Mtoto aliyesafirishwa kwa siri apatikana amekufa Paris

Mwili wa mtoto mwenye umri wa karibia miaka 10 umepatikana katika sehemu ya gurudumu la ndege ambayo ilikuwa imewasili Paris kutoka Abidjan, vyanzo vilivyo karibu na uchunguzi vimeiambia Shirika la Habari la Ufaransa.

Shirika la ndege la Ufaransa limethibitisha kwamba mwili wa mtoto huyo aliyekuwa anaingizwa nchini humo kwa njia haramu, ulipatikana katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mapema asubuhi.

Mwili huo umegunduliw
a kwenye eneo la magurudumu la ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Ivory Coast, shirika hilo limesema.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea.

"Shirika hilo la ndege limetuma rambirambi zake na kuonyesha kuchukizwa na tukio hilo," Shirika la ndege la Ufaransa limeandika hivyo katika mtandao wa Twitter bila kuweka umri wa mtu aliyepatikana.

Ndege ya shirika hilo, Boeing 777 ilikuwa imetoka Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast,siku ya Jumanne jioni.

Chanzo cha usalama cha Ivory Coast kimeambia Shirika la Habari la AFP: "Mbali na kwamba tukio hili linagusa mioyo ya wengi, limeonyesha utepetevu wa kiusalama katika uwanja wa ndege wa Abidjan."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?