Mtendaji mkuu raia wa Ufaransa kufurushwa Kenya kufuatia mzozo wa mafuta.

Newsday Swahili
Image caption: Kenya imekumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta katika wiki za hivi karibuni.

Mamlaka nchini Kenya imeripotiwa kufuta kibali cha kufanya kazi cha mtendaji mkuu wa Ufaransa wa mojawapo ya kampuni ya kubwa ya kuuza mafuta nchini Kenya kutokana na tatizo la uhaba wa bidhaa hiyo.

Serikali inasemekana kuamuru kufukuzwa nchini kwa Christian Bergeron, mtendaji mkuu wa Rubis Energy Kenya - kampuni tanzu ya Rubis Group yenye makao yake nchini Ufaransa.

Siku ya Jumanne mamlaka ya udhibiti wa kawi nchini humo iliwashutumu baadhi ya wauzaji mafuta kwa kuzuiausambazaji wa mafuta katika soko la ndani na kutoa kipaumbele kwa mauzo ya mafuta kwa nchi jirani.

Mamlaka hiyo aidha ilisema kampuni hizo zitaadhibiwa kwa kupunguziwa kiwango cha mafuta watakayoruhusiwa kuagiza kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

Makampuni ya mafuta ya Kenya yanauza takriban 65% ya bidhaa zao kutoka nje kwa soko la ndani na nyingine kwa nchi jirani zisizo na bandari kama vile Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo


Follow us on Facebook

Follow us on Instagram

Follow us on Twitter 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?