Mbwa aliyewaokoa wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakishambuliwa na al-Qaeda Afghanistan
Mbwa wa jeshi aliyekimbia na bila kuogopa risasi zilizokuwa zikifyatuliwa na adui ili kuokoa maisha ya wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakipigana na al-Qaeda nchini Afghanistan anatarajiwa kutuzwa tuzo ya juu zaidi ya wanyama. Wakati wa uvamizi , mbwa huyo aina ya Malinois kutoka Ubelgiji kwa Jina Kuno alimkabili mpiganaji mmoja aliyekuwa na bunduki na alipigwa risasi katika miguu yake yote miwili. Baada ya kupoteza mguu wake mmoja kutokana na shambulio hilo la risasi , alikuwa mbwa wa kwanza wa Uingereza kuwekwa miguu bandia. Mbwa huyo mwenye umri wa miaka minne atapokea medali yake ya Dickin kutoka kwa shirika la hisani linaloshughulikia wanyama wagonjwa PDSA. Akiwa mwanajeshi mstaafu na kupelekwa nyumbani Uingereza, Kuno ambaye alifunzwa kufichua vilipuzi , silaha na kuwakabili maadui atatuzwa medali hiyo katika sherehe mwezi Novemba. Kuno na wamiliki wake walikuwa wamepelekwa nchini Afghanistan kusaidia vikosi maalum wakati wa shambulio la usiku lililokuw...