Ndege ya RwandaAir yapoteza mwelekeo baada ya kuteleza katika uwanja wa Entebbe.

Newsday Swahili

Ndege ya abiria iliteleza na kutoka kwenye njia yake ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda Jumatano asubuhi. 

Katika taarifa, RwandAir ilisema tukio hilo "lilitokana na hali mbaya ya hewa".

Abiria wote na wafanyakazi wa ndege walishuka salama bila majeraha yoyote, iliongeza.

Mdhibiti wa anga alisema njia mbadala ya ndege kurukia inafanya kazi kwa ajili ya ndege ndogo na nyepesi.

"Juhudi zote zinaendelea ili kuondoa ndege kwenye ukanda wa kuruka na kutua ndege ili njia kuu ya kuruka na kutua ndege irudi kutumika kikamilifu," ilisema.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda, limeripoti kuwa abiria 20 kati ya 60 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameratibiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba.

Inaripoti kuwa tafrija ya kuzaliwa kwa Jenerali Kainerugaba ya kutimiza miaka 48 imepangiwa kufanyika Jumapili.

Jenerali Kainerugaba, ambaye pia ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alichapisha ujumbe mtandaoni siku ya Jumatatu kwamba aliyekuwa Miss Rwanda atakuwa miongoni mwa wageni watakaohudhuria hafla hiyo.

  • Mutyambai

    Takriban maafisa 2,000 wa polisi wa Kenya hawana uwezo wa kiakili kufanya kazi yao, mkuu wa huduma ya kitaifa ya polisi nchini anasema.

    Inspekta Jenerali Hilary Mutyambai amesema hayo leo katika kongamano la maaskofu na makasisi wakuu akiongeza kwamba wamebaini visa hivyo "vya kushangaza" baada ya kuwafanyia uchunguzi wa kimatibabu maafisa wote wa polisi.

    Kenya ina maafisa 100,000 wa polisi wanaofanya kazi chini ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi.

    Ufichuzi huo unakuja huku kukiwa na ongezeko la idadi ya visa vya maafisa kujitoa uhai ndani ya jeshi la polisi.

    Bw Mutyambai amesema shughuli ya kuwaondoa kazini baadhi ya maafisa wa polisi walioathiriwa imeanza kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na polisi walio sawa kiakili.

    "Zana yetu ya kazi ni bunduki, na risasi moja inapotolpigwa, madhara yake ni makubwa," alisema.

    Hata hivyo alisema mchakato wa kuwaondoa maafisa hao kazini sio rahisi kwa sababu ya taratibu za kina zinazohusika.

    Kumekuwa na wasiwasi unaoongezeka katika miaka ya hivi karibuni juu ya afya ya akili ya maafisa wa polisi na serikali imekuwa ikisonga kushughulikia suala hilo.

    Bw Mutyambai alisema kwa sasa polisi wana bodi ya kitaalamu ya afya inayojumuisha washauri na madaktari wa akili walioidhinishwa na wizara ya afya kutoa huduma za afya ya akili.

    Kituo cha televisheni cha NTV kimeshiriki video inayaoangazia baadhi ya maelezo ya mkuu wa polisi:

  • kamanda wa Mariupol
    Image caption: Kamanda wa Ukraine Mariupol

    Kamanda mmoja wa jeshi la wanamaji nchini Ukraine akiwa miongoni mwa wanajeshi waliozungukwa na Urusi katika mji wa Mariupol ametoa kanda ya videomapeme leo alfajiri akisema wanajeshi wenzake wamesalia na saa chache.

    Katika kanda ya video iliotumwa kwa BBC na vyombo vingine vya habari , Meja jenerali Serhiy Volyna alisema wanajeshi wake hawatasalimu amri , lakaini akatoa wito kwa mataifa ya kigeni kutoa usaidizi kwa wanajeshi 500 waliojeruhiwa na mamia ya wanawake na watoto wanaojificha nao katika kamapuni moja ya kuunda vyuma mjini humo.

    ‘’Huu ndio wito wetu wa mwisho duniani., huenda ukawa wetu wa mwisho kabisa. Inawezekana kwamba tumesalia na saa chache’’, Meja Volyna alisema.

    ‘’Tunatoa wito kwa viongozi kote duniani kutusaidia’’ aliongezea. ‘’Tunawaomba kuja kutusaidia kuondoka na kwenda katika nhci nyingine’’.

  • Mwanamume ameshikilia kopo la mkojo

    Wanasayansi wanasema wamegundua bakteria ya mkojo ambayo inahusishwa na saratani ya kibofu kali.

    Ugunduzi huo unaweza kutoa njia mpya za kugundua na hata kuzuia uvimbe huu hatari, wataalam wanatumai.

    Ni mapema sana kubaini ikiwa bakteria wanaweza kusababisha saratani, badala ya kuwa ishara ya kusaidia.

    Kundi la watafiti Chuo Kikuu cha Anglia Mashariki inafanya uchunguzi zaidi mpango kubaini ikiwa kutibu maambukizi kwa dawa za antibiotiki kunaweza kuzuia uvimbe mbaya.

    Maambukizi ya bakteria yanajulikana kuwa na sehemu katika maendeleo ya saratani nyingine - mdudu anayeitwa H. pylori anaweza kusababisha saratani ya tumbo, kwa mfano, na dozi ya tiba ya antibiotiki inaweza kuzuia hatari hiyo.

    Saratani ya tezi dume sio hatari kwa maisha kila wakati - uvimbe fulani hukua polepole sana hivi kwamba haiwezi kusababisha matatizo yoyote.

    Changamoto ni kuwatambua na kuwatibu haraka wanaume walio na uvimbe unaokuwa kwa kasi, na kuwaepusha wengine na matibabu yasiyo ya lazima.

    Vipimo vinavyopatikana kwa sasa, ni kama vile uchunguzi wa damu wa PSA na biopsy, sio kila mara vinaweza kutabiri ni saratani zipi zitakuwa na madhara.

    Soma zaidi:

  • Urusi yatoa makataa mpya ya 1100 GMT (Jumatano) kwa wanajeshi wa Ukrania huko Mariupol kujisalimisha.

    Ikiwa unajiunga nasi muda huu haya ndio matukio ya hivi punde nchini Ukraine:

    • Wanajeshi wanaopingana wameendelea na makabiliano katika kwenye mstari wa mbele wa maili 300 (480km).
    • Wizara ya ulinzi ya Urusi imewapa wanajeshi wa Ukraine, ambao wamezuiliwa katika jengo la ujenzi wa chuma la Azovstal katika mji wa bandari wa Mariupol, uamuzi mpya, kuweka chini silaha zao ifikapo 1100 GMT siku ya Jumatano. 
    • Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake.
    • Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake Lakini Ukraine imefikia makubaliano ya awali na Urusi kuwahamisha raia, naibu Waziri Mkuu anasema. 
    • Haya yamekuwa magumu kutekeleza katika vita hadi sasa Mwakilishi wa Uingereza ameishutumu Urusi kwa "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari wa Mariupol Katika kukabiliana na mashambulizi ya Moscow, wanajeshi wa Ukraine hadi sasa wameshikilia mstari huo, kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Wanajeshi wa Ukraine.
    • Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake.
    • Lakini Ukraine imefikia makubaliano ya awali na Urusi kuwahamisha raia, naibu.
    • Waziri Mkuu anasema. Haya yamekuwa magumu kutekeleza katika vita hadi sasa.
    • Mwakilishi wa Uingereza ameishutumu Urusi kwa "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari wa Mariupol Katika kukabiliana na mashambulizi ya Moscow, wanajeshi wa Ukraine hadi sasa wameshikilia mstari huo, kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Wanajeshi wa Ukraine.
  • Jiji la Iten ni msingi maarufu wa mafunzo kwa wanariadha wa masafa marefu.

    Mwanariadha wa kike amepatikana ameuawa huko Iten - mji wa Kenya ambapo mwanariadha wa Olimpiki, Agnes Tirop, aliuawa miezi sita iliyopita - polisi wanasema.

    Damaris Muthee Mutua, ambaye alizaliwa nchini Kenya lakini alikuwa na uraia wa Bahrain, alikuwa na umri wa miaka 28. 

    Maafisa wanasema aliuuawa kwa kudungwa kisu.

    Wanamsaka mpenzi wake, mwanariadha wa Ethiopia ambaye polisi wanasema ni mshukiwa mkuu.

    Iten ni kambi ya mafunzo kwa wakimbiaji wa masafa marefu. 

    Mwezi Oktoba mwaka jana mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop yalishtua nchi.

    Mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha kuhusika na mauaji hayo.

  • Rais wa Ukraine
    Image caption: Rais Zelensky wa Ukraine

    Katika hotuba yake ya mara kwa mara katika kanda ya video kwa taifa lake, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kwamba iwapo Ukraine ilikuwa ikimiliki silaha bora ikilinganishwa na zile za Urusi , ingekuwa imemaliza vita.

    Rais Zelensky alisema kwamba katika mahojiano yakena majadiliano na viongozi wa mataifa yaliopiga hatua kubwa kidemokrasia, ‘’sio haki kwa Ukraine kuendelea kuomba usaidizi wa kile ambacho washirika wake wamekuwa wakihifadhi kwa miaka kadhaa’’.

    Alisema kwamba iwapo mataifa hayo yanamiliki silaha ambazo Ukraine inahitaji ni jukumu lao kusaidia kulinda na kuokoa maisha ya maelfu ya raia wa Ukraine.

    Aliongezea kwamba iwapo taifa lake lingefanikiwa kupata silaha hizo ambazo wameahidiwa wiki zijazo, zingesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

    Rais aliongezea kwamba uwezo wa mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kharkiv, Donbasna Dnipropetrovsk umeongezekana hata kulenga makaazi ya raia. 

    ‘’Hatma ya makumi ya maelfu ya wakaazi wa Mariupol ambao walipelekwa katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi haijulikani’’, alisema Zelensky’’.

    Hatua hii inajiri huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikitoa masharti mapya kwa wanajeshi wa Ukraine waliozungukwa katika mji wa Mariupol kusalimu amri.

  • Joe Biden
    Image caption: Joe Biden

    Utawala wa Biden unapanga kutangaza kifurushi kingine cha msaada wa kijeshi wenye thamani ya $800m (£615m) kwa Ukraine, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

    Alipoulizwa Jumanne huko Portsmouth, New Hampshire, ikiwa angetuma silaha zaidi kwa Ukraine, Rais Biden alijibu: "Ndiyo."

    Ikulu ya White House wiki iliyopita ilitangaza kutuma msaada wa kijeshi wa thamani ya $800m kwa Ukraine ambao utajumuisha raundi 40,000 za mizinga na Howitters 18 (155mm.

  • n

    Liverpool waliwashinda Manchester United waliokata tamaa katika mchezo wa aibu uliozidi upande mmoja kwenye uwanja wa Anfield na kupanda hadi kileleni mwa Ligi ya Premia.

    Manchester City huenda wakachukua nafasi yao kilelelni mwa ligi hiyo dhidi ya Brighton siku ya Jumatano , lakini mechi hii imeonesha jinsi timu hiyo ya Jurgen Kllop iko tayari kuwafukuza hadi siku ya mwisho ili kuweza kushinda mataji matatu mwaka huu.

    Pia ilikuwa mechi ambayo ilionesha jukumu kubwa analotarajia mkufunzi mpya aliyeteuliwa kuinoa klabu hiyo Erik ten Hag huku United ikizidiwa katika kila safu ya mchezo .

    United ilimkosa nyota wao Cristiano Ronaldo kufuatia kifo cha mtoto wake aliyezaliwa huku wafuasi wa timu zote mbili wakituma rambirambi zao katika dakika ya saba ya mechi.

    Liverpool tayari ilikuwa kifua mbele wakati huo baada ya Luis Diaz kufunga pasi muruwa ya Mohammed Salah kabla ya mshambuliaji huyo wa Misri kumaliza njaa yake ya mabao katika mech inane kufuatia pasi ya Sadio Mane kunako dakika ya 22.

    Mane alifuta matumaini yoyote ya Man United kwa kufunga bao kunako dakika ya 69 alipopata pasi nzuri kutoka kwa Diaz huku Salah akifunga goli la nne ikiwa imesalia dakika 5 za mchezo.

    Baada ya mabao 5-0 katika uwanja wa Old Trafford mwezi Oktoba, Liverpool sasa ndio klabu ya kwanza kufunga magoli manane dhidi ya Manchester United katika msimu mmoja.

  • m

    Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imetoa taarifa yake hivi karibuni kuhusu mapigano nchini Ukraine, ikiangazia hali ya mashariki mwa nchi hiyo. 

    Katika kurasa ya tweeter, MoD anasema: The MoD anasema Ukraine ilijaribu mara kadhaa kuviondoa vikosi vya Urusi.

    Mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya Urusi kwenye udhibiti katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine yanaendelea kuongezeka 

    Urusi bado inatatizwa na "changamoto za mazingira, vifaa na kiufundi" ambazo tayari zimeonekana katika vita - na vilevile upinzani "uliochochewa sana" kutoka kwa kuwatetea Waukraine.

    Urusi inatumia "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.

    MoD anasema hii ilionyesha kutokuwa na uwezo wa Moscow kufikia malengo yake haraka kama wangependa.

  • Maoni

    Machapisho maarufu kutoka blogu hii

    Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

    Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?