Bayern Munich wailaza PSG na kushinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya

Bayern Munich iliizidia Paris St-Germain katika fainali kali ya kombe la ligi ya mabingwa Ulaya ili kutawazwa mabingwa kwa mara ya sita katika mechi iliochezwa Lisbon.
Kingsley Coman ambaye alianza soka yake katika klabu ya PSG alifunga goli la pekee kunako dakika ya 59 kupitia kichwa kufuatia krosi iliopigwa na Joshua Kimmich na kuwawacha mabingwa hao wa Ufaransa wakisalia kutafuta ushindi wa kombe hilo.
Ulikuwa usiku wa furaha kwa mkufunzi wa Bayern Hansi Flick , ambaye aliisaidia timu hiyo kupata kombe lake la pili msimu huu baada ya lile la ligi, alipochukua ukufunzi wa timu hiyo kufuatia kufutwa kwa Niko Kovac mwezi Novemba.
Ulikuwa usiku mrefu kwa nyota wawili wa mabingwa hao wa Ufaransa Neymar na Mbappe ambao walishindwa kuonesha umahiri wao na kujipata wakifadhaishwa na kipa wa Bayern Manuel Neuer aliepewa tuzo la mchezaji bora wa mechi wakati walipopoteza fursa za wazi.
Uchungu wa Mbappe uliongezeka katika kipindi cha pili wakati alipoonekana kuchezewa visivyo na Kimmich katika eneo hatari la goli , lakini hatua ya PSG kutaka kuzawadiwa penalti ilipuuzwa na kuiwacha Bayern ikisherehekea kutawaza kuwa mabingwa wa Ulaya.
Bayern walihitaji kushinda kombe hilo ambalo ni la sita kupitia uwezo wao na udhabiti wa kuzishinda tikmu nyengine lakini pia walionesha ari ya kuwafadhaisha washambuliaji Neymar na Mbappe.
Lakini sifa kubwa inafaa kumwendea kocha Flick , a,mbaye ameiongoza Bayern kushinnda mara 21 mfulululizo , akiigugua timu hiyo na kuisaidia Bayern baada ya kufutwa kwa Kovac mwezi Novemba huku klabu hiyo ikiwa katika mzozo.
Flick pia alionesha uwezo wake wa kuchagua wachezaji akimuanzisha Coman badala ya raia wa Croatia Ivan Perisic

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?