Urusi yatoa masharti ya kusitisha vita Ukrane.
Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni "wakati wowote" ikiwa Ukraine itatimiza masharti ya
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Ukraine lazima itambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama mataifa huru.
Mbali na hayo, Peskov anasema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote (kama vile Nato, kwa mfano).
Anaongeza kuwa Urusi itamaliza "kuondoa jeshi" kwa Ukraine, na ikiwa masharti haya yatatimizwa hatua za kijeshi za Urusi "zitakoma mara moja".
Msemaji wa Kremlin amesisitiza kuwa Urusi haitaki kutoa madai yoyote zaidi ya eneo nchini Ukraine.
Maoni
Chapisha Maoni