambia Newsday Swahili ya Maisha eneo hilo.

Kupata mahitaji muhimu imekua chanzo cha mawazo.

Wengi wetu tunapata tatizo hili na pesa imekua adimu.

Unaweza pia kusoma

Sijaweza kutumia akaunti yangu tangu mwezi juni mwaka jana na badala yake nimekua nikikopa kutoka kwa ndugu na jamaa hapa ili niweze kununua chakula kwa ajili ya familia.

Ndugu kutoka nje pia wanataka kusaidia lakini simu zote na mtandao imezimwa, na haiwezekani kuzungumza nao.

Na gharama ya chakula pia imepanda sana, Unga wa ngano na mafuta ya kupikia ni ngumu kumudu.

Mwaka uliopita bei ya nafaka ya teff ilikua inagharimu $80 lakini sasa imefikia $146.

Kwa wale ambao wanaweza kununua wanatumia teff kidogo na wanachanganya na mtama ili kutengeneza mkate wa Injera, ambao ni muhimu katika kila chakula nchini Ethiopia.

Lakini wengi hawawezi kununua nafaka hii kabisa.

Matunda
Maelezo ya picha, 

Tumeambiwa tupande mbogamboga katika nyumba zetu, na tunalifanyia kazi hilo. Lakini tatizo ni upatikanaji wa maji.

Tulikua tukinunua lita 200 za maji kwa matumizi ya wiki nzima, lakini sasa hatuwezi kumudu tena na tunapata maji kupitia visima.

Viatu vipya kwa Watoto na kula nyama sasa imekua ni starehe.

Maji ya kunywa safi na umeme imekua vya mgao, tunaweza kukaa siku kadhaa bila vyote

Watu wengi hawana ajira, maduka maduka mengi hapa Makelle yamefungwa, wafanyabiashara hawana kodi za kulipa na wengine hawana bidhaa kwenye maduka yao.

Maduka
Maelezo ya picha, 

Baadhi ya watu pia wameanza kuuza vitu vyao kama magari, samani za ndani na vito vya thamani, wanauza kwa bei ya chini.

Pete ya dhahabu ilikua ikiuzwa $64 sasa inaweza kuuzwa kima cha chini hadi $12.

Watu wakiishiwa vitu vya kuuza wanaanza kuomba, kuna Watoto wengi na wanawake wamegeuka kuwa omba omba wengi mitaani.

Vituo vya afya vina upungufu wa dawa. Wale wenye magonjwa ya kudumu wanakufa kutokana na kukosa dawa.

Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanapata dawa kwa msimu.

Sherehe za kidini na harusi vilikua vitu muhimu katika jamii yetu lakini sasa imebaki kumbukumbu.

Kw ratiba yangu ya siku, kabla shule kufunguliwa nilikua silali mapema, kwasababu nilikua nafatilia Habari mbalimbali.

Kwasasa ni ngumu kujua kinachoendelea, hakuna mtandao hivyo kuwa naenda kwa kwa wauzaji kwenye mitaa ambao huuza video na sauti kwa $0.20.

Wakati mwingine nasoma vitabu na kuzungumza na majirani.

Kupanda kwa bei ya mafuta

Mtoto wangu amerudi kutoka shule, nimetembea sana, natembela kilometa 2 kumfikisha shule, na muda chakula cha mchana mke wangu humfuata tena kwa miguu.

Tulikua tukienda kwa gari, lakini nimeliegesha nje ya nyumba yangu kwa zaidi ya miezi 18 sasa, siwezi kumudu kununua mafuta.

Lita moja ya petroli kwa sasa ni $10, ilikua $0.42 katika vituo vya mafuta.

Kuchukua tax au bajaji pia haiwezekani gharama yake ni kubwa sana.

Kwa sasa farasi wanatumika pia kama usafiri.

Farasi
Maelezo ya picha, 

Watu wengi wameanza kuendesha baiskeli lakini hata baiskeli pia zinauzwa bei juu.

Watu hapa wanataka kumaliza mzozo huu kwa amani, na tulifurahi sana kusikia kuwa kuna makubaliano ya kusimamisha mzozo wiki iliyopita.

Wamekaa wakisubiri kuona kama je ni ahadi tupu, lakini baada ya kufika kwa misaada ya kwanza siku ya ijumaa inaonekana sasa huenda mambo yakabadilika.

Nashkuru sana kuwa ninaishi na ninaweza kutoa simulizi yangu, najua wengi wako kwenye hali mbaya zaidi, na huenda wakawa wanakufa.

Lakini bado watu wanasaidiana.

''Wale wanaokula peke yao, hufa peke yao'' msemo huu unatumiwa na Tigray na watu wanaufuata. Kila wanachopata wanagawa na wengine hata kama watakufa njaa kesho yake. Kuna umuhimu wa kushirikiana.Hatujata jina la mkazi huyu kutokana na sababu za kiusalama.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?