Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2020

Wakenya sasa ruksa kushiriki mazishi ya waliokufa na corona

Picha
Kuanzia sasa raia wa Kenya wataweza kushiriki shughuli za mazishi ya wapendwa wao waliofariki kutokana na virusi vya corona baada ya serikali kulegeza masharti tofauti na awali ambapo walipiga marufuku. Awali ndugu wa karibu wa mtu aliyekufa kwa corona hakuruhusiwa kufanya chochote zaidi ya kuangalia kwa mbali wakati maafisa wa afya waliojihami kwa mavazi maalum wakifanya shughuli za mazishi. Maafisa wa afya wamesema kuwa miili ya marehemu waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona haiwezi kuambukiza virusi hivyo. Shirika la afya duniani (WHO) na kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika CDC hawajasema bado kama maiti haiweza kuambukiza Covid-19, lakini wamebadilisha utaratibu na kuruhusu familia kuaga wapendwa wao. Nchini Kenya', maofisa wa afya watakuepo katika mazishi ili kutoa muongozo na kuhakikisha usalama unazingatiwa. "Tutaruhusu shughuli zote za mazishi za kidini na kitamaduni kufuatwa kulingana na tamaduni za marehemu," Serikali imekiri kuwa

Jaji wa Mahakama ya Juu Marekani Ruth Ginsburg afariki

Picha
Jaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani Ruth Bader Ginsburg, mpiganiaji wa haki za wanawake ambaye alikuwa jaji wa pili mwanamake katika mahakama hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 Kifo chake ambacho kimetokea wiki sita tu kabla ya Uchaguzi wa Rais huenda kikaanzisha mapambano makali ya kisiasa kuhusu kama Rais Donald Trump anapaswa kumteuwa, na baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublican liidhinishe, mrithi wake, au kama kiti hicho kibaki wazi hadi baada ya kujulikana matokeo ya kinyang'anyiro chake dhidi ya Mdemocrat Joe Biden. Ginsburg ni Mliberali alijetambulika kwa kutetea haki za wanawake na jamii za walio wachache. Kiongozi wa Maseneta wa Republican Mitch McConnell amesema Seneti itapiga kura ya kuidhinisha au kupinga jaji atakayependekezwa na Trump kumrithi Ginsburg, hata ingawa ni mwaka wa uchaguzi.  Trump amemuita Ginsburg "mwanamke wa ajabu" na hakutaja kuhusu kujaza kiti chake kilichobaki wazi katika Mahakama ya Juu wakati akizungumz

Mazungumzo ya amani: Mjumbe wa Marekani hafurahii mpango wa kuwaachia wafungwa wa Taliban

Picha
Mjumbe wa Marekani katika mkutano wa kutafuta amani nchini Afghanstan ameiambia Newsday Swahili kuwa "hafurahii" makubalino yenye utata ya kuwaachia huru wafungwa 5,000 wa Talban ili kufanikisha mazungumzo ya amani ya kihistoria. Hatahivyo mwakilishi huyo Lyse Doucet, Zalmay Khalilzad aliongeza kuwa "Inabidi kufanya maamuzi magumu". Alipoulizwa kuhusu waliokuwa wafungwa kurejea katika mapigano, bwana Khalilzad alisema "hawana ushahidi wowote". Mazungumzo ya Amani kati ya viongozi wa Afghan na Talban yalianza mjini Qatar siku ya Jumamosi. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Afghanistan kuwa na mazungumzo ya amani na kundi la wanamgambo wa kiislamu. Lengo likiwa ni kusitisha mapigano ya miaka 19. Kuachiwa huru kwa wafungwa 5,000 lilikuwa sharti walilokubaliana Marekani na Taliban baada ya mazungumzo ya amani ya mwaka jana na kuanza mazungumzo haya. Serikali ya Afghanistan haikuhusishwa katika kuweka makubaliano hayo

Uchaguzi Tanzania 2020: Dini zina mchango gani katika siasa za Tanzania?

Picha
Katika hotuba yake ya kuaga Watanzania wakati akistaafu maisha ya kisiasa takribani miongo minne iliyopita, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisimulia kisa kinachoeleza uhusiano baina ya dini na siasa za Tanzania. Alisimulia kisa kilichotokea wakati Tanganyika (ambayo Muungano wake na Zanzibar ndiyo umeunda Tanzania), ikipigania Uhuru wake dhidi ya wakoloni Waingereza. Mwalimu Nyerere, alikuwa amechukuliwa na wazee wa chama cha TANU ambao wengi wao walikuwa waumini wa dini ya Kiislamu. Wakampeleka Bagamoyo, Pwani kwa ajili ya kufanya ibada maalumu ya kumwondoa mkoloni. Kukatisha hadithi hiyo, Nyerere alieleza namna yeye (Mkristo), alivyokubalika na kupokewa na Waislamu wa Dar es Salaam kiasi cha kukabidhiwa madaraka ya juu zaidi hapa nchini. Mkasa huu wa Baba wa Taifa la Tanzania unaeleza pia kuhusu ukweli mwingine kuhusu taifa hili; kwamba ingawa kuna dini mbili kubwa, kuna dini ya tatu ambayo huwa haisemwi sana lakini ina nguvu sana - dini ya nyumbani.

Majaribio ya chanjo ya corona kuanza tena

Picha
Majaribio ya chanjo ya corona yameanzishwa tena baada ya zoezi hilo kusimamishwa kwa muda mfupi. Wakati huo huo idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka katika nchi kadhaa kote ulimwenguni. Matumaini ya kupata afueni kutokana na janga la corona duniani kote yalididimia mapema wiki hii wakati kampuni ya dawa ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza zilipotangaza kuwa zimesitisha majaribio ya chanjo hiyo baada ya mtu aliyejitolea kutoka Uingereza kupata ugonjwa ambao haueleweki. Lakini hapo Jumamosi 12/09/2020 majaribioya chanjo hiyoyalipewa ruhusa ya kuanza tena na wasimamizi wa Uingereza baada ya chanjo hiyo kufanyiwa ukaguzi na kudhihirishwa kuwa ni salama. Kampuni ya dawa ya AstraZeneca pia imetangaza  kwamba itaanza tena majaribio ya chanjo hiyo huko nchini Brazil baada ya kupewa ruhusa. Huku mamilioni ya watu wakiwabado wanakabiliwa na athari za maambukizi ya corona na ugonjwa wa COVID -19, mbio za kutafuta chanjo ulimwenguni kote  zinaendelea. Kam

Jeshi la Mali kuunda serikali ya mpito ya miezi 18

Picha
Jeshi la mapinduzi nchini Mali limeapa kuunda serikali ya mpito ya muda wa miezi 18 ili kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya mwezi uliopita dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubacar Keita Kamati iliyoteuliwa na jeshi hilo la mapinduzi iliidhinisha kwa kauli moja ''mkataba wa mpito'' katika mkutano wa faragha kuhusu ubadilishanaji wa mamlaka hatua inayotoa njia kwa serikali ya muda itakayoongoza kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mpya. Lakini moja ya masuala tata zaidi bado halijapata ufumbuzi kuhusu iwapo serikali hiyo ya mpito itaongozwa na raia ama mwanajeshi. Moussa Camara, katibu wa kamati hiyo, amesema jana kwamba serikali mpya itaundwa na wanachama zaidi ya 25,  pamoja na waziri mkuu. Soma zaidi:  Imam Mali aunga mkono rais wa kiraia wa mpito Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa chini ya mkataba wa awali, rais wala mawaziri wa serikali ya mpito hawawezi kuwania madaraka muda wao wa kuhudumu utakapokamilika.     Camara

Bahrain yaungana na UAE kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel

Picha
Bahrain siku ya Ijumaa 11.09.2020 ilijiunga na Muungano wa falme za kiarabu katika kukubali kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli hatua iliyochochewa kiasi na hofu ya pamoja kuhusu Iran . Ikulu ya White House nchini Marekani imesema rais Donald Trump alitoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.Akiwahutubia wanahabari katika ofisi yake, Trump aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria na kwamba anaamini mataifa mengine yatafuata mkondo huo. Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Bahrain na Israeli zimesema kuwa kufungua mawasiliano ya moja kwa moja na  ushirikiano kati ya  pande hizo mbili na chumi  zilizoimarika kutaendelea kuleta mabadiliko ya manufaa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza uthabiti, usalama na ufanisi katika eneo hilo. Hofu ya Wapalestina Wapalestina walifadhaika, wakihofia kuwa hatua hiyo ya  Bahrain na Muungano wa

Mwanamke mwenye macho ya bluu afunga ndoa tena na mumewe baada ya kupatana

Picha
Risikat Azeez, mwanamke mwenye macho ya buluu kutoka Kwara na mume wake, Wasiu Omo-Dada, inaripotiwa kwamba wameoana tena. Wawili hao hatimaye wametatua tofauti zao na kufunga pingu za maisha. Mwanamke huyo wa watoto wawili alikuwa amemshutumu mume wake kwa kuwatelekeza yeye na wanawe wawili kwasababu macho ya bluu. Lakini muda mfupi baada ya taarifa yake kusambaa mtandaoni, mume wake ambaye walikuwa wametengana Omo Dada alijitokeza na kuanza kuzungumzia upande wake na hatimaye wakafikia maridhiano. Awali, Mwanamke huyo alisema kwamba ameachana na mume wake. Yeye na watoto wake wanakabiliana na unyanyapaa kutoka kwa watu ambao walifikiri macho yao yaliwafanya kuwa wachawi.  Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter Subscribe our YouTube channel

Maktaba kubwa ya propaganda za kundi la IS yabainika

Picha
Moja ya eneo kubwa lenye mkusanyiko wa nyenzo nyingi za matandaoni za kundi la Islamic Stale limebainika na watafiti katika Taasisi ya majadiliano ya Kimkakati. Maktaba hiyo ya mtandaoni ina nyenzo zaidi ya 90,000 na inasemekana wageni wanaoitembelea kwa mwezi idadi yao inakadiriwa kuwa 10,000. Wataalamu wanasema maktaba hiyo imewezesha kundi hilo lenye msimamo mkali kubadilisha na kuongeza maudhui yake mtandaoni. Lakini kuondoa maktaba hiyo ni changamoto kwasababu data hiyo haihifadhiwi sehemu moja. Licha ya hatua za kukabiliana na ugaidi, Uingereza na Marekani zimetahadharishwa kuhusu maktaba hiyo inavyozidi kupanuka. 'G aidi mzuri' Ugunduzi wa maktaba hiyo umewadia baada ya kufariki dunia kwa kiongozi maarufu Abu Bakr al-Baghdadi, Oktoba 2019. Wakati huo, ujumbe mwingi wa mitandao ya kijamii unaounga mkono shirika ukiwa na viunganishi vifupi Viunganishi hivyo vimesaidia watafiti kufikia nyaraka na video zilizohifadhiwa