Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, Marekani itaendelea kuiunga mkono au kuitelekeza Ukraine baada ya uchaguzi?


sdxc
  • Author,

Rais ajaye wa Marekani ataamua kuhusu matarajio ya Ukraine kuingia NATO, kuendelea na usambazaji wa silaha za Magharibi na masharti ya mazungumzo ya amani kati ya Kyiv na Moscow.

Wafuatiliaji wa mambo wanakubali kwamba ushindi wa Kamala Harris utapokelewa vizuri zaidi huko Kyiv kuliko muhula wa pili wa Donald Trump.

Diplomasia ilikuwa sehemu ya jukumu la Harris kama makamu wa rais katika utawala wa Biden, alipewa kazi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali.

Pia unaweza kusoma

Mipango ya Harris

szx

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Mwaka 2022, Congress ilimkaribisha Zelensky kwa shangwe

Mwaka 2022, Urusi ilifanya uvamizi nchini Ukraine, na diplomasia ya Harris iliongeza msaada kwa Kyiv. Amekutana na Rais Volodymyr Zelensky mara saba, katika mazungumzo na wanachama wa NATO na kuiwakilisha Marekani katika Mkutano wa Usalama wa Munich.

Harris anasema iwapo atashinda, ataendelea na sera za Biden - kuunga mkono Ukraine kwa msaada wa kijeshi, kukataa kufanya mazungumzo na Kremlin bila ushiriki wa Kyiv na kuheshimu haki ya Zelensky ya kuamua masharti ambayo nchi yake iko tayari ili kusitisha mapigano.

Huko Marekani na Ulaya, “uchovu wa vita umeenea, na hata wanaunga mkono Ukraine wanakiri kwamba uwezo wa Magharibi wa kuunga mkono Kiev katika vita unaanza kukauka,” anaandika mwandishi wa gazeti la Washington Post, Ishaan Tharoor.

"Ukraine inahisi kuwa inapata silaha za kutosha ili kutopoteza vita, lakini sio za kutosha kushinda. Sera hizo huenda zikaendelea hivyo chini ya Harris,” anaandika mwandishi kutoka Taasisi ya Brookings, taasisi ya fikra huria ya huko Washington.

Mpango wa Zelensky, ni nchi hiyo kujiunga NATO, lakini Harris bado hajazungumza wazi juu ya suala hili. Katika mahojiano na CBS, alisema atashughulikia suala hilo "wakati ukifika."

Mipango ya Trump

Wapinzani wa Donald Trump wanaelezea sera yake ya kigeni kuwa isiyo tabirika, na anaegemea kwa viongozi wa kimabavu kama Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban hadi Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Kwa miaka minne katika Ikulu ya White House, mara kwa mara alipinga Marekani kushiriki migogoro ya kijeshi. Kwa mfano, licha ya msimamo wake wa kuunga mkono Israel bila masharti, rais huyo alizungumzia kuhusu haja ya kumaliza vita huko Gaza.

"Kiuhalisia hapendi vita," anasema Peter Baker, mwandishi wa White House wa gazeti la New York Times.

Trump pia anaamini ni muhimu kusitisha vita nchini Ukraine haraka iwezekanavyo. Aliahidi kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano ndani ya saa 24 iwapo atachaguliwa kuwa rais, akaweka bayana kuwa atalifanikisha hilo kabla ya kuapishwa kwake Januari 2025.

Shida ni kwamba Trump hasemi jinsi anavyopanga kufanikisha mambo yake.

"Nina mpango wa wazi wa jinsi ya kumaliza vita vya Ukraine na Urus…," Trump alisema mwezi Septemba. "Lakini siwezi kufichua mipango hii, kwa sababu ikiwa nitafichua, sitaweza kuitekeleza."

Katika hali ya kutokuwa na uhakika, wafuasi na wapinzani wanatafsiri mipango ya Trump kwa njia zao wenyewe.

Trump na Putin

dsx

CHANZO CHA PICHA,KREMLIN POOL

Maelezo ya picha,Trump anasema ana uhusiano mzuri na Putin

Mgombea mwenza wa Trump, J.D. Vance ni mmoja wa wakosoaji wakuu wa misaada ya kijeshi kwa Ukraine. Anataka kuuzima mgogoro huo kwa kusimamisha usambazaji wa silaha. Analiita lengo la Zelensky la kutaka kuirejesha Ukraine ndani ya mipaka ya 1991 kuwa la ajabu.

Maoni sawa na hayo yametolewa hadharani na wafuasi wengine wa Trump ambao maoni yao kwa kawaida hujulikana kama ya kujitenga na mgogoro huo.

Mike Pompeo, mkurugenzi wa zamani wa CIA na waziri wa mambo ya nje katika utawala wa Trump, katika makala yake "Mpango wa Amani wa Trump kwa Ukraine," anaahidi vikwazo vikali dhidi ya Moscow na Ukraine kuingia NATO ikiwa mgombea wa Republican atashinda uchaguzi.

Ni kundi gani kati ya haya mawili, ambalo Trump atalisikiliza iwapo atashinda? Hilo halijulikani.

Trump anasisitiza kuwa atafanya mazungumzo na Putin na Zelensky. Hilo ni kinyume na sera ya utawala wa Joe Biden, ambayo inazingatia haki ya Kyiv ya kuamua masharti ya makubaliano ya baadaye.

Mwaka 2019, Zelensky alikataa kuanzisha uchunguzi dhidi ya Biden kwa ombi la Trump. Tukio hili liliunda msingi wa kushtakiwa kwa Trump na baraza la Congress, ambalo lilidhibitiwa na Democrats.

Mashaka ya Trump dhidi ya NATO yanaweza pia kuzuia msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Rais huyo wa zamani anaamini wanachama wa muungano huo wanategemea ulinzi wa Marekani.

Haiwezekani kutabiri jinsi uhusiano wa White House na Kremlin utakavyokuwa ikiwa Trump atachaguliwa kwa muhula wa pili. Democrats wanaamini kiongozi huyo wa Republican anamuhusudu Putin – jasusi wa zamani wa FSB. Na Trump mwenyewe anadai ana uhusiano mzuri na Putin.

Trump na Urusi

Hadithi ya kweli hasa ya uhusiano kati ya utawala wa Trump na Kremlin ni ngumu sana. Kwani wakati wa utawala wake, vikwazo vipya vilianzishwa, wanadiplomasia 60 wa Kirusi walifukuzwa kutoka Marekani.

Haya yote yamemfanya Putin akumbuke bila kutamani: "Kuhusu Trump, wakati wa urais wake idadi kubwa ya vikwazo na vigingi viliwekwa dhidi ya Urusi."

Kwa upande mwingine, ilikuwa Trump mwaka 2017 aliyeondoa marufuku ya usambazaji wa mifumo ya kupambana na vifaru ya Marekani kwa Ukraine.

Na nje ya Ukraine, utawala wa Trump ulikuwa na uhusiano mbovu na nchi nyingine: Vikwazo dhidi ya Venezuela na Cuba, kujiondoa katika mapatano ya nyuklia na Iran, mauaji ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani, kuhamishwa ubalozi wa Marekani hadi Jerusalem na kutambua mamlaka ya Israel juu ya Miinuko ya Golan ni hatua ambazo Moscow ilizikosoa.

Haya yote yanamfanya Mick Ryan, mtaalamu wa masuala ya kijeshi na jenerali mstaafu wa jeshi la Australia, kuamini, ikiwa mazungumzo na Putin yatakwama wakati wa muhula wa pili wa Trump, rais wa Marekani anaweza kuigeuka Urusi na kuongeza uungaji mkono kwa Ukraine

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga