Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 13.08.2020: Thiago, Lacazette, Sarr, Grealish, Diawara, Pogba

Manchester City wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati wa Bayern Munich Muhispania Thiago Alcantara na wanaaminiwa kutoa ofa ya malipo zaidi ya Liverpool kwa ajili ya kumpata kijana huyo mwenye umri wa miaka 29. (SportBild - via Star)
Manchester United wamesitisha kwa muda biashara ya kuwahamisha wachezaji huku wakijaribu kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20.
Watford wako tayari kudai rekodi ya garama ya zadi ya pauni milioni 40 kwa winga Msenegal Ismaila Sarr, 22, huku Liverpool na klabu nyingine za Ulaya zikitangaza nia yao ya kumchukua. 
Sarr amewaambia waandishi wa habari nchini Senegal kwamba "kile mtu angependa " kuchezea Liverpool. (Sans Limites - via Goal)
Roma wanaweza kumbadilisha kiungo wa kati Mguinea Amadou Diawara mwenye umri wa miaka 23 na kiungo wa kati Arsenal Lucas Torreira ambaye ni raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka , 24. (Gazzetta dello Sport - via Mail)
Valencia wamezifahamisha klabu za Primia Ligi kuwaweka sokoni wachezaji wao wote isipokua mmoja ili kupata pesa. 
Jack Grealish atafanya mazungumzo kadhaa na Mkurugenzi mkuu wa Aston Villa Christian Purslow juu ya kurejea kwake kutoka mapumzikoni , huku Manchester United wakiwa bado wanania na kiungo huyo wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 24 .(Mirror)
Benfica wanaongoza katika mbio za kumsaini beki wa zamani wa Tottenham Jan Vertonghen na Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 33- anaweza kujiunga katika klabu hiyo pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Paris St-Germain Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 33.
Mkurugeni wa mchezi wa Lyon Juninho amefichua kuwa kiungo wa kati Houssem Aouar anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu, huku Arsenal, Manchester City na Juventus zote zikimfuatilia Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mail)
West Bromwich Albion na Fulham wanakimbia kusaini mkataba na mshambuliaji wa Peterborough Muingereza Ivan Toney, mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)
Juventus wamewasiliana na Arsenal juu ya uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, mwenye umri wa miaka 29.
Arsenal wako makini sana kusaini mkataba na mchezaji mwenye umri wa miaka 17 anayechezea timu ya Sporting Lisbon 17- Joelson Fernandes. Mshambuliaji huyo amepewa jina la 'Cristiano Ronaldo mpya' na the Gunners wanaweza kutoa ofay a pesa na hata kuwatoa wachezaji wake ili kupata saini . (Mirror)
Kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27, anaitarajia Manchester United ifungue mazungumzo ya mkataba pale michuano ya Ligi ya Uropa itakapokamilika. 
Napoli wanakamilisha mchakato wa kusaini mkataba wa pauni milioni 22 na Mbrazili Gabriel Magalhaes, na wanaaminiwa kwamba wamefikia makubaliano ya kibinafsi na difenda huyo wa timu ya Lille, ambayo yanaweza kuiwezesha Manchester City kumuondoa difenda Kalidou Koulibaly, mwenye umri wa miaka 29, kutoka klabu ya Italia. 
Tottenham wako tayari kuwaruhusu viungo wa kati -Waingereza Oliver Skipp mwenye umri wa miaka 19 na Jamie Bowden kuondoka kwa deni baada ya kusaini mkataba na Dane Pierre-Emile Hojbjerg, mwenye umri wa miaka 25, fkutoka Southampton. (Football Insider)
Atletico Madrid wamemtaja golikipa wa timu ya Eibar Mserbia Marko Dmitrovic, mwenye umri wa miaka 28, kuwa ndiye mlindalango wa kwanza wanayemlenga katika kipindi cha dirisha la uhamisho, ili kuwa na mlindalango wa akiba baada ya Mslovenia Jan Oblak kuhusishwa na Chelsea- . (Goal)
Leicester City ni moja ya klabu zinazohusishwa na uhamisho wa winga wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 23- David Brooks - lakini bosi mpya wa Cherries Jason Tindall anasisitiza kuwa hakutakuwa na "mauzo ya makubwa " ya wachezaji nyota wa klabu . (Leicester Mercury)
Velez Sarsfield wanania ya kumnunua mshambuliaji wa safu ya kati wa Southampton Muargentina Guido Carrillo, 29. (TyC Sports - via Daily Echo)
Meneja wa timu ya Manchester United ya vijana walio chini ya miaka 23 Neil Wood amesisistiza kuwa Mfaransa Hannibal Mejbri anayecheza safu ya kati ya vijana walio chini ya miaka ,17, atasalia katika sehemu ya timu ya vijana inayopangwa kwa ajili ya msimu ujao . (Manchester Evening News)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?