Ukigundua una dalili hizi 10 nenda ukapimwe maradhi ya Kisukari


Madaktari wanasema kwamba inawezekana kuishi maisha yenye afya kwa muda mrefu ikiwa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Afroza Akhtar hakuelewa kwamba alikuwa na kisukari kwa muda mrefu. Hakujua kwamba sababu za kujihisi kiu, uchovu na mwili kuishiwa nguvu huenda ni baadhi ya dalili za maradhi hayo.

''Nilikwenda kwa daktari na kumueleza baada ya kujisikia vibaya kwa muda mrefu.Alinifanyia vipimo vya kisukari na magonjwa mengine. Ni pale ndipo niligundulika kuwa nina ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu ''

Tangu hapo alianza matibabu katika hospitali maalum ya ugonjwa wa kisukari.

Si yeye pekee, kwa mujibu wa wataalamu wa kisukari, zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye maradhi ya kisukari hawafahamu kuwa wana ugonjwa huo

Ugonjwa huo uligunduliwa wakati wa alipokuwa akipimwa maradhi mengine.

Unaweza pia kusoma

Wataalamu wanasema kutokana na hali hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kutoa hamasa kwa jamii kuhusu ugonjwa wa kisukari.

Utafiti mmoja wa Taasisi ya Mafunzo ya Idadi ya Watu (NIPORT) unaonyesha kuwa katika jumla ya wagonjwa wa kisukari milioni 10. Miongoni mwao ni wenye umri wa miaka 18 hadi 34 ambao ni laki 2.6 na idadi ya watu zaidi ya miaka 35 ni laki 8.4.

Wataalamu wanasema kwamba ikiwa ugonjwa wa kisukari haujatambuliwa au haujatibiwa kwa muda mrefu, figo, ini na macho huharibika.

Pamoja na hayo, ngozi ya mwili huharibika, nywele hudondoka. Sehemu zingine za mwili pia zinaweza kuathirika.

"Wale wanaofanya shughuli nyingi, kama vile kutembea angalau hatua 10,000 kila siku, hata kama ana kisukari, inawezekana kudhibiti. Lakini ni wangapi wanaofanya hivyo?''

Inashauriwa na wataalamu kwamba yeyote aliye na kisukari lazima afanye mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Epuka sukari

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wataalamu wanasema kwamba asilimia 75 ya ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2 inaweza kuzuiwa ikiwa utakuwa mwangalifu mapema, kufanya mazoezi, na kudhibiti lishe na mtindo wako wa maisha.

Lakini mara tu unapogundulika kuwa na kisukari hakuna namna ya kuondoa ugonjwa huu.

Chukua hatua ukiona dalili hizi:

  • Kukojoa mara kwa mara na kiu
  • Kuhisi udhaifu na kizunguzungu
  • kuongezeka kwa hamu ya kula
  • Ikiwa hutakula na kunywa kwa wakati, sukari ya kwenye damu hupungua
  • Kuongezeka kwa hamu ya pipi
  • Kupoteza uzito mwingi bila sababu
  • Hata ikiwa kuna jeraha au kukatwa kwenye mwili, huchukua muda mrefu kupona
  • Ngozi kavu, inayowaka na kuwasha
  • Kuwashwa
  • Macho kuanza kupoteza uoni
Kuna aina tano za kisukari, sio mbili - wanaeleza watafiti

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ni nani aliye katika hatari kubwa zaidi?

Wataalamu wanasema kwamba wale ambao wazazi wao, ndugu au jamaa wa karibu wana kisukari wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Mbali na hilo, wale ambao hawana utamaduni wa kutembea mara kwa mara au kufanya mazoezi ya mwili, au wasio na mtindo ufaao wa Maisha wana hatari ya kuathiriwa na ugonjwa huu.

Kwa kuongezea, wanawake wanaweza kupata ugonjwa wa sukari wakati wa ujauzito.

Watu wenye magonjwa ya moyo, cholesterol kubwa ya damu, shinikizo la damu pia wako katika hatari ya kupata ugonjwa huu.

Watoto walio na uzito mkubwa, wazazi, ndugu, babu au jamaa wa karibu wenye ugonjwa wa kisukari, ambao mama yao alikuwa na kisukari wakati wa ujauzito, wako katika hatari ya kupata kisukari.

Kisukari ni tatizo kubwa la kiafya duniani kote

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hatua za kuzingatia

Wale ambao wako katika hatari, lazima wapimwe ugonjwa wa kisukari mara moja kwa mwaka.

Sio lazima kila wakati kwenda hospitalini.

Vipimo vya haraka vya kisukari sasa vinapatikana katika maduka mengi ya dawa kwa gharama nafuu.

Ikiwa utagundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari, ni lazima kupata ushauri wa daktari.

Watoto ambao jamaa zao wa karibu wana historia ya ugonjwa wa kisukari wanapaswa pia kuchunguzwa angalau mara moja kwa mwaka.

Kisukari kinapogunduliwa mapema, ndivyo inavyokuwa vema mgonjwa,Kwa kuwa ataweza kuanza matibabu ya ugonjwa huo haraka, mtindo wake wa maisha pia utadhibitiwa.Wanaeleza wataalamu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga

Yanga wamlilia Manji