Nilikuwa katika uwanja wa Etihad siku ya Jumamosi wakati Raheem Sterling alipopoteza nafasi nzuri dhidi ya Watford. Ungewasikia mashabiki walionizunguka walivyokuwa wakigugunia na kupiga kelele 'hafai' au 'mtoe'. Manchester City walikuwa wanaongoza mabao 3-1 wakati huo na Sterling alikuwa akicheza vizuri sana. Hilo lilikuwa shuti lake la kwanza katika mchezo huo na, ingawa sikusema chochote kwa watu walio karibu nami, nilikuwa nikifikiria tu kwamba walihitaji kutulia na kuwa na subra. Hata hivyo hilo sio jambo jipya. Sterling anaonekana kushambuliwa zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa City. Haijalishi ni mabao mangapi anayofunga au mambo mazuri anayofanya katika mchezo - ikiwa atakosa, ni kawaida kwa Sterling sivyo? CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Sterling amefunga mabao 10 katika ligi kuu England katika michezo 26 msimu huu, goli moja nyuma ya wachezaji wanaoongoza kwa mabao msimu kwenye timu ya City, Riyad Mahrez and Kevin de Bruyne wenye mab...