Harry Maguire: Polisi wanadai kwamba nahodha wa Manchester United alijaribu kuwahonga

Nahodha wa Manchester United Harry Maguire aliuliza polisi waliomkamata katika visiwa vya Ugiriki vya Mykonos "Je unajua mimi ni nani?" na kutaka kuwapa pesa kulingana na kesi inayoendelea kusikilizwa.
Mlinzi huyo wa Uingereza, 27, alikuwa miongoni mwa watu watatu waliokamatwa Alhamisi kwa madai ya mabishano na polisi.
Wengine waliokuwepo ni kaka yake Maguire, 28 na rafiki yake Christopher Sharman, 29.
Wote watatu wanashutumiwa kwa kuvamia polisi na kuzua vurugu.
Harry na Joe Maguire pia wanashutumia kwa madai ya kujaribu kutoa rushwa, huku Harry Maguire na Christopher Sharman wakishtumiwa kwa kutoa cheche za matusi.
Hata hivyo, watatu hao wamekanusha mashitaka dhidi yao.
Harry Maguire, ambaye Jumanne alitajwa katika kikosi cha hivi karibuni cha Gareth Southgate timu ya Uingereza, haudhurii kesi hiyo huko Syros, lakini baba yake, Alan, anahudhuria.
Anawakilishwa na Alexis Anagnostakis, wakili maarufu anayetetea haki za binadamu huko Ugiriki ambaye alitaka kesi hiyo kuahirishwa lakini ombi hilo likakataliwa na hakimu.
Anagnostakis ameiambia mahakama kwamba tukio hilo lilitokana na kitendo cha dada yake Maguire kuwekewa dawa na kundi la Kialbania na papo hapo akazimia.
Mshitakiwa aliitisha usafiri na kuomba kupelekwa hospitali lakini badala yake wakapelekwa katika kituo cha hospitali.
Mwendesha mashtaka anadai kwamba Maguire, kaka yake na rafiki yake, waliwashambulia kimwili na kimaneno maafisa wa polisi.
Polisi mmoja alidai kwamba akiwa kituoni: Maguire alimuuliza "Unajua mimi ni nani? Ni nahodha wa timu ya Manchester United, Nitajiri sana, Naweza kukupa pesa, Naweza kuwalipa, tafadhali tuachilieni tuondoke."
Wenzake waliongeza kwamba Maguire alimwambia: "Tafadhali, niache niende, mimi nitajiri, Naweza kulipa, ni kiongozi wa Manchester United."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?