Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.05.2023
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Dakika 30 zilizopita Tottenham wamedhamiria kuzima majaribio ya Manchester United ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 29, msimu huu wa joto, huku mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akigoma kumuuza Kane kwa timu pinzani ya Ligi kuu England. (Mirror) Erik ten Hag ana imani kuwa anaweza kumshawishi kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 ajiunge na Manchester United kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake kwenye usajili wa majira ya joto. (Telegraph) Bayern Munich wako tayari kulipa pauni milioni 95 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, huku timu hiyo ya Ujerumani ikiwa na nia ya kuipiku Arsenal katika kuinasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mirror) Paris St-Germain wana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 24. (Mail) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Martin Odegaard Tottenham, Newcastle n...