Raheem Sterling: Kwanini mashabiki wa Man City hawamkubali sana’ Sterling? Uchambuzi wa Micah Richards
Nilikuwa katika uwanja wa Etihad siku ya Jumamosi wakati Raheem Sterling alipopoteza nafasi nzuri dhidi ya Watford. Ungewasikia mashabiki walionizunguka walivyokuwa wakigugunia na kupiga kelele 'hafai' au 'mtoe'.
Manchester City walikuwa wanaongoza mabao 3-1 wakati huo na Sterling alikuwa akicheza vizuri sana. Hilo lilikuwa shuti lake la kwanza katika mchezo huo na, ingawa sikusema chochote kwa watu walio karibu nami, nilikuwa nikifikiria tu kwamba walihitaji kutulia na kuwa na subra.
Hata hivyo hilo sio jambo jipya. Sterling anaonekana kushambuliwa zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa City. Haijalishi ni mabao mangapi anayofunga au mambo mazuri anayofanya katika mchezo - ikiwa atakosa, ni kawaida kwa Sterling sivyo?
Bila shaka ninaelewa kwa nini anabebeshwa lawama na mashabiki wakati anapofunga mabao magumu lakini anakosa nafasi za wazi na rahisi kufunga.
Mashabiki wanakosea, pengine pia hatothaminiwa vizuri bila kujali ni mabao mangapi anayofunga au kufanya - au ni mataji mangapi anayoisaidia City kushinda.
Takwimu zake ni za kushangaza. Tangu alipojiunga na City mwaka 2015 amefunga mabao 112 katika mechi 286 alizocheza katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa, na kutoa pasi 55. Hilo ni jambo kubwa kwa kwa mtu ambaye mara nyingi hutumiwa kama mshambualji wa pembeni .
Ana majukumu makubwa kwa timu, kutokana na kasi na mikimbio yake inayoweza kuleta madhara uwanjani.
Kama ilivyo kwa Gabriel Jesus, Sterling ana mkataba unaomalizika mwaka 2023 na mpaka sasa wachezaji hao ambao hawajaongeza mikataba yao, wanahusishwa kuhamia vilabu vingine.
Arsenal wanadaiwa kukaribia kumnasa Jesus na nilisoma habari wiki iliyopita kuhusu Sterling kutakiwa na AC Milan, lakini kwangu mimi ni suala rahisi - City wanapaswa kujaribu kuwabakiza wote wawili kama wanaweza.
Wachezaji wote hawa wawili ni hodari na wanafanya kazi kwa bidii, na wanaweza kucheza kwenye wing azote katikati.
Sterling kuendelea kuimarika
Bado ana umri wa miaka 27 tu. Hakika, kutakuwa na wakati ambapo anapaswa kufunga zaidi, lakini napenda kusema hilo linaweza kuwa hoja kwa wachezaji wengine wachache wa City kutokana na idadi ya nafasi za kufunga ambazo timu inatengeneza.
Sterling aliigharimu City kitita cha £49m alipojiunga kutoka Liverpool mwaka 2015. Unaweza kuona ni gharama kiasi gani kumleta mchezaji mwingine ambaye angeweza kuwa msaada kama anavyofanya Sterling sasa.
Sterling kucheza dhidi ya Real Madrid leo?
Real Madrid ni wageni wa City leo katika uwanja wa Etihad, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Pep Guardiola na ana maamuzi magumu ya kufanya. Mara nyingi hulazimika kuacha washambuliaji wake wengi nje.
Mara ya mwisho kwa City kucheza na Real katika uwanja wa Etihad ilikuwa ni msimu wa 2019-20. Katika mechi ya mkondo wa pili katika uwanja wa Etihad, Guardiola aliamua kutumia washambuliaji watatu mbele, Jesus, Foden na Sterling, kasi yao na kukaba kuanzia mbele kuliwafanya Real Madrid kuwa na kibarua kigumu, City ilishinda 2-1.
Wakati huu, kama City wangekuwa imara katika safu ya ulinzi nadhani Guardiola angemwacha Sterling nje ya kikosi cha kwanza, aanze safu ya ushambuliaji yenye Foden, Jesus na Rihad Mahrez, na kuangalia namna ya kumtumia akitokea benchi.
Lakini kutokana kutokuwepo kwa mlinzi tegemeo wa pembeni, Joao Cancelo, mwenye kadi na mwingine, Kyle Walker, mwenye majeraha huenda asicheze, City inaweza kuwa na udhaifu wa kujihami kwenye eneo lake la ulinzi kila upande, kulia na kushoto.
Maoni
Chapisha Maoni