Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2020

Uchaguzi Tanzania 2020: Je, namna gani wapiga kura wanaweza kuepuka migogoro wakati wa kampeni?

Picha
  Matukio ya vurugu za kisiasa miongoni mwa wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais,ubunge na udiwani unaoendelea nchini Tanzania yameathiri mahusiano moja kwa moja kutokana na itikadi tofauti za vyama vya siasa licha ya Katiba ya nchi hiyo kusisitiza uhuru wa kila mwananchi katika kuchagua itikadi hizo pamwe na kudumisha misingi ya demokrasia na siasa za vyama vya vingi. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na matamko ya vitisho dhidi ya wafuasi na wanasiasa wa pande mbili tofauti, kujinyonga, kupigana kwa kutumia mapanga na silaha zingine za jadi hali ambayo inachochea uvunjaji wa sheria pamoja na kuibua taharuki miongoni mwa familia, ndugu, marafiki na taifa kwa ujumla. Duru za kisiasa zimetafsiri hali hiyo ni kiwango duni cha uvumilivu wa kisiasa miongoni mwa wapigakura, na kusababisha baadhi ya wapiga kura kuchukua uamuzi wa kukatisha uhai wao kwa sababu ya kutokukubaliana na wengine ndani ya familia, pamoja na viongozi kushindwa kuwa na lugha za ushawishi wafuasi wao

Carlo Acutis, atununikiwa utakatifu wa digitali

Picha
Kanisa Katoliki limepata baraka mpya Oktoba 10, kwa namna ya kipekee mno : Mshawishi ambaye mwili wake umeoneshwa kwenye laba,jeans na sweta. Leo hii Carlo Acutis anatangazwa kuwa mtakatifu katika mji wa Assisi, jimbo la Perugia, Italia. Acutis alifariki akiwa na umri wa miaka 15 kutokana na kansa ya damu mnamo Oktoba 12, 2006. Kijana huyo mdogo alijulikana sana katika jumuiya wa wakristo kutokana na kazi aliyoifanya katika kanisa kwa kutumia teknolojia mpya , kwa mujbu wa taarifa kutoka Vatican. Acutis alizaliwa mjini London mwaka 1991, ambako wazazi wake walihamia kwa ajili ya kazi lakini alikulia Milan. Acutis anatunukiwa utakatifu mapema sana tofauti na watakatifu wengine waliopita, ni baada ya miaka 14 tu tangu kifo cha kijana huyo. Acutis ni mwenye heri wa kwanza wa "millenia hii " aliyetumia mtandao kutumika katika kanisa, aliyeonesha mfano wa teknolojia inavyoweza kutumika vizuri sana katika kanisa. Hivi ndivyo Papa Pope Francis mwenyewe alivyomuelezea , kwa kusema ku

Ubalozi wa Marekani: Hatutasita kuwachukulia hatua watakaovuruga au kukwaza demokrasia Tanzania

Picha
Ubalozi wa Marekani umesema kwamba haumuungi mkono mgombea yeyote au chama chochote katika uchaguzi ujao wa Tanzania. ''Tunaunga mkono mchakato wa kweli wa uchaguzi huru, wa haki na wenye uwazi, kabla, wakati na baada ya siku ya uchaguzi. Hii ni pamoja na usalama wa wagombea wote, kuheshimiwa kwa utawala wa kisheria na hali ya mamlaka na vyombo vilivyopewa wajibu wa kusimamia na kuendesha uchaguzi kutokupendelea kabisa upande wowote'', ulisema ubalozi huo. Kupitia taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya ubalozi wa taifa hilo nchini Tanzania, ubalozi huo hatahivyo umesema kwamba utafuatilia kwa karibu matendo ya watu wanaoingilia na kuvuruga mchakato wa kidemokrasia au kuchochea vurugu dhidi ya raia. Aidha ubalozi huo umesema kwamba unaunga mkono wito uliotolewa na wagombea wakuu wa kuwepo kwa mchakato wa uchaguzi wa amani na wenye uwazi. ''Tunatoa wito kwao na kwa wafuasi wao kuchukua hatua kutanzua hali ya usalama inayojengeka na kuepuka ma

Wakenya sasa ruksa kushiriki mazishi ya waliokufa na corona

Picha
Kuanzia sasa raia wa Kenya wataweza kushiriki shughuli za mazishi ya wapendwa wao waliofariki kutokana na virusi vya corona baada ya serikali kulegeza masharti tofauti na awali ambapo walipiga marufuku. Awali ndugu wa karibu wa mtu aliyekufa kwa corona hakuruhusiwa kufanya chochote zaidi ya kuangalia kwa mbali wakati maafisa wa afya waliojihami kwa mavazi maalum wakifanya shughuli za mazishi. Maafisa wa afya wamesema kuwa miili ya marehemu waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona haiwezi kuambukiza virusi hivyo. Shirika la afya duniani (WHO) na kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika CDC hawajasema bado kama maiti haiweza kuambukiza Covid-19, lakini wamebadilisha utaratibu na kuruhusu familia kuaga wapendwa wao. Nchini Kenya', maofisa wa afya watakuepo katika mazishi ili kutoa muongozo na kuhakikisha usalama unazingatiwa. "Tutaruhusu shughuli zote za mazishi za kidini na kitamaduni kufuatwa kulingana na tamaduni za marehemu," Serikali imekiri kuwa

Jaji wa Mahakama ya Juu Marekani Ruth Ginsburg afariki

Picha
Jaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani Ruth Bader Ginsburg, mpiganiaji wa haki za wanawake ambaye alikuwa jaji wa pili mwanamake katika mahakama hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 Kifo chake ambacho kimetokea wiki sita tu kabla ya Uchaguzi wa Rais huenda kikaanzisha mapambano makali ya kisiasa kuhusu kama Rais Donald Trump anapaswa kumteuwa, na baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublican liidhinishe, mrithi wake, au kama kiti hicho kibaki wazi hadi baada ya kujulikana matokeo ya kinyang'anyiro chake dhidi ya Mdemocrat Joe Biden. Ginsburg ni Mliberali alijetambulika kwa kutetea haki za wanawake na jamii za walio wachache. Kiongozi wa Maseneta wa Republican Mitch McConnell amesema Seneti itapiga kura ya kuidhinisha au kupinga jaji atakayependekezwa na Trump kumrithi Ginsburg, hata ingawa ni mwaka wa uchaguzi.  Trump amemuita Ginsburg "mwanamke wa ajabu" na hakutaja kuhusu kujaza kiti chake kilichobaki wazi katika Mahakama ya Juu wakati akizungumz

Mazungumzo ya amani: Mjumbe wa Marekani hafurahii mpango wa kuwaachia wafungwa wa Taliban

Picha
Mjumbe wa Marekani katika mkutano wa kutafuta amani nchini Afghanstan ameiambia Newsday Swahili kuwa "hafurahii" makubalino yenye utata ya kuwaachia huru wafungwa 5,000 wa Talban ili kufanikisha mazungumzo ya amani ya kihistoria. Hatahivyo mwakilishi huyo Lyse Doucet, Zalmay Khalilzad aliongeza kuwa "Inabidi kufanya maamuzi magumu". Alipoulizwa kuhusu waliokuwa wafungwa kurejea katika mapigano, bwana Khalilzad alisema "hawana ushahidi wowote". Mazungumzo ya Amani kati ya viongozi wa Afghan na Talban yalianza mjini Qatar siku ya Jumamosi. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Afghanistan kuwa na mazungumzo ya amani na kundi la wanamgambo wa kiislamu. Lengo likiwa ni kusitisha mapigano ya miaka 19. Kuachiwa huru kwa wafungwa 5,000 lilikuwa sharti walilokubaliana Marekani na Taliban baada ya mazungumzo ya amani ya mwaka jana na kuanza mazungumzo haya. Serikali ya Afghanistan haikuhusishwa katika kuweka makubaliano hayo

Uchaguzi Tanzania 2020: Dini zina mchango gani katika siasa za Tanzania?

Picha
Katika hotuba yake ya kuaga Watanzania wakati akistaafu maisha ya kisiasa takribani miongo minne iliyopita, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisimulia kisa kinachoeleza uhusiano baina ya dini na siasa za Tanzania. Alisimulia kisa kilichotokea wakati Tanganyika (ambayo Muungano wake na Zanzibar ndiyo umeunda Tanzania), ikipigania Uhuru wake dhidi ya wakoloni Waingereza. Mwalimu Nyerere, alikuwa amechukuliwa na wazee wa chama cha TANU ambao wengi wao walikuwa waumini wa dini ya Kiislamu. Wakampeleka Bagamoyo, Pwani kwa ajili ya kufanya ibada maalumu ya kumwondoa mkoloni. Kukatisha hadithi hiyo, Nyerere alieleza namna yeye (Mkristo), alivyokubalika na kupokewa na Waislamu wa Dar es Salaam kiasi cha kukabidhiwa madaraka ya juu zaidi hapa nchini. Mkasa huu wa Baba wa Taifa la Tanzania unaeleza pia kuhusu ukweli mwingine kuhusu taifa hili; kwamba ingawa kuna dini mbili kubwa, kuna dini ya tatu ambayo huwa haisemwi sana lakini ina nguvu sana - dini ya nyumbani.