Virusi vya corona: Dkt Anthony Fauci atahadharisha kuwa Marekani itakuwa na visa 100,000 kwa siku
Mtafiti mkuu wa magonjwa Dkt Anthony Fauci ameliambia bunge la seneti nchini Marekani kuwa ''hatashangazwa'' ikiwa maambukizi mapya yatafikia 100,000 kwa siku. ''Ni wazi hatujaudhibiti kwa sasa,'' alikiri, akitoa tahadhari kuwa haitoshi kwa Wamarekani kuvaa barakoa na kutochangamana Katika hotuba yake, alisema kuwa karibu nusu ya watu wote wapya walioambukizwa wanatoka katika majimbo manne. Awali, Gavana wa New York alisema karibu nusu ya Wamarekani wote lazima wajiweke karantini ikiwa watatembelea jimbo hilo. Siku ya Jumanne, idadi ya watu walioambukizwa iliongezeka kwa zaidi ya 40,000 kwa siku moja kwa mara ya nne katika kipindi cha siku tano. Ongezeko- ambalo limekuwa kubwa katika majimbo ya Kusini na Magharibi limelazimu majimbo karibu 16 kusitisha na kutazama upya mipango yao ya kuyafungulia majimbo hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la CNN. Florida, Arizona,Texas na California ni majimbo manne yaliyotolewa mfano na Dkt...