Uchaguzi Tanzania 2020: Pingamizi la Tundu Lissu dhidi ya rais Magufuli na professa Lipumba lashindwa kufurukuta

Mgombea wa urais nchini Tanzania kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA Tundu Lissu ameshindwa kuwazuia wapinzani wake katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka huu kuondolewa katika orodha ya watakaogombea wadhfa huo.
Tundu Lissu alikuwa amewasilisha pingamizi dhidi ya rais John Pombe Magufuli na profesa Ibrahim Harun Lipumba kuondolewa katika orodha ya kuwania urais kwa sababu za kutokamilisha matakwa ya kisheria katika kujaza fomu za uteuzi wa kiti hicho.
Katika pingamizi hilo alilolowasilisha kwa tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC , bwana Lissu pia alidai kwamba rais John Pombe Magufuli hakuambatanisha picha katika fomu zake za uteuzi.
Lakini ikitoa uamuzi wake, tume ya uchaguzi nchini humo NEC imesema kwamba baada ya kupitia pingamizi zote mbili na utetezi uliotolewa, imejiridhisha kuwa rais John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM alirejesha fomu zake ambazo ziliambatanishwa na picha kwa mujibu wa sheria za tume ya taifa ya uchaguzi.
Kulingana na taarifa hiyo iliotiwa saini na Mkurugenzi wa uchaguzi Dkt. Wilson M Charles , tume hiyo imejiridhisha na kwamba pingamizi hizo hazina msingi wa kisheria na imezipuuzilia mbali.
'' Kwa maana hiyo Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea kuwa mgombea halali wa kiti cha urais kupitia chama cha CCM''.ilisema.
Kuhusu pingamizi dhidi ya mgombea wa urais kupitia chama cha CUF, Profesa Ibrahim Harun Lupumba , tume hiyo vilevile imepuuzilia mbali madai ya bwana Lissu ikisema kwamba imejiridhisha kwamba bwana Lipumba alirejesha fomu zake kwa mujibu wa sheria za tume ya uchaguzi nchini humo na kuongezea kwamba mgombea huyo ataendelea kukiwakilisha chama chake katika uchguzi huo mkuu.
Tume hiyo iliongezea kusema kwamba kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa urais na wabunge za mwaka 2020, sababu za uamuzi huo wa tume zitapeanwa kwa maandishi kwa yule aliyewasilisha pingamizi hiyo pamoja na wale waliowekewa.
''Kwa msingi wa uamuzi huu , vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu kwa kiti cha rais na makamu vinabaki kuwa kumi na tano'', taarifa hiyo ilitamatisha.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?