Mabinti za Putin ni akina nani? Tunachojua kuhusu familia yake


TH

CHANZO CHA PICHA, ALAMY

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amekuwa na usiri kila wakati linapokuja suala la maswali juu ya familia yake.

Mnamo 2015, wakati wa moja ya mikutano yake ya habari, alikwepa maswali kuhusu utambulisho wa binti yake.

"Binti zangu wanaishi Urusi na walisoma nchini Urusi tu, ninajivunia wao," alisema. "Wanazungumza lugha tatu za kigeni kwa ufasaha. Sijawahi kujadili familia yangu na mtu yeyote."

"Kila mtu ana haki ya hatima yake, anaishi maisha yake mwenyewe na anafanya kwa heshima," aliongeza.

Labda hataki kuwataja, lakini wengine wamewataja. Awamu ya hivi punde ya vikwazo vya Marekani imewalenga Maria Vorontsova, 36, na Katerina Tikhonova, 35.

"Tunaamini kwamba mali nyingi za Putin zimefichwa na wanafamilia, na ndiyo maana tunawalenga," afisa mmoja wa Marekani alisema.

Ingawa machache yamethibitishwa rasmi kuhusu maisha ya familia ya Rais Putin, nyaraka, ripoti za vyombo vya habari na matamshi ya mara kwa mara hadharani yanatosha kutoa picha ya wawili hao.

Wawili hao ni mabinti wa Rais Putin na mke wake wa zamani Lyudmila. Wawili hao walioana mwaka wa 1983 alipokuwa mhudumu wa ndege na yeye afisa wa KGB. Ndoa yao ilidumu kwa miaka 30, ikichukua kasi ya Bw Putin kufikia kilele cha mfumo wa kisiasa wa Urusi.

Mnamo 2013, walitengana . Bw Putin alisema "ulikuwa uamuzi wa pamoja: ni vigumu kuonana, kila mmoja wetu ana maisha yake". Alisema "alikuwa amezama kabisa kazini".

Mkubwa wao, Maria Vorontsova, alizaliwa mwaka wa 1985. Alisoma biolojia katika Chuo Kikuu cha St Petersburg na utabibu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Moscow.

H

CHANZO CHA PICHA, AFP

Bibi Vorontsova sasa ni msomi, aliyebobea katika mfumo wa endocrine. Aliandika pamoja kitabu juu ya ukuaji duni wa watoto, na ameorodheshwa kama mtafiti katika Kituo cha Utafiti wa Endocrinology huko Moscow.

Yeye pia ni mfanyabiashara. BBC Russia ilimtambua kama mmiliki mwenza wa kampuni inayopanga kujenga kituo kikubwa cha matibabu.

Unaweza pia kusoma

Bi Vorontsova ameolewa na mfanyabiashara Mholanzi Jorrit Joost Faassen, ambaye aliwahi kufanya kazi katika kampuni kubwa ya nishati ya serikali ya Urusi Gazprom, ingawa wameripotiwa kutengana.

Watu ambao wamezungumza naye tangu uvamizi wa Ukraine wanasema anamuunga mkono babake, na ametia shaka juu ya ripoti ya kimataifa ya mzozo huo.

Akilinganishwa na dada yake Katerina Tikhonova amekuwa machoni pa umma sana , sio kwa sababu ya talanta yake kama mwanadensi ya rock n'roll. Yeye na mwenzi wake walishika nafasi ya tano katika hafla ya kimataifa mnamo 2013.

TH

CHANZO CHA PICHA, AFP

Mwaka huo huo, aliolewa na Kirill Shamalov, mtoto wa rafiki wa muda mrefu wa Rais Putin. Harusi yao ilifanyika katika hoteli ya i karibu na St Petersburg. Wafanyikazi huko walisema wanandoa hao walifika kwa gari lililovutwa na farasi watatu weupe.

Bw Shamalov aliwekea vikwazo na Marekani mwaka wa 2018 kwa jukumu lake katika sekta ya nishati nchini Urusi. Hazina ya Marekani ilisema kwamba "bahati yake iliboreka sana kufuatia ndoa". Wawili hao wametengana 

Kufuatia uvamizi wa Ukraine, wanaharakati wawili wa Urusi walikamatwa kwa kumiliki jumba la kifahari huko Biarritz linalosemekana kumilikiwa na Bw Shamalov.

Bi Tikhonova sasa yuko katika taaluma na biashara. Alijitokeza kwa ufupi kwenye vyombo vya habari vya serikali ya Urusi mwaka wa 2018 ili kuzungumza kuhusu teknolojia ya neva na pia katika kongamano la biashara mnamo 2021. Katika hali zote mbili uhusiano wake na rais haukutajwa.

Hakuna kati yao anayesemekana kutumia muda mwingi na Rais Putin.

Bw Putin pia ana wajukuu. Aliwataja kwenye simu mnamo 2017, lakini hakusema ni wangapi alikuwa nao au ni bintiye yupi alikuwa nao.

"Kuhusu wajukuu zangu mmoja tayari yuko shule ya chekechea, naomba unielewe sitaki wakue kama wana wa kifalme, nataka wakue kama watu wa kawaida," alisema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?