Choo unachoweza kuona kinachoendelea ndani Japani

Moja ya maeneo maarufu nchini Japani umeongeza kivutio kisicho cha kawaida ambacho ni vyoo vya umma angavu.
Mbunifu wa vyoo hivyo ambaye pia ni mhandisi Shigeru Ban, amesema vyoo hivyo ambavyo unaweza kuona mwenzio anachofanya upande wa pili au akiwa ndani vimewekwa mji wa Shibuya wenye watu wengi.
Ingawa hilo linaonekana kama kuvuka mipaka ya utamaduni hivi, lengo ni kubadilisha mitazamo ya watu kuhusu vyoo vya umma.
Mbunifu Shigeru ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Pritzker amesema katika taarifa "Vyoo angavu vimewekwa katika bustani mbili za Shibuya, ya - Yoyogi Fukamachi na Haru-no-Ogawa.
"Kuna mawili yanayotutia wasiwasi, wakati unaingia choo cha umma, hasa vilivyo maeneo ya bustani," amesema kwenye tovuti rasmi ya mradi huo, "Kwanza ni usafi, na pili ni ikiwa kuna mtu ndani au la."
Ubunifu wa Shigeru Ban unatoa ufumbuzi wa matatizo hayo mawili baada ya utengenezaji wake wa vyoo ambayo ukuta wake ni kioo - kwanza mtu anaweza kuona kinachoendelea ndani akiwa nje.
"Hili linamruhusu mtu kuangalia kama choo ni kisafi na iwapo kuna mtu anayekitumia," taarifa hiyo imesema. "Usiku, vyoo hivyo vinatoa mwanga wa kuvutia kama taa ya kandili."
Vyoo hivyo vina muonekano wa kuvutia na rangi za kupendeza.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba unaweza kusema ikiwa kioo kimeganda kwa barafu au la. Kuta zake zimewekwa kioo na kumfanya mtumiaji kuwa na hisia kwamba anaonekana anachofanya kwa nje.
Lakini mtu anapoingia ndani na kufunga mlango vioo vinabadilika na kutanda wingu fulani ili kumpa faragha.
Na hivyo basi ni muhimu sana mtu kufunga mlango - sehemu iliyo chini ya mpini wa kufungia vinginevyo, kwa nje watu watakuwa wanajionea maajabu yaani kila kitu kinachoendelea.

Katika bustani zote mbili kuna choo wa wanawake, wanaume na kile cha watu wenye ulemavu.
"Utumiaji wa vyoo vya umma Japani ni mchache sana kwasababu ya dhana kwamba ni vichafu, vina giza, vinanuka na kuogopesha''.
Ili kuondoa dhana hiyo, mji umeamua kubadilisha vyoo 17 vilivyopo miji ya Shibuya na Tokyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?