Israel na UAE kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatumai mpango wa Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu unaweza kusaidia kufikiwa suluhisho la mataifa mawili na Wapalestina kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati. 
Israel na UAE zimekubaliana kurejesha mahusiano katika muafaka wa kihistoria, ambao ni wa tatu pekee wa aina hiyo ambao taifa hilo la Kiyahudi limewahi kusaini na taifa la Kiarabu, ambapo imeahidi kusitisha unyakuzi wa ardhi za Wapalestina.
Guterres amesema unyakuzi unaweza "ukafunga kabisa mlango" wa mazungumzo kati ya Israel na viongiozi wa Palestina na "kuharibu matumaini" ya kupatikana taifa la Kipalestina chini ya suluhisho la mataifa mawili. Waziri Mkuu wa Israel Bwenjamin Netanyahu amesema ni "siku ya kihistoria" na muafaka huo utafungua enzi mpya kwa ulimwengu wa Kiarabu na Israel. 
Makubaliano haya ni pamoja na mahusiano kamili ya kidiplomasia, kufunguliwa kwa balozi na kubadilishana mabalozi, uwekezaji mkubwa ambao utaufaidi pakubwa uchumi wa Israel hasa wakati huu wa virusi vya corona, mahusiano ya kibiashara, utalii na safari za ndege zikiwemo za moja kwa moja kati ya Israel na Abu Dhabi."

Rais wa Marekani Donald Trump alisema viongozi wa Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu watasaini muafaka huo katika Ikulu ya White House katika kipindi cha karibu wiki tatu zijazo. Akizungumza baada ya mpango huo kutangazwa, Trump aliwasifu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Kiongozi wa UAE Sheikh Mohamed bin Zayed Al-Nahyan akisema ni washirika "wazuri zaidi" ambao wamedhihirisha "maono na uongozi bora".
Follow us on Facebook
Follow us on Instagram
Follow us on Twitter
Subscribe our YouTube channel

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?