Ndege 4 za Urusi zaangushwa Ukraine huku baadhi ya wanajeshi wakikataa kutekeleza amri
Baadhi ya wanajeshi wa Urusi wakataa amri , ndege nne zaangushwa - vimesema vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine
Wakati Ukraine ikielekea katika siku ya ishirini ya uvamizi wa Urusi katika ardhi yake, Maafisa wakuu wa jeshi la Ukraine wametoa taarifa yao kila alfajiri
Vikosi vya Urusi vinasalia kushambulia maeneo kadhaa nchini Ukraine , na vimeshindwa kupiga hatua zaidi
Hata hivyo wanajeshi wa Urusi wameendelea kufanya mashambulizi ya makombora na mabomu kwenye miundombinu muhimu
Wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakitumia vituo vya afya katika maeneo yanayokaliwa kuwatibu waliojeruhiwa
Helikopta nne za Urusi ziliangushwa na vikosi vya Ukraine
Vikosi vya Ukraine vimefanikiwa kuzuia majaribio ya Urusi ya kuuteka mji wa bandari wa kusini wa Mariupol uliokuwa na ushindani mkubwa na hakujawa na dalili zozote za kutua kwa jeshi la Urusi katika eneo la Bahari Nyeusi.
Baadhi ya wanajeshi wa Urusi wanakataa kutekeleza amri.
Maoni
Chapisha Maoni