Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2020

Askari walevi waua watu 12 DRC

Picha
Askari waliokuwa wamelewa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamemimina risasi na kuua watu 12 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mmoja wa wahanga anaripotiwa kuwa mtoto wa miaka miwili. Mauaji hayo yalitokea Alhamisi katika jimbo la Kivu kusini mashariki mwa nchi hiyo Kumekuwa na waandamanaji wenye hasira dhidi jeshi la Kongo katika mji wa Sange, eneo ambalo barabara nyingi zilikuwa zimefugwa. Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter Subscribe our YouTube channel

Wabunge wa Marekani waamriwa kuvaa barakoa

Picha
Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi ameamuru kuwa wabunge na wafanyakzi wote wa chombo hicho watapaswa kuvaa barakoa katika kipindi chote cha janga la virusi vya corona. Akizungumza bungeni jana Jumatano, spika Pelosi amesema anatumai wabunge na wafanyakazi wote wataheshimu sharti hilo kama ishara ya kulinda afya na usalama wa kila mmoja ndani ya majengo ya Bunge. Uamuzi huo umefikiwa baada ya mbunge wa chama cha Republican Louie Gohmert aliyepinga vikali uvaaji barakoa kutangaza kuwa ameambukizwa virusi vya corona jana Jumatano. Kulingana na Pelosi, chini ya kanuni hiyo mpya wabunge wataruhusiwa tu kuondoa barakoa wakati wa kuhutubia au kutoa michango mbele ya Bunge. Hayo yanajiri wakati Marekani imefikisha idadi ya vifo 150,000 vya COVID-19 ambayo ni kubwa kuliko taifa lingine lolote duniani. Barani Ulaya ambako mataifa kadhaa yametangaza vizuizi vya kusafiri kwenda na kutoka Uhispania, viongozi wake wamejikuta katika vita ya maneno juu ya iwapo kuna umakini kati

Ibada ya Hijja yaanza chini ya kiwingu cha COVID-19

Picha
Waumini wa dini ya kiislamu wanaanza ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia ambayo itashuhudia idadi ndogo kabisa ya mahujaji katika historia kutokana na janga la virusi vya corona Ibada hiyo ya kila mwaka inaanza leo katika mji mtukufu wa Makka chini ya kiwingu cha janga la virusi vya corona ambalo limesababisha  waislamu wasiopindukia 10,000 pekee kuwa ndiyo wataruhusiwa kushiriki tukio hilo la kidini la siku tano. Idadi hiyo waumini ambao wamechaguliwa kwa mchujo maalum ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na mahujaji milioni 2.5 waliohudhuria ibada ya hijja mwaka uliopita. Theluthi mbili ya mahujaji waliochaguliwa mwaka huu ni wageni wanaoishi nchini Saudi Arabia na serikali imesema kuna uwakilishi wa mataifa 160 ambayo kwa kawaida waumini wake wa kiislamu kila mwaka hushiriki ibada hiyo. Hijja, moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu na ambayo muumuni mwenye uwezo anapaswa kuitimiza walau mara moja katika maisha yake kwa kawaida ni moja ya mikusanyiko mikubwa sana ya kidi

Najib Razak wa Malaysia kukata rufaa hukumu ya ufisadi

Picha
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak, atakata ru faa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu mjini Kuala Lumpur kumtia hatiani kwa mashitaka ya ufisadi dhidi yake na kumhukumu kifungo cha miaka 12. Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la mahakama mjini Kuala Lumpur mchana wa Jumanne (29 Julai), Najib alisema kuwa mashitaka dhidi yake yalikuwa ya kisiasa na kwamba hahusiki na kadhiya hiyo ya ubadhirifu wa kiasi cha mabilioni ya dola yaliyotoweka kwenye mfuko wa maendeleo wa serikali, maarufu kama kashfa ya 1MDB: "Kama ilivyo kawaida, mtu hutegemea kheri lakini hujiandaa kwa shari. Na huu si mwisho wa dunia. Bado kuna nafasi ya kuukatia rufaa uamuzi huu, nasi tutaelekea huko na naamini tutafanikiwa. Kwa wafuasi wangu, natarajia wataendelea kuniunga mkono na kuniamini na kuamini mapambano yetu na kutovunjika moyo," alisema. Awali Jaji Muhammad Nazlan Ghazali wa Mahakama Kuu mjini Kuala Lumpur alisema ameridhika na hoja zilizowasilishwa na upande wa mashit

Serikali zachukua hatua kuzuia wimbi jipya la COVID-19

Picha
Serikali kadhaa duniani zimechukua hatua za kurejesha vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona zikijaribu kuepuka wimbi jipya la maambukizi wakati idadi ya vifo vilivyotokana na COVID-19 imepindukia 650,000. Mataifa ya Ulaya yamejikuta njia panda wakati yanajaribu kurekebisha athari za kiuchumi za janga la virusi vya corona kwa kufungua tena shughuli za kawaida ikiwemo utalii huku yakijilinda na wimbi jipya la maambukizi ya COVID-19. Sekta ya utalii ya Uhispania jana ilipata baada ya moja ya kampuni kubwa ya utalii kusitisha mipango ya safari kwa raia wa Uingereza kufuatia uamuzi wa serikali mjini London wa kurejesha sharti la kuwaweka watu karantini kwa muda wa wiki mbili pindi wanaporejea kutoka nje. Kampuni mashuhuri ya utalii ya TUI imetangaza kufuta safari zote za watalii wa Uingereza kuanzia Agosti 9 ikisema kanuni ya kuwaweka watu karantini itazuia walio wengi kufanya safari nje ya Uingereza. Ujerumani kuwapima kwa lazima wasafiri  Nchini Ujerumani se

China yaripoti maambukizi mapya 46 ya virusi vya corona

Picha
China imeripoti kesi mpya za maambukizi ya virusi vya corona katika  China bara  Julai 25, ikiwa  ni ongezeko  kutoka  kesi 34 siku moja kabla, tume  ya  afya  imesema leo Jumapili(26.07.2020). Miongoni mwa  maabukizi  hayo  mapya, 22 yalikuwa  katika  jimbo  la  magharibi  ya  mbali la  Xinjiang, kwa mujibu wa  taarifa  iliyotolewa  na  tume ya  taifa  ya  afya. C hina iliripoti kesi mbili mpya za watu walioonesha dalili, ikiwa  ni chini kutoka  watu 74  siku moja  kabla. Hadi Jumamosi, China  bara  ilikuwa  na  kesi  za  maambukizi ya virusi  vya  corona  83,830 zilizothibitishwa, mamlaka hiyo  ya afya  imesema. Vifo  kutokana  na  COVID-19 vimefikia jumla  ya  watu 4,634. Marekani  siku ya Jumamosi (25.07.2020) ilirekodi maambukizi  mapya  ya watu 68,212 katika  masaa  24 yaliyopita, chuo kikuu  cha  Johns Hopkins  kiliripoti  katika  hesabu  zake za  kila  siku. Hii  inafikisha  jumla  ya  idadi  ya  kesi  za  maambukizi  katika  taifa  hilo lililoathirika  zaidi 

Wabunge 15 wa Zambia wakutwa na virusi vya corona

Picha
Waziri wa Afya wa Zambia Chitalu Chilufya amesema baada ya zoezi la lazima la upimaji wa virusi vya corona katika bunge la nchi hiyo, wabunge 15 wamekutwa na maambukizi. Amri ya upimaji huo ilitolewa baada ya wabunge wawili kufariki dunia juma lililopita. Mmoja miongoni mwa hao aliugua ugonjwa wa COVID-19, hadi kipindi hicho binge la Zambia lilikuwa na Wabunge 158. Katika hatua nyingine Msemaji wa Serikali ya Kenya Cyrus Oguna pia amethibitishwa kuwa na virusi vya corona. Katika ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa aliona dalili na kwa sasa anapatiwa matibabu katika eneo alilojitenga. Mawaziri wa Afrika ya Kusini pia waambukizwa Nchini Afrika Kusini mawaziri wawili walifikishwa hospitali baada ya kupata maambukizi. Hadi wakati huu Zambia ina visa 3,584 vya  maambukizi, wakati Kenya 15,601. Shirika la Afya Dunia WHO hivi karibuni lilionya kutokana na kuchelea kuanza kwa mripuko huo barani Afrika visa vyake katika kipindi hiki vinaongezeka kwa kasi.. Rekodi kama hizi z

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 24.07.2020: Cavani, Torres, Gimenez, Havertz, Alcantara, Zaniolo, Balotelli

Picha
Benfica imesitisha azma yake ya kumsaka mshambuliaji Edinson Cavani, 33, huku mchezaji huyo aliyekuwa Paris St-Germain akidai karibu pauni milioni 18 kwa kila msimu. (A Bola - in Portuguese) Chelsea imekuwa ikimfuatilia mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25, huku kocha Frank Lampard akiwa anafuatilia kutatua mapungufu ya upande wa ulinzi wa kikosi chake. (Telegraph - subscription required) Leroy Sane, 24, alionekana kuthibitisha wakati anatambulishwa Bayern Munich kwamba mchezaji mwenzake wa Ujerumani Kai Havertz, 21, ianaelekea Chelsea kutoka Bayer Leverkusen msimu huu. Chelsea na ajenti wa Havertz wamefikia makubaliano ya kibinafsi kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Leverkusen. (Nicolo Schira, via Star) Brighton haina mpango wowote wa kumuuza mlinzi wa Uingereza Ben White, 22, kwa Leeds United, ambapo amekuwa kwa mkopo msimu huu. (Mail) Jesse Lingard, 27, amemtaka kiungo wa kati raia mwenzake wa Uingereza Jadon Sancho, 20, kuondoka Borussi

WHO kuzifanyia utafiti dawa za mitishamba juu ya COVID-19

Picha
Shirika  la  afya  ulimwenguni WHO na  kituo cha udhibiti wa  magonjwa  barani Afrika CDC yameanzisha juhudi kuangalia uwezekano wa madawa ya mitishamba katika kupambana  na  janga  la  virusi vya  corona. Jopo hilo  jipya la ushauri litaunga mkono nchi katika majaribio ya kitabibu, utafiti mwingine na utengenezaji wa dawa nyingine za  kienyeji  wakati hivi  sasa  janga likisambaa kwa  kasi  katika  baadhi  ya sehemu  za  bara la  Afrika. Kesi zilizothibitishwa  katika  bara  hilo zimekaribia  kufika  750,000, zaidi  ya  nusu zikiorodheshwa  nchini  Afrika  kusini. Taarifa  ya  WHO imesema  dawa  za  asili, zina  faida nyingi na  bara  hilo lina  historia  ndefu  ya  matumizi yake. Mkuu  wa  WHO  barani  Afrika Matshidiso Moeti amesema  utafiti unapaswa  kuwekwa katika  misingi  ya kisayansi. Mataifa  kadhaa  yalionesha  shauku  baada  ya  rais  wa Madagascar kutangaza  dawa  ya  mitishamba  kama sehemu ya  taifa  hilo  la  kisiwani  kupambana  na  janga la  virusi  vya  c

'Mende wa baharini': Kombamwiko mkubwa apatikana chini ya bahari

Picha
Mwaka huu taarifa za kisayansi zimehusisha mambo tofauti, dunia kukabiliwa na janga la virusi vya corona na wimbi la nzige wanaokula mazao shambani. Lakini sasa hivi wanasayansi nchini Indonesia wametangaza kwamba wamepata familia ya mdudu mkubwa zaidi katika kina cha chini cha bahari - ambaye wanamueleza kuwa ni kombamwiko mkubwa wa baharini. Mdudu huyo ni jamii ya isopodi wenye uhusiano wa mbali na kaa na kamba ambao wako tambarare, miili yao ina ugumu mfano wa aina fulani ya chawa - anayeishi chini kabisa ya bahari. Kombamwiko au mende huyo wa baharini alipatikana katika mlango bahari wa Sunda kati ya visiwa vya Java na Sumatra, kati ya mita 957 na 1,259 chini ya usawa wa bahari. Kawaida wadudu hao wanapokua, ukubwa wao huwa ni sentimita 33 na wanachukuliwa kwamba ndio wakubwa zaidi. Lakini kuna spishi nyengine ya wadudu hao ambao ukubwa wao kuanzia kichwani hadi kwenye mkia huwa ni sentimita 50. Ukubwa wake ni wa juu zaidi," amesema msimamizi wa utafiti h

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Picha
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya hatimaye Jumanne asubuhi walifikia makubaliano ya yuro bilioni 750 za kuufufua uchumi wao. Pesa hizi ni za kukabiliana na athari zilizotokana na janga la virusi vya corona. Viongozi hao walioonekana wenye uchovu wamekubaliana bajeti ya yuro trilioni 1.82 pia pamoja na hizo pesa za kufufua uchumi baada ya janga la virusi vya corona. Hatua hii imefikiwa kufuatia majadiliano ya siku nne ya usiku na mchana yaliyojawa na makabiliano na ubishi mkali kuhusiana na pesa na nguvu katika mojawapa ya mkutano wao mrefu zaidi wa kilele kuwahi kushuhudiwa. Hizo bilioni 750 zitatolewa kama mkopo kwa nchi zilizoathirika  vibaya zaidi na janga hilo huku makubaliano yakiafikiwa pia kuhusiana na bajeti hiyo ya miaka saba ya zaidi ya trilioni moja. Mkutano ulitarajiwa kuisha Jumamosi Charles Michel ni mwenyekiti wa mkutano huo wa kilele. "Tumeonyesha imani kwa mustakabali wetu na makubaliano haya yanaonyesha kuwa Ulaya ni nguvu ya vitendo. Tumejadiliana