Rais Magufuli amesema Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola ameamuandikia barua ya kujiuzulu

Rais John Pombe Magufuli amesema amepokea na kuridhia ombi la kutaka kujiuzulu alilowasilisha kwa barua.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi nyumba za askari magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, kingozi huyo amesema kuwa licha ya kuwa rafiki mkubwa wa kiongozi huyo, hafai kusalia katika ofisi yake kutokana na makosa aliyoyafanya.

Akionesha kusikitishwa kwake rais Magufuli alisema: ''Tuna changamoto nyingi na hasa hii ya mambo ya ndani, kama kuna wizara inanitesa ni wizara ya mambo ya ndani, nataka muelewe hivyo watanzania, inatesa sana''.

''Katika kipindi cha miaka minne kuna tume nyingi tu zimeundwa kwa ajili ya kuchunguza wizara ya mambo ya ndani kwa miradi ya hovyo iliyokuwa ikifanyika, na mimi nilitegemea watu watakuwa wanajifunza.Ninajua leo waziri wa mambo ya ndani haonekani hapa ameshaleta barua ya kujiuzulu na nimeshamkubalia na nimempongeza kwa hilo''.

Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa wizara ya mambo ya ndani wenye thamani ya Euro milioni 408 , mradi huo umetayarishwa na kusainiwa na Kamishna Jenrali wa zimamoto, haujapangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na Bunge. ''

''Wakati wa vikao na kampuni moja wahusika wote watanzania walipokuwa wanakwenda kwenye majadiliano walikuwa wanalipwa kwanza sitting allowance ya dola 800 na bado wanalipiwa tiketi za ndege, mradi wa hovyo wameusaini memorandum of understanding lakini kilichoelezwa ndani ni kuwa iwapo mkataba ukitaka kuuvunja yale yaliyoanza kutekelezwa lazima yaendelee kutekelezwa.'' Alieleza rais Magufuli.

''Urafiki upo lakini katika suala la kazi siwezi kuruhusu na hivyo ndivyo nilivyo. Nakupenda sana lakini katika hili hapana , Kangi Lugola mwanafunzi wangu umenisifia sana hapa nakushukuru lakini katika hili hapana.....na lazima niwe mkweli sitaki kuwa mnafiki ,unafiki ni mbaya , Andegenye umefanya kazi nzuri sana lakini katika hili ulilolifanya hapana. Unakwenda Ulaya kutia saini miradi ambayo haijapitishwa na bunge'',alisema .

Ametoa onyo kwa wale wote aliowateua au kuteuliwa na wasaidizi wake watambue kuwa wana jukumu kubwa la kuwafanyia kazi wananchi.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga