Papa Benedict amemtaka Papa Francis kutolegeza kamba kuhusu sheria ya useja

Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa wakati ambapo mrithi wake anafikiria kulegeza marufuku hiyo kwa wanaume wanaooa ambao wanahudumu kama makasisi.

Papa Benedict amesema hayo katika kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah.

Hatua hiyo inawadia kujibu pendekezo la kuruhusu wanaume waliooa kutawazwa kama makasisi katika eneo la Amazon.

Papa Benedict, ambaye alistaafu mwaka 2013, amesema hakuweza kunyamazia suala hilo.

Katika kitabu hicho, Papa Benedict amesema kutofunga ndoa kwa makasisi ni utamaduni wa kale ambao umekuwepo kwa karne nyingi tu ndani ya kanisa hilo, una umuhimu mkubwa kwasababu unaruhusu makasisi kuangazia majukumu yao.

Papa Benedict mwenye umri wa miaka 92 amesema "Halionekani kuwa jambo linalowezekano kutimiza majukumu ya ukasisi na ndoa kwa wakati mmoja".

Ni nadra sana kwa Papa Benedict ambaye alikuwa wa askofu wa kwanza kujiuzulu katika kipindi cha karibia miaka 600, kuingilia masuala ya ukasisi.

Vatican bado haijasema lolote kuhusu na kitabu hicho, ambacho kiliangaziwa kidogo katika gazeti la Ufaransa la Le Figaro kabla ya kuchapishwa leo Jumatatu.

Wachambuzi wa Vatican wameshangazwa na hatua ya Papa Benedict kuingilia suala hilo, na kuongeza kwamba hatua ya Papa Benedict inavunja utamaduni ambao umekuwepo.

"Papa Benedict siyo kwamba anavunja ukimya wake kwasababu hakuhisi kwamba anavunja ahadi kwa kiapo alichokula. isipokuwa amekiuka kabisa,"Massimo Faggioli, mwanahistoria na mwanatheolojia. katika chuo kikuu cha Villanova ameandika katika mtandao wa Twitter.

Maoni ya papa Benedikto yalielezewa kama ya kushangaza na Joshua McElwee, mwanahabari wa gazeti la National Catholic Reporter.

Lakini tangu wakati huo, amekuwa akitoa maoni yake kupitia Makala, vitabu na mahojiano, akitaka papa Francis kuchukua njia tofauti, ambaye anaonekana kupendelea mabadiliko. Papa Benedict bado anaishi Vatican katika yaliyokuwa makao ya watawa.

Nini kilichopendekezwa kubadilika katika useja wa kidini?

Oktoba, Maaskofu wa Kikatoliki kutoka kila pembe ya dunia walifanya mkutano kujadiliana hatma ya kanisa hilo katika eneo la Amazon.

Katika kilele cha mkutano huo, kulitolewa ripoti yenye kuangazia m

asuala yanayoathiri Kanisa hilo na ndani yake, kukawa na pendekezo la kuruhusu wanaume walioa katika maeneo ya vijijini ya Amazon, watawazwe kuwa makasisi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?