Wana anga waeleza mitikisiko waliyoipata walipokuwa wakirejea duniani

Wanaanga Bob Behnken na Doug Hurley wameeleza changamoto, joto na mitikisiko waliyopitia walipokuwa wakirejea duniani kwa chombo chao wakitokea anga ya mbali.
Waziwazi kabisa Behken alieleza namna walivyokuwa wakipishana na mawingu na mitikisiko hali iliyowafanya kujihisi kama ''kupigwa nyuma ya viti kwa ubao wa mpira wa magongo.''
Lakini Hurley na Behnken amesema kuwa chombo kimefanya kazi kama ilivyotarajiwa.
Walitua katika ghuba ya Mexico, wakikamilisha safari yao ya kwanza kibiashara ya anga za mbali.
''Wakati tukitua, binafsi nilistaajabishwa kwa namna tukio hilo lilivyokuwa. Ilikuwa kama dakika chache, tuliweza kutazama dirishani na kushuhudia tukikata mawingu,'' alisema katika akiwa katika kituo cha Nasa cha Johnson Space mjini Houston.
Mara tu tuliposhuka kidogo angani, chombo kilikuja kikiwa hai. Ilianza kuwasha moto na kutuelekeza mwelekeo unaofaa. - unaweza kusikia mlio nje ya chombo. Na wakati chombo kikijaribu kudhibiti unahisi kidogo hali ya kuyumba.
Chombo kilipokuwa kikitua duniani, mitikisiko iliongezeka . ''Nilirekodi sauti lakini haisikiki kama mashine, inasikika kama sauti ya mnyama,'' alisema Behnken
Behnken pia alieleza ile hali ya ''joto'' ndani ya chombo . Aliwasifu mafundi waliofanya kazi na chombo hicho: ''Sina maneno ya kutosha kusema namna jinsi kikosi cha Space X kilivyotufundisha,'' alisema
Baada ya kutua, boti zilikuwa zikikaribia chombo hicho, ambacho kilitua eneo la mwambao wa Pensacola, Florida.
Boti hizo zilitakiwa kuondoka kutokana na chombo hicho kutos kemikali hatari kutoka kwenye mifumo yake.
''Tunawashukuru wale waliotaka kushiriki kwenye tukio hili lakini kuna tahadhari za kiusalama- kama mwongozaji mkuu wa Nasa Jim Bridenstine alivyosema-zinapaswa kutazamwa.''
Nasa anasimamia usafirishaji wa wanaanga kwenda na kutoka ISS kwa kampuni binafsi, Space X na Boeing. Tangu ilipoacha kutumia vyombo vyake vya safari za anga za mbali mwaka 2011, Marekani haikuwa na chombo cha kusafirisha wana anga wake kutoka katika ardhi yake.
Marekani imeilipa Urusi mamilioni ya dola kwa kila kiti kwa ajili ya wanaanga wake kwenda kwenye chombo cha Soyuz.
Wakati wa safari ya mwisho, wanaanga wa Marekani waliacha bendera ya Marekani katika kituo cha anga kwa lengo la kuwa wanaanga wengine watakaosafiri kwenye chombo wairudishe duniani bendera hiyo.
Ni miaka tisa sasa, Hurley na Behnken wamerejesha bendera hiyo, ambao pia waliruka kwa mara ya kwanza kwenye operesheni hiyo mwaka 1981.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?