Israel ina mpango wa kutaka kuitwaa Gaza kaskazini


xx

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Magazeti kadhaa ya Kiarabu, Uingereza na Marekani yaliangazia matokeo ya kurejea kwa Donald Trump katika kiti cha urais nchini Marekani kwa eneo la Mashariki ya Kati.

Katika muktadha huu, Makala haya yanaangazia kuhusu hofu ya Israel kunyakua ardhi ya Palestina, na kwa upande mwingine kuhusu safu ya viongozi wapya wa Trump.

Pia utafahamu kuhusu mwelekeo wa uhusiano kati ya Trump na Iran katika siku za usoni.

Tunaanza na gazeti la Uingereza The Guardian na makala iliyoandikwa na Ben Reeve, ambapo aliangazia matamshi, harakati za kijeshi, na hatua za kisiasa ambazo zinaonyesha kuwa Israeli inapambana kunyakua Ukanda wa kaskazini mwa Gaza.

Mwandishi wa gazeti la Uingereza alirejelea matamshi ya Itzik Cohen, afisa mkuu wa jeshi la Israel, aliyoyaona kama "ukiri" kwamba Israel inatekeleza "maangamizi kwa jamii hiyo ya kaskazini mwa Gaza, na kuuhadaa ulimwengu kuhusu malengo yake halisi katika eneo ililodhibiti.

Makala hiyo ilieleza kwamba Cohen "alijigamba" kwamba vikosi vya Israel vilikuwa karibu "kuhamisha" maeneo ya Jabalia, Beit Hanoun na Beit Lahia, kaskazini mwa Gaza, ambayo yamekuwa yakikabiliwa na mashambulizi makali ya Israel tangu mapema Oktoba.

Mwandishi ananukuu kauli ya Cohen mbele ya vyombo vya habari kwamba ''hakuna nia ya kuwaruhusu wakazi wa Gaza kaskazini kurejea makwao,na kuongeza kwamba kanuni ziko wazi kwamba mpango ulikuwa ni kuwa na eneo hilo baada ya kuwaondoa akimaanisha wapalestina.

Unaweza pia kusoma

Licha ya jeshi kujitenga na kauli ya Cohen mwandishi anaamini kwamba kile kinachotokea Kaskazini mwa Gaza ndicho hasa Cohen anachoeleza.

Mwandishi aliendelea akionesha namna hilo lilivyokubalika kwa kiwango cha juu" na Waziri wa Ulinzi wa Israeli aliyefutwa kazi, Yoav Galant, wakati wa mazungumzo yake na familia za mateka wa Israeli huko Gaza, akisema, "Hakuna chochote ambacho hakijafanyika huko Gaza.

Malengo makuu yameafikiwa. Ninaogopa kwamba tuko pale kwa sababu tu tunataka kubaki huko.

Mwandishi anaeleza kwamba "kuwaondoa wapalestina kaskazini mwa Gaza kutawawezesha "walowezi wa Israel na wapanga mipango wakuu kufanikisha kile walichotamani kitokee kwa kuanzisha upya makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo hilo," akisema kwamba "ukweli unathibitisha kwamba tayari wamepanga mipango."

Dalili nyingine ya mwelekeo huu, Reif aliongeza, ni mwaliko wa hivi karibuni wa mawaziri wawili kutoka siasa kali za mrengo wa kulia Orit Struck na Yitzhak Wasserlauf ili kujiunga na baraza la mawaziri la usalama la Israel,akitoa maoni kwamba hao ndio “watu sahihi wa kutoa ushauri kuhusu makazi katika eneo la Gaza.

Hatimaye, kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House, kunamaaanisha hatari inayokaribia kaskazini mwa Gaza ikimaanisha Udhibiti wa kudumu wa Israel kwa sehemu ya eneo hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi anaona kwamba Israel ikipata uungwaji mkono kutoka kwa Marekani kuhusu hatua ya kulitenganisha eneo la kaskazini mwa Gaza iwe kwa muktadha wa mpango uliorekebishwa mnamo Karne hii au kwa mkataba mdogo kwamba Netanyahu anapata anachotaka kwa kukomesha vitendo vya kikatili kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Trump

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Uongozi mpya tiifu kwa Trump

Kwa upande wa gazeti la Marekani Washington Post na Makala inayogusia wazo la ‘’Utii’’ kitakuwa kigezo cha msingi kwa rais mteule Donald Trump atakitumia katika kuunda safu ya uongozi wake ujao,kwa kuhakikisha wale wanaomzunguka hawatakwenda kinyume nae kama ilivyotokea awali.

Mwandishi Karen Tumulty amekiita kiwango hiki "Jaribio la Januari 7," akimaanisha matokeo ya vurugu za 2021 huko Capitol na wafuasi wa Trump wakipinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani, ambayo Joe Biden alitangazwa kuwa mshindi.

Tumulty anasema kwamba uteuzi wa baadhi ya viongozi katika utawala mpya wa Trump kunakuja licha ya ukosoaji wa vurugu zilizotokea Capitol,kwa sababu ya kupuuzwa kwa jukumu la Trump katika kuchochea wafuasi wake kufanya vitendo vya umwagaji damu.‘

’Ikiwa wanaweza kuvumilia kile Trump alichofanya siku ile,ni sawa kuamini kwamba hawatamzuia katika desturi za demokrasia ambazo rais huyo anayerejea ataamuru’’anaeleza mwandishi huyo.

Ingawa idadi ya watu ambao Trump atawateua kushika nyadhifa za juu bado haijawekwa wazi, mwandishi huyo anaamini kwamba rais wa Marekani anayerejea atawataka "kutii," hasa katika vyombo vya sheria, sera za kigeni na usalama wa taifa, baada ya kuangushwa na aliowateua awali katika muhula wake wa kwanza.

Mwandishi huyo alimwelekezea kidole Seneta wa chama cha Republican Marco Rubio, ambaye anaripotiwa kuwa waziri wa Mambo ya Nje, baada ya kuzindua kampeni kali dhidi ya Trump katika kinyang'anyiro cha uteuzi ndani ya chama cha Republican 2016, akimtaja kama "msanii" na asiyefaa kuongoza katika ofisi hiyo,anaeleza mwandishi huyo.

Hata hivyo uteuzi wake kwa nafasi hiyo sambamba na wengine zinakuja ndani ya mkakati ambao mwandishi anauita ''huruma'' ya Trump hasa kwa nafasi ya Rubio katika vurugu za Capitol mwaka mmoja baadaye aliposema ghasia ndio neno sahihi linalofaa kuelezea tukio hilo ambalo halikulenga kupindua serikali.

Mwandishi alitoa mfano mwingine: Mwakilishi Lee Zeldin, ambaye Trump alimchagua kuongoza Shirika la Uhifadhi wa Mazingira, baada ya kusema kuhusu matukio ya Capitol kwamba wahusika halisi wa vurugu walikuwa "watendaji wa serikali."

Mwakilishi Elise Stefanik, ambaye rais mteule anapanga kumteua kuwa mwakilishi wa Washington katika Umoja wa Mataifa, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na mashaka ambao baadaye walibadili mawazo yao kuhusu Trump, na kuanza kuwaita wale waliofungwa kwa kuhusika na vurugu za Capitol "mateka."

Mwakilishi Mike Waltz, ambaye anatazamiwa kuwa mshauri wa usalama wa taifa, pia alisema hatua ya Democrats kulinganisha shambulio la Capitol na 9/11 au Pearl Harbor ilikuwa "ujinga".

Mwandishi huyo wa gazeti la Marekani anathibitisha kwamba wale waliosimama dhidi ya Trump wakati wa muhula wake wa kwanza waliondolewa madarakani, kama ilivyotokea kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wakati huo Mark Esper, ambaye "alikejeli wazo la kurusha makombora ya Patriot nchini Mexico ili kumaliza magenge ya wafanyabishara wa dawa za kulevya na kuishutumu nchi nyingine kwa kufanya hivyo."

Esper alikuwa mmoja wa mawaziri watano wa ulinzi ambao walihudumu wakati wa muhula wa kwanza wa Trump, na msimamo wake ulisababisha kufutwa kwake.

Lakini angalau alikuwa na nafuu kuliko aliyekuwa mnadhimu mkuu wa serikali Generali Mark Milley, ambaye Trump alisema anapaswa kuhukumiwa kwa uhaini, "kosa ambalo adhabu yake ni kifo," kwa mujibu wa mwandishi.

Iran na Trump…Mazungumzo au Uhasama zaidi?

Tunahitimisha kwa kuangazia makala ya mwandishi wa Saudi Tariq Al-Hamid wa gazeti la Asharq Al-Awsat, kuhusu mustakabali wa uhusiano wa Tehran na Washington katika muhula wa pili wa rais mteule Donald Trump.

Al-Hamid amebainisha katika makala yake kwamba Netanyahu alitangaza kwamba amewasiliana na rais mteule mara tatu tangu Novemba 5, na kuongeza katika taarifa yake: “Tunaona kwa macho yetu tishio la Iran katika vipengele vyote, na hatari iliyopo,” akizungumza kuhusu yeye na Trump.

Mwandishi huyo anaamini kwamba wanasiasa wa Iran walio karibu na Washington au walio karibu zaidi na Kiongozi Mkuu wa Iran wote wanaona kuwa "kurejea kwa Trump katika kiti cha urais ni fursa ya mazungumzo."

Mwandishi huyo wa Saudia alitumia kile ambacho gazeti la Marekani, The New York Times, lilinukuu kutoka gazeti la wanamageuzi la Iran, Shargh, lililochapisha tahariri kwenye ukurasa wa mbele: “Rais mpya wa Iran mwenye msimamo wa wastani, Masoud Pezeshkian, lazima aepuke makosa ya zamani na kupitisha sera ya vitendo, yenye nyanja nyingi.

Al-Hamid pia alikuwa na maoni tofauti katika Jarida la Wall Street wiki iliyopita kwamba utawala mpya wa Trump utatoa shinikizo kubwa kwa Tehran tangu siku yake ya kwanza kuingia Ikulu ya White House.

Tariq Al-Hamid alirejelea mazungumzo kati yake na afisa mmoja wa Kiarabu miezi michache iliyopita, alipomwambia, "Ikiwa Trump atashinda, usizuie chochote, na kumbuka kwamba yeyote aliyeelewana na Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini, anaweza kuelewana na kiongozi wa Iran.

Mwandishi huyo anatoa maoni kwamba Trump ana uwezo wa kufanya mazungumzo na Iran, hasa kwa vile anajigamba kwamba anaweza kufikia makubaliano na upande wowote, lakini alishangaa kuhusu uwezo wa Iran kufanya hivyo, hasa kwa vile hilo linamaanisha "mabadiliko kamili na ya gharama kubwa ya kiutawala.

Aidha mwandishi wa Saudi alihitimisha makala yake kwa kusema kwamba chaguzi zote ni ngumu kwa Iran, iwe inaamua kubadilika au kukabiliana, hususan na kutoeleweka kwa Netanyahu.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga

Yanga wamlilia Manji