Vita vya Ukraine: Je China itaweza kuisaidia Urusi kijeshi?

Newsday Swahili

Urusi inatafuta washirika ili kupunguza athari za vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa kujibu shambulio lake dhidi ya Ukraine.

China inatafuta kutoegemea upande wowote katika mzozo huo na kutoa wito wa suluhu ya amani.

Lakini bado haijalaani uvamizi wa Urusi na kukosoa vikwazo vya Magharibi.

Biashara ya China na Urusi imekuwa ikiongezeka

China inasema "itaendeleza ushirikiano wa kawaida wa kibiashara na Urusi" licha ya viongozi wa nchi za Magharibi kusisitiza kutolegeza vikwazo.

Kwa mujibu wa takwimu za forodha za China, biashara baina ya China na Urusi iliongezeka kwa 28% katika robo ya kwanza ya mwaka ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Mnamo Machi, baada ya uvamizi wa Urusi, biashara ya jumla kati ya nchi hizo mbili iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka jana.

China ilichangia karibu asilimia 18 ya jumla ya biashara ya Urusi mwaka 2021 - karibu dola bilioni 110 mwaka jana.

Wakati wa ziara ya Vladimir Putin mjini Beijing mwezi Februari kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi, nchi hizo mbili zilisema zitaongeza biashara hadi dola bilioni 250 ifikapo mwaka 2024. 

Hata hivyo EU kwa ujumla inasalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Urusi.

Mnamo mwaka 2021, jumla ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilikuwa karibu mara mbili ya thamani ya biashara ya Uchina na Urusi.

Hali hii inaweza kubadilika sasa.

"Kupunguza biashara ya Ulaya-Urusi katika kukabiliana na vikwazo ni jambo lisiloepukika. Mgogoro wa sasa umeongeza mwelekeo wa Ulaya juu ya haja ya kubadilisha usambazaji, "alisema Dk Rebecca Harding, mwanauchumi wa biashara.

Je, China inaweza kununua nishati zaidi kutoka Urusi

China ni moja ya soko kubwa la mafuta, gesi na makaa ya mawe la Urusi.

Wiki moja tu kabla ya uvamizi wa Ukraine, nchi hizo mbili zilikubaliana juu ya makubaliano mapya ya makaa ya mawe ya Urusi yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 20.

Bw Putin pia alizindua kandarasi mpya za mafuta na gesi za Urusi zenye thamani ya dola bilioni 117.5 na China.

Lengo la nchi hizo mbili ni kujenga bomba jipya la gesi (Siberian Power 2).

Bomba la sasa lilizinduliwa mnamo mwaka 2019 na mkataba wa miaka 30 wenye thamani ya zaidi ya 400$ bilioni.

پایانه چین در تیانجین گاز طبیعی مایع را از روسیه دریافت می‌کند

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Kituo cha China huko Tianjin kinapokea gesi asilia iliyoyeyuka kutoka Urusi

Hata hivyo, soko kubwa la nishati nchini Urusi hadi sasa limekuwa Umoja wa Ulaya, ambao unatoa asilimia 40 ya gesi ya umoja huo na takriban asilimia 26 ya mafuta yake.

"Usafirishaji wa mafuta na gesi wa Urusi [kwenda Uchina] umekua kwa zaidi ya asilimia 9 kila mwaka katika miaka mitano iliyopita. Huu ni ukuaji wa haraka, lakini pamoja na haya yote, soko la China ni karibu nusu ya ukubwa wa soko la mafuta la Urusi la Umoja wa Ulaya. "anasema Dkt. Harding.

"Umoja wa Ulaya unapunguza utegemezi wake kwa nishati ya Urusi kwa kupunguza uagizaji wa gesi kutoka nje kwa thuluthi mbili kufuatia vita vya Ukraine. 

Ujerumani, nchi ambayo ni kituo kikuu cha usafirishaji wa gesi cha Urusi, imetangaza kuwa itasitisha bomba jipya la gesi la Stream 2. 

Kulingana na uchanguzi mmoja, usambazaji kupitia bomba jipya lililokubaliwa kati ya Urusi na Uchina itakuwa na moja ya tano tu ya uwezo wa bomba la Stream 2.

کار روی بخش چینی یک خط لوله گاز از روسیه در سال ۲۰۱۷

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Kazi ikiendelea katika eneo la upande wa China kwenye bomba la gesi kutoka Urusi mnamo 2017

Pia haijulikani ni lini bomba jipya la gesi kutoka Siberia litazinduliwa.

Kwa muda mrefu, China inaweza kutaka kuongeza uangizaji wa gesi ya Urusi ili kupunguza utegemezi wake kwa makaa ya mawe na kufikia malengo yake ya kupunguza gesi chafu.

Lakini data zinaonyesha kuwa uagizaji wa mafuta ghafi nchini China kutoka Urusi ulipungua kwa asilimia 9 katika miezi miwili ya kwanza ya 2022. 

Viwanda vya kusafisha mafuta vinavyomilikiwa na serikali ya China pia vimeripotiwa kuwa waangalifu na kwa sasa havisaini mikataba mipya ya mafuta ya Urusi.

Je, China inaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Urusi?

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari zilizonukuliwa na afisa mmoja wa Marekani, Moscow imeiomba China vifaa vya kijeshi kusaidia uvamizi wake nchini Ukraine.

Uchina inasema hii sio kweli na imeziita ripoti hizo "taarifa za kupotosha."

Katika miaka ya hivi karibuni, mwelekeo wa jinsi silaha zinavyokwenda kwa ujumla umebadilishwa.

چین دارای قابلیت‌های پهپاد مسلح پیشرفته است

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

China ina uwezo wa hali ya juu wa ndege zisizo na rubani

China inategemea sana vifaa vya kijeshi vya Urusi kufanya vikosi vyake vya kijeshi kuwa vya kisasa, jambo ambalo lilizidi kuwa muhimu kutokana na vikwazo vya silaha vya Marekani na Ulaya kufuatia kukandamizwa kwa Tiananmen Square mwaka 1989. 

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI), karibu asilimia 80 ya jumla ya uagizaji wa silaha wa China kati ya 2017 na 2021 ulitoka Urusi.

China, mteja wa pili kwa ukubwa nchini Urusi, inachangia asilimia 21 ya jumla ya mauzo ya silaha nchini humo.

Lakini China imeongeza hatua kwa hatua uwezo wake wa uzalishaji kijeshi.

Sasa ni muuzaji silaha wa nne kwa ukubwa duniani.

"Silaha za China zinazidi kuwa za hali ya juu sasa. Urusi, kwa mfano, inavutiwa sana na ndege zisizo na rubani za China," Simon Wazman wa SIPRI alisema.

Lakini anasema "hatujaona ushahidi wowote" kwamba Urusi imenunua ndege zisizo na rubani za China.

Je, China inaweza kuisaidia Urusi kifedha?

Baadhi ya benki za Urusi zimezuia ufikiaji wa mfumo wa malipo wa kimataifa wa Swift

ذخایر ارزی باقی مانده روسیه پس از تحریم‌ها، طلا و یوان چین است

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Akiba ya fedha za kigeni iliyosalia ya Urusi baada ya vikwazo ni dhahabu na Yuan ya Uchina

Hii imewalazimu makampuni nchini Uchina na mataifa mengine kupunguza ununuzi kutoka Urusi kwa sababu wafanyabiashara wanatatizika kupata ufadhili.

Katika miaka ya hivi majuzi, Uchina na Urusi zimehimizwa kubadili kutumia njia mbadala za malipo.

Urusi ina mfumo wake wa kutuma ujumbe wa kifedha (STFM), wakati Uchina ina mfumo wake wa malipo wa kuvuka mpaka (CIPS), ambao wote hufanya kazi kwa kutumia sarafu zao.

Lakini mfumo wa Swift bado unatawala shughuli za kifedha katika mtandao wa biashara wa kimataifa.

Kulingana na takwimu rasmi za Urusi, ni takriban asilimia 17 tu ya biashara kati ya Urusi na Uchina kwa sasa iko katika Yuan ya Uchina (ikilinganishwa na asilimia 3.1 mnamo 2014).

Biashara ya nishati kati ya nchi hizo mbili bado inafanywa zaidi kwa dola za Kimarekani.

Lakini makampuni kadhaa ya China yanaripotiwa kutumia Yuan mwezi Machi kununua makaa ya mawe na mafuta ya Urusi.

Je, China inaweza kupanua biashara ya chakula na Urusi?

Uchina ni muagizaji mkuu wa nafaka kama vile ngano na shayiri, na moja ya vyanzo vyake muhimu ni Urusi - moja ya wazalishaji wakubwa zaidi ulimwenguni.

Hadi hivi majuzi, Uchina ilikuwa imezuia uagizaji wa ngano na shayiri kutoka Urusi kwa sababu ya wasiwasi juu ya kuenea kwa ugonjwa huo.

Lakini vikwazo hivi vyote viliondolewa siku ambayo Urusi ilianzisha uvamizi wake kwa Ukraine.


Follow us on Facebook

Follow us on Instagram

Follow us on Twitter 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?