Coronavirus: Uganda yathibitisha kuwa na wagonjwa 44 wa Covid 19
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza visa vipya 11 vya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo, wote wakiwa wanakwaya wa kwaya maarufu nchini humo 'Watoto Children's Choir. Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani. Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza. Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44. Katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya corona, tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma. Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku. Mtu yeyote anayehitaji huduma za dha...