Kutoka Vietnam hadi Iran: Nani na kwa namna gani Korea Kaskazini ilisaidia Kupambana


h

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Bunge la Urusi lililofahamika kama State Duma limeidhinisha mkataba wa "ushirikiano wa kimkakati wa kina" na Korea Kaskazini.

Hati hii ina kifungu cha kutoa usaidizi wa kijeshi wa pande zote katika shambulio la moja ya nchi, ambapo Wall Street Journal iliandika kwamba mkataba huo pia una kifungu cha siri juu ya kutumwa wanajeshi wa Korea Kaskazini Kwenda vitani na Ukraine.

Siku ya Jumatano, Oktoba 23, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema Pentagon ina ushahidi wa wanajeshi wa Korea Kaskazini kutumwa Urusi.

Taarifa za kijasusi za Korea Kusini imeripoti kwamba DPRK imeipatia Moscow askari elfu tatu, na kufanya jumla ya askari 10,000.

Hapo awali, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alizungumza juu ya brigedi mbili za askari 6,000 kila moja.

Ikiwa data hizi zitathibitishwa, ya kwamba DPRK kweli ilituma maelfu ya askari wake kusaidia jeshi la Urusi, basi kampeni hii itakuwa kesi ya kwanza ya ushiriki mkubwa wa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita nje ya Korea.

Hata hivyo, wanajeshi wa Korea Kaskazini wamesaidia nchi marafiki katika vita vyao hapo awali, ingawa sio kwa idadi kama hiyo.

Wameshiriki katika migogoro duniani kote, kuanzia Asia ya Kusini-Mashariki hadi Mashariki ya Kati na Afrika.

Makala haya ya BBC yanaeleza jinsi jeshi la DPRK lilivyopata uzoefu wa mapambano katika vita vya watu wengine.

Unaweza pia kusoma:

Vita vya Vietnam

Mara ya kwanza Korea Kaskazini iliingilia moja kwa moja vita nje ya mipaka yake ilikuwa miaka ya 1960.

Vita vya Vietnam vilikuwa sawa kwa namna nyingi na Vita vya Korea: Kaskazini ya kikomunisti dhidi ya Kusini inayounga mkono na Marekani.

Korea Kaskazini ilishinda vita vyake na ilikuwa tayari kusaidia Vietnam kupambana na Wamarekani.

Mnamo Oktoba 1966, Chama tawala cha Wafanyakazi wa Korea kiliamua kutoa msaada wa kijeshi kwa Vietnam. Mapema mwaka wa 1967, DPRK ilianza kusambaza silaha kwa Hanoi, risasi, na hadi sare milioni 2 kwa Vietnam.

Kwa kuongeza ili kulinda Hanoi, Vietnam ilipokea wapiganaji kutoka Korea Kaskazini, ambayo iliimarisha jeshi la anga la 921 na 923.

Wakati huo, ilijulikana tu kwamba wapiganaji walipatikana kwa "hali fulani."

Na katika mwaka wa 1996 pekee Pentagon ilithibitisha kwa hakika kwamba wapiganaji walitolewa na Pyongyang, na Vietnam yenyewe ilikubali rasmi hili hata baadaye, mwaka wa 2001.

Aidha, wakati wa vita, hadi marubani 200 wa Korea Kaskazini walipigana upande wa wakomunisti wa Kivietnamu.

g

CHANZO CHA PICHA,AFP KUPITIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Marubani 12 wa Korea Kaskazini waliouawa wakati wa vita walizikwa katika jimbo la Vietnam la Bac Giang. Mnamo 2001, mabaki ya miili yao yalisafirishwa hadi DPRK, lakini iliamuliwa yahifadhiwe katika kumbukumbu ya vita huko Vietnam.

Mashariki ya Kati

Mwanzilishi na kiongozi wa muda mrefu wa Korea Kaskazini Kim Il Sung aliita Israel "satelaiti ya kifalme" na kuwaunga mkono maadui wa taifa hilo la Kiyahudi tangu miaka ya 1960.

Pyongyang ilishirikiana rasmi na Misri na Syria, na kwa njia isiyo rasmi na Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina na vikundi vingine vyenye itikadi kali, ikiendesha kambi za mafunzo kwa wapiganaji.

Lakini jeshi la Korea Kaskazini lilishiriki moja kwa moja katika mzozo wa Waarabu na Israeli mnamo 1973 tu.

Mnamo Julai 18, 1972, Rais wa Misri Anwar Sadat aliamuru kuondolewa kwa wanajeshi wote wa Soviet kutoka nchi hiyo na kuhamishiwa kwa kambi.

Wakati huo, Umoja wa Kisovieti ulikuwa ukifuata sera ya "détente" na kuepuka kwa makini migogoro ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na Marekani.

Sadat hakufurahishwa na vikwazo vya matumizi ya silaha ambavyo Moscow ilisisitiza.

Matokeo yake, Misri iliachwa bila washauri wa kijeshi, marubani, na mafundi kutoka USSR, licha ya ukweli kwamba jeshi la anga la nchi hiyo lilikuwa na MiG-21 ya Soviet.

g

CHANZO CHA PICHA,UNIVERSAL IMAGES GROUP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Anwar Sadat katika nyadhifa za jeshi la Misri karibu na Mfereji wa Suez mnamo Oktoba 1973

Vita vya Iran na Iraq

Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Kim Il Sung alitaka kuboresha uhusiano na uongozi mpya wa jamhuri hiyo. Marekani iliiwekea vikwazo Iran na, baada ya majeshi ya Iraq kuivamia nchi hiyo mwaka 1980, iliimarisha zaidi vikwazo vya silaha.

Pyongyang ilianza kuipatia Iran silaha kinyume na vikwazo,pamoja na kurusha makombora, wanajeshi wa Korea Kaskazini, takriban 100, waliwasili katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Ushirikiano mkubwa wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili uliendelea baada ya kumalizika kwa mzozo wa Iran na Iraq, hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, wakati mzozo wa kiuchumi ulipozuka DPRK.

Africa

Katika kilele cha Vita Baridi, Korea Kaskazini ilikuwa na rasilimali za kujihusisha na siasa za Kiafrika.

Washauri wa kijeshi wa Korea Kaskazini walisaidia Polisario Front, kikosi cha kudai uhuru katika Eneo la Sahara Magharibi, na kutoa mafunzo kwa waasi nchini Angola na Namibia.

Katika miaka ya 1970, Pyongyang ilianzisha uhusiano na madikteta wawili mashuhuri wa Kiafrika: Francisco Nguema wa Guinea ya Ikweta na kiongozi wa Uganda Idi Amin.

Nguema hakuficha jinsi alivyovutiwa na Kim Jong-il, wakufunzi wa Korea Kaskazini walikuwa sehemu ya maelezo yake ya usalama, na Equatorial Guinea ilikuwa njia ya kupitishia silaha za Korea kwa waasi kusini magharibi mwa Afrika.

Baada ya dikteta kupinduliwa, familia yake ilikimbilia DPRK.

g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Naibu Waziri wa Usalama wa Umma wa Korea Kaskazini, Lee Song Chol, akitembelea chuo cha polisi mjini Kampala, Uganda, 2013. Tangu 1988, wataalamu wa Korea Kaskazini wamesaidia kutoa mafunzo kwa maafisa wa kutekeleza sheria huko

Katika kilele cha Vita Baridi, Korea Kaskazini ilikuwa na rasilimali za kujihusisha na siasa za Kiafrika.

Washauri wa kijeshi wa Korea Kaskazini walisaidia Polisario Front, kikosi cha kudai uhuru katika Eneo la Sahara Magharibi, na kutoa mafunzo kwa waasi nchini Angola na Namibia.

Katika miaka ya 1970, Pyongyang ilianzisha uhusiano na madikteta wawili mashuhuri wa Kiafrika: Francisco Nguema wa Guinea ya Ikweta na kiongozi wa Uganda Idi Amin.

Nguema hakuficha jinsi alivyovutiwa na Kim Jong-il, wakufunzi wa Korea Kaskazini walikuwa sehemu ya maelezo yake ya usalama, na Equatorial Guinea ilikuwa njia ya kupitishia silaha za Korea kwa waasi kusini magharibi mwa Afrika.

Baada ya dikteta kupinduliwa, familia yake ilikimbilia DPRK.

Uhusiano wa karibu wa Korea Kaskazini na Uganda haukuisha baada ya kuanguka kwa utawala wa Idi Amin.

Kiwanda cha kijeshi kilijengwa katika nchi hiyo ya Kiafrika kwa msaada wa DPRK.

Ushirikiano huo uliendelea kwa miongo kadhaa, licha ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya DPRK. Kwa mfano, mwaka 2007, Uganda na Korea Kaskazini zilitia saini makubaliano ya mafunzo ya marubani na mafundi kwa jeshi la Uganda.

Mnamo mwaka wa 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio nambari 2770, ambalo lilipiga marufuku kwa uwazi matumizi ya "wakufunzi, washauri au maafisa wengine kutoka DPRK katika kutoa mafunzo kwa polisi au vikosi vya kijeshi."

Lakini ilipita miaka miwili kabla ya Uganda kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa, kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Pyongyang na kuwanyima visa wakufunzi 14 wa marubani kutoka Korea Kaskazini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga