Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2020

Paul Makonda apigwa marufuku kuingia Marekani

Picha
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, apigwa marufuku kuingia Marekani. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani leo Ijumaa, Januari 31 2020 marufuku hiyo pia inamhusisha mke wa Makonda Bi Mary Felix Massenge. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Makonda anashutumiwa kwa kushiriki katika ukandamizaji wa haki za binaadamu. Ukandamizaji wa haki ambao Makonda anashutumiwa kuutenda ni pamoja na kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu. "Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wagonjwa wanne wanaoshukiwa kuwa na virusi ya Corona wachunguzwa Ethiopia

Picha
Watu wanne wanaoshukiwa kuwa na virusi hatari vya corona wametengwa na wanafanyiwa uchunguzi zaidi katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa. Tangu Jumatano iliyopita abiria wote wanaowasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Bole kutoka China wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi kubaini kama wanaambukizwa virusi hivyo. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Addis Ababa, Waziri wa Afya wa Ethiopia Dkt. Liya Tadesse, amesema kuwa wagonjwa wanne wanaoshukiwa kuwa na virusi hatari vya corona wametengwa na wanafanyiwa uchunguzi zaidi. Wagonjwa wote ni raia wa Ethiopia na kwamba watatu kati yao ni wanafunzi kutoka chuo kikuu cha eneo la Wuhan nchini China, ambako ni chimbuko la mlipuko wa virusi hivyo. Maafisa wa afya wa Ethiopia wanasema kuwa sampuli ya damu imetolewa kwa wagonjwa hao na inatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi. Kufikia sasa shirika la ndege la Ethiopia limewafanyia uchunguzi zaidi ya abiria elfu 22. Awali mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na virusi vya C

Rais Magufuli amesema Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola ameamuandikia barua ya kujiuzulu

Picha
Rais John Pombe Magufuli amesema amepokea na kuridhia ombi la kutaka kujiuzulu alilowasilisha kwa barua. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi nyumba za askari magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, kingozi huyo amesema kuwa licha ya kuwa rafiki mkubwa wa kiongozi huyo, hafai kusalia katika ofisi yake kutokana na makosa aliyoyafanya. Akionesha kusikitishwa kwake rais Magufuli alisema: ''Tuna changamoto nyingi na hasa hii ya mambo ya ndani, kama kuna wizara inanitesa ni wizara ya mambo ya ndani, nataka muelewe hivyo watanzania, inatesa sana''. ''Katika kipindi cha miaka minne kuna tume nyingi tu zimeundwa kwa ajili ya kuchunguza wizara ya mambo ya ndani kwa miradi ya hovyo iliyokuwa ikifanyika, na mimi nilitegemea watu watakuwa wanajifunza.Ninajua leo waziri wa mambo ya ndani haonekani hapa ameshaleta barua ya kujiuzulu na nimeshamkubalia na nimempongeza kwa hilo''. Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa wizara ya mambo ya

Je, serikali ya Dolnald Trump kuzuia raia wa Tanzania kuingia Marekani?

Picha
Nchi nne za Afrika ikiwemo Tanzania zinaweza kupigwa marufuku raia wake kuingia nchini Mare kani, vyombo vya habari vinaripoti. Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani vimeripoti vyanzo vinavyodai kuiona orodha ya nchi hizo ambayo inaweza kuwekwa wazi na serikali ya nchi hiyo Jumatatu ijayo, Januari 27. Nchi nyengine za Afrika kwa mujibu wa ripoti hizo ni Nigeria, Sudan na Eritrea. Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa Davos nchini Uswizi amelithibitishia gazeti la Wall Street Journal kuwa ana mpango wa kuongeza idadi ya nchi kwenye orodha ya zuio la kuingia Marekani, lakini aligoma kuzitaja nchi hizo. Kwa mujibu wa gazeti la Politico, rasimu ya nchi hizo bado haijakuwa rasmi na inaweza kubadilishwa. Magazeti hayo pia, likiwemo la New York Times yanaripoti kuwa bado kuna mabishano baina ya maafisa wa Ikulu ya White House juu ya kujumuishwa ama kutolewa kwa nchi moja au mbili kwenye orodha hiyo. Nchi nyengine nje ya Afrika ambazo zinasadikiwa kuwemo kwenye rasimu hiyo ya or

Aston Villa yamsajili Mtanzania Mbwana Samatta

Picha
Aston Villa inafurahi kutangaza rasmi kumsaini Mbwana Samatta kutoka KRC Genk.Mshambuliaji huyo amemwaga wino kwenye mpango wa miaka minne unusu chini ya idhini ya kibali cha kazi na idhini ya kimataifa. "Nimefurahi sana," Samatta alisema. "Ni hatua kubwa kwangu katika kazi yangu. Ni hatua kubwa kwa nchi yangu pia. Kila mtu alikuwa akitafuta Mtanzania kucheza kwenye Ligi Kuu za kimataifa hatimaye nimewatoa kimasomaso. "Ninajua mengi juu ya Aston Villa. Nilikuwa nikitazama rekodi ya Ligi kuu wakati Gabby Agbonlahor alipokuwa hapa." Mbwana Samatta amefunga mabao 10 kwa timu yake ya awali ya Genk katika mashindano yote msimu huu ikiwa ni pamoja na bao alilolifunga huko Anfield dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa. Meneja wa villa Dean Smith alionesha furaha yake baada ya saini kuwekwa ."Nimefurahiya sana tumefanikiwa kumleta Mbwana Samatta klabuni," "Amefunga mabao katika kipindi chote cha kazi yake na ninatarajia kufanya kazi nay

Mbwana Samatta: Kauli ya 'Haina Kufeli' imenifaa maishani na katika kandanda

Picha
Jina la Mtanzania Mbwana Ally Samatta linagonga tena vichwa vya habari katika ulimwengu wa soka. Baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Ubelgiji na kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya KRC Genk ya Ubelgiji, na hivi sasa ripoti zinaeleza kuwa anatarajiwa kusajiliwa na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi ya EPL. Alianzaje na nini kilimpa msukumo wa kuendelea kujiboresha? Samatta alibainisha majibu ya maswali hayo alipofanya mahojiano na mwandishi wa Newsday Swahili mwaka 2018.

Misri, Ethiopia, Sudan zakubaliana matumizi ya mto Nile

Picha
Misri, Ethiopia na Sudan wamefikia makuabliano ya awali ya kujaza maji na shughuli nyengine kwenye bawa kubwa linalojengwa mto Nile Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi tatu, pamoja na Marekani na Benki ya Dunia, imesema kwamba washiriki wanaojadiliana wamekubaliana kujaza bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia wakati wa msimu mvua kati ya miezi ya Julai na Agosti. Hata hivyo taarifa hiyo haikusema lolote kuhusu masuala ya msingi yanayozunguka mgogoro huo ambayo ni kasi ya kujaza bwawa hilo. Ethiopia inataka kujaza bawa la Grand Renaissance kwa miaka 6 lakini Misri imependekeza angalau mradi huo uchukue kipindi cha miaka 10 - kwa kuhofia kwamba kuchukua kipindi kifupi kutaathiri mtiririko wa maji ya mto Nile ambayo inategemea asilimia 90 ya maji ya mto huo. Makubaliano ya mwisho yatatiwa saini Januari 28-29, wakati ambapo mawaziri kutoka nchi tatu watakuwa wanakutana Washington. Makubaliano ya awali ambayo yalifikiwa na waziri wa fedha wa Marekani na Rais wa benki

Uasi Sudan: Jeshi lakabiliana na waasi jijini Khartoum

Picha
Vikosi vilivyokuwa vitiifu kwa rais Omar al Bashir vyafatua risasi katika jaribio la uasi Khartoum Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir, ripoti zinaeleza. Mapambano yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko ilisikika. Kitengo hicho cha usalama wa taofa kwa sasa kinavunjwa. Serikali inaadai kuwa uasi huo umechochewa na mlipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo. Japo Dagalo anasema hachukulii jambo hilo kama jaribio la mapinduzi, lakini amesema jambo hilo halivumiliki. Kumekuwa na wasiwasi juu ya uwezekao wa baadhi ya viongozi waliokuwa na ushawishi wakati wa Bashir kujaribu kutatiz

Papa Benedict amemtaka Papa Francis kutolegeza kamba kuhusu sheria ya useja

Picha
Kiongozi mstaafu wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 ametetea suala la makasisi kutofunga ndoa wakati ambapo mrithi wake anafikiria kulegeza marufuku hiyo kwa wanaume wanaooa ambao wanahudumu kama makasisi. Papa Benedict amesema hayo katika kitabu walichoshirikiana na Kadinali Robert Sarah. Hatua hiyo inawadia kujibu pendekezo la kuruhusu wanaume waliooa kutawazwa kama makasisi katika eneo la Amazon. Papa Benedict, ambaye alistaafu mwaka 2013, amesema hakuweza kunyamazia suala hilo. Katika kitabu hicho, Papa Benedict amesema kutofunga ndoa kwa makasisi ni utamaduni wa kale ambao umekuwepo kwa karne nyingi tu ndani ya kanisa hilo, una umuhimu mkubwa kwasababu unaruhusu makasisi kuangazia majukumu yao. Papa Benedict mwenye umri wa miaka 92 amesema "Halionekani kuwa jambo linalowezekano kutimiza majukumu ya ukasisi na ndoa kwa wakati mmoja". Ni nadra sana kwa Papa Benedict ambaye alikuwa wa askofu wa kwanza kujiuzulu katika kipindi cha karibia miaka 600, kuingili

Mzozo wa Iran: Marekani iko 'tayari kufanya mazungumzo' na Tehran

Picha
Marekani imesema iko "tayari kujadiliana na Iran bila masharti" baada uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya jenerali Qasim Soleimani. Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani ilijitetea kuwa ilimuua jenerali wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda Iran ilijibu hatua hiyo kwa kushambulia kwa makombora kambi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa. Jenerali Soleimani ilichukuliwa kuwa afisa wa pili wa ngazi ya juu nchini Iran. Kama mkuu wa kikosi maalum cha Quds Force, katika jeshi la ulinzi la Revolutionary Guards' alilikuwa mtekelezaji wasera za Iran katika eneo la mashariki ya kati. Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa "kofi la usoni" kwa Marekani na kutoa wito kwa nchi hiyo kuondoka mashariki ya kati. Shambulio dhidi ya Soleimani pia liliwaua wanachama wa kundi la waasi wanaounga mkono Iran ambao pia wamesema watalipiza kisasi. Hatah

Mtoto aliyesafirishwa kwa siri apatikana amekufa Paris

Picha
Mwili wa mtoto mwenye umri wa karibia miaka 10 umepatikana katika sehemu ya gurudumu la ndege ambayo ilikuwa imewasili Paris kutoka Abidjan, vyanzo vilivyo karibu na uchunguzi vimeiambia Shirika la Habari la Ufaransa. Shirika la ndege la Ufaransa limethibitisha kwamba mwili wa mtoto huyo aliyekuwa anaingizwa nchini humo kwa njia haramu, ulipatikana katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mapema asubuhi. Mwili huo umegunduliw a kwenye eneo la magurudumu la ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Ivory Coast, shirika hilo limesema. Kwa sasa uchunguzi unaendelea. "Shirika hilo la ndege limetuma rambirambi zake na kuonyesha kuchukizwa na tukio hilo," Shirika la ndege la Ufaransa limeandika hivyo katika mtandao wa Twitter bila kuweka umri wa mtu aliyepatikana. Ndege ya shirika hilo, Boeing 777 ilikuwa imetoka Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast,siku ya Jumanne jioni. Chanzo cha usalama cha Ivory Coast kimeambia Shirika la Habari la AFP: "Mbali na kwamba tukio hili linag

Nini kinaweza kutokea baada ya mauaji ya Qasem Soleiman?

Picha
Kuuliwa kwa jenerali Qasem Soleimani, kiongozi wa kikosi maalum cha jeshi la ulinzi wa Iran nje ya nchi kinachofahamika kama Quds, kinachohusishwa katika mzozo wa kiwango cha chini kati ya Marekani na Iran, huenda matokeo yake lazimu kuwa na mwisho mbaya. Kulipiza kisasi kutokana na mauaji hayo ni jambo ambalo linatarajiwa. Mlolongo wa hatua za kulipiza kisasi kunaweza kuzifikisha nchi hizo mbili kufikia karibu katika mzozo wa moja kwa moja. Siku za mbeleni, Marekani inaweza kutakiwa kuhojiwa na Iraq. Na harakati za Rais Trump katika kanda hiyo-kama zipo zozote - zitafuatiliwa kwa karibu zaidi ya awali. Philip Gordon, ambaye ni mratibu wa Ikulu ya Marekani na mataifa ya Uarabuni wakati wa utawala wa Obama, kuelezea mauaji hayo ni uhalalisho wa vita kati ya Wamarekani na Wairan. Jeshi la Quds ni sehemu ya jeshi la usalama la Iran ambalo linafanya kazi katika mataifa ya kigeni. Kwa miaka mingi Lebanon, Iraq, Syria au maeneo mengine, Soleimani alikuwa kiongozi mkuu katika k

Norwich na Brighton zamnyatia Mbwana Samatta wa Tanzania

Picha
Klabu za Norwich na Brighton zimeulizia kuhusu mshambuliaji wa Genk na Tanzania Mbwana Samatta. Akiwa na thamani ya £10m, amefunga magoli 10 msimu huu matatu katika ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool na RB Salzburg. Pia mchezaji huyo amevutia klabu kama vile Eintracht Frankfurt ya Ujerumani na Lazio ya Itali. Samatta mwenye umri wa miaka 27 alikuwa mfungaji bora katika ligi ya Ubelgiji msimu uliopita akifunga magoli 25 na kuisaidia Genk kushinda taji lao la nne la ligi katika historia yao. Samatta pia alitawazwa kuwa mshindi wa taji la Ebony Shoe mwaka uliopita ambalo hutolewa kwa mchezahi bora wa Afrika nchini Ubelgiji. Mchezaji huyo wa kimataifa awali alihusishwa na uhamisho wa klabu kadhaa za Uingereza ikiwemo Leicester, Aston Vill na Watford. Msimu uliopita kulikuwa na tetesi kwamba nyota hyo alikuwa akinyatiwa na klabu kama vile West Ham, Everton na Burnley. Kuvuma akiwa TP Mazembe Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mka