Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sheria ya Gompertz-Makeham, mbinu ya hisabati inayokupatia muda ambao binadamu anaweza kuishi


.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

"Mahitaji ya kwanza ya kutokufa ni kifo," alisema Stanislaw Jerzy Lec.

Asili ina kila kitu, na kwamba kila kitu kinajumuisha tofauti kubwa katika muda wa kuishi wa viumbe vyake.

Ingawa Ephemeroptera, mdudu huyo anayeruka kwa jina mayfly, anaishi kwa saa 24 tu, Turritopsis dohrnii pia anaishi kulingana na jina lake: aina ya samaki asiyeweza kufa.

Wakiwa wadogo, wana ujuzi wa ajabu wa kuishi: hurudi kwenye ujana wao wakati wa mfadhaiko, kama vile wanapojeruhiwa kimwili au hata njaa, na wanaweza kuishi milele.

Wanaonekana kuwa wamegundua siri ya kizushi ya ujana ambayo wanadamu, wakijua kwamba, kama mwanafalsafa Montaigne alivyosema, "kifo kinatupata kila wakati" na hatimaye hutunyonga.

Kwa kweli, hadithi ya zamani zaidi tunayojua, "Epic of Gilgamesh," inahusu hilo.

Ikiwa imechorwa kwenye mabango ya udongo miaka elfu nne iliyopita huko Mesopotamia, inasimulia juu ya safari iliyofanywa na Mfalme Gilgamesh katika kutafuta njia ya kukishinda kifo.

Anachopata ni maana ya maisha:

"Wanadamu huzaliwa, huishi, kisha hufa,

Hii ndiyo amri waliyoiweka miungu.

Lakini hadi mwisho utakapokufa, furahia maisha yako,

Tumia kwa furaha, sio kukata tamaa. "

Ushauri wake, hata hivyo, haukuzingatiwa, na hadi leo kuna wanasayansi katika vituo bora vya utafiti juu ya sayari ambao misheni yao inafanana na ile ya Mfalme Gilgamesh.

Licha ya juhudi zote, kwa sasa, wastani wetu wa kuishi duniani ni miaka 73.4 (2019, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani).

Na ingawa imeongezeka, kuna sheria ya maisha na kifo ambayo imebakia kutumika tangu ilipowekwa karibu karne mbili zilizopita.

Kitu kisichoweza kuepukika

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jellyfish asiyeweza kufa hutimiza kile ambacho wanadamu wengi wametaka.

Jambo la ajabu ni kwamba sheria hii kuhusu muda wa kuishi kwa wanadamu haikutoka kwa sayansi iliyotafuta kutokufa, au angalau kurefusha maisha, bali kutoka kwa nyanja nyingine ya ujuzi ambayo pia inapendezwa na somo la maisha marefu: sayansi ya kutathmini

Ni taaluma inayotumika katika mifano ya takwimu na hisabati kwa tathmini ya hatari hasa katika tasnia ya bima na kifedha.

Hasa zaidi, lengo la sheria lilikuwa kufanya sayansi ya kuhesabu viwango vinavyofaa kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaa zinazoaminika zaidi.

Na aliyeashiria enzi mpya kwa sayansi hiyo alikuwa mwanahisabati Benjamin Grompertz katika karne ya 19, ambaye alikuwa mtaalamu wa bima.

Mnamo 1825 aliwasilisha maandishi yenye kichwa "Juu ya asili ya kazi ya wazi ya sheria ya vifo vya binadamu, na njia mpya ya kuamua thamani ya dharura ya maisha", mbele ya Royal Society huko London.

Ilikuwa ni mbinu ya hisabati iliyosema kwamba hatari ya kifo huongezeka kwa kasi kadiri tunavyozeeka , na sasa inajulikana kama "Sheria ya Gompertz ya Vifo vya Binadamu".

Kwa miaka mingi, seli zetu huacha polepole kugawanyika, na kuweka mzigo mkubwa kwa wale waliobaki, ambapo uharibika hadi miili yetu haiwezi kuendelea kuishi

Lakini ufunguo ni katika neno "exponentially".

Grompertz alikuwa amechanganua ripoti za viwango vya vifo na akagundua mbinu hiyo.

Siri

Mwishowe, sisi sote huvunjika moyo, lakini lini?

Sheria kimsingi ni hesabu ya uwezekano kwamba tutakufa katika mwaka fulani.

Yaani ukiulizwa swali lisilo la kawaida unafikiri kuna uwezekano gani wa wewe kufa mwaka ujao, ungejibu nini?

1 kati ya 1,000? 1 kati ya milioni 1?

Bila kujali hesabu yako, uwezekano huo utaongezeka maradufu kila baada ya miaka 8 .

Ikiwa una umri wa miaka 25, uwezekano wako wa kufa mwaka ujao ni mdogo: 0.03%, takriban 1 kati ya 3,000.

Ukiwa na umri wa miaka 33 ni takriban 1 kwa 1,500, Miaka 42, 1 kwa 750, na kadhalika.

Unapofikia umri wa miaka 100, uwezekano wa kuishi hadi 101 utakuwa umepungua hadi 50%.

Tangu Gompertz apendekeze sheria yake, data kutoka kwa takwimu za vifo imeithibitisha, ikiweka kikamilifu katika idadi kubwa ya nchi, vipindi vya muda, na hata katika aina mbalimbali za wanyama.

Ingawa wastani halisi wa umri wa kuishi unabadilika, kanuni ile ile ya jumla ya kwamba "nafasi ya kufa huongezeka maradufu kila baada ya miaka X" bado ni ya kweli.

Hiyo, pamoja na kushangaza, ni siri : haijulikani kwa hakika kwa nini ni hivyo.

Cha kushangaza kuna ‘’lakini’’ mbili

Kitu chengine na cha ajabu

"lakini" ya kwanza ni kwamba , mtindo tunaozungumzia unaitwa sheria ya Gompertz-Makeham, kwa hivyo tunakosa kitu.

Na kwamba kitu hicho kiliongezwa mnamo 1860 na William Makeham, mwanasayansi mwingine wa Uingereza, alipopendekeza kwamba mtindo wa Gompertz ungeweza kuboreshwa kwa kuongeza kutotegemea umri kila wakati kwa ukuaji mkubwa.

Mtindo wa Gompertz hufanya kazi vizuri sana katika mazingira ya hifadhi ambapo visababishi vya nje ya vifo ni nadra, kama vile hali ya maabara au nchi zilizo na viwango vya chini vya vifo.

lakini, kama tujuavyo, haijalishi wewe ni mchanga au mzee kiasi gani, maisha yanaweza kukatizwa kwa sababu zingine, kama vile ajali, utapiamlo, magonjwa, na kadhalika.

Gompertz alikuwa tayari ameeleza: "Inawezekana kwamba kifo ni matokeo ya sababu mbili zinazoishi pamoja; moja, bahati, bila mwelekeo wa awali wa kufa au kuzorota; nyingine, kuzorota au kutokuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia uharibifu" .

Lakini alikuwa Makeham aliyeongeza kipengele hicho cha mbinu ya hisabati, kipengele kinachobadilika zaidi ambacho kinaweza kupunguzwa kwa kupunguza hatari za kijamii na kiuchumi na siasa za kijiografia.

Hatua zilizopigwa kisayansi, dawa na usafi wa mazingira, kwa mfano, yamemaanisha viwango vya chini vya vifo katika nchi zote.

Kwa hivyo, sheria hii iliyoundwa kuuza sera za bima ikawa nyenzo muhimu kwa wanademografia na wanasosholojia na vile vile kwa wanabiolojia.

‘’Lakini’’ iliosalia hatahivyo bado inachunguzwa.

Sheria ya Gompertz-Makeham ya vifo inaelezea mienendo ya umri wa vifo vya binadamu kwa usahihi sana katika dirisha la umri la kati ya miaka 30 hadi 80.

Lakini baadhi ya tafiti zimegundua kuwa katika umri mkubwa viwango vya vifo hupanda polepole zaidi, jambo linalojulikana kwa wanasayansi kama "nadharia ya kupungua kwa vifo vya uzeeni."

Gompertz mwenyewe inaonekana kuwa aliona viwango hivi kwasababu meza za maisha ya binadamu zilionyesha kwamba kuanzia umri wa miaka 92 kiwango cha vifo vya kila mwaka kilikuwa 0.25.

Kwa nini sheria inaacha kutumika baada ya miaka 80? Nini kinabadilika unapofikia umri huo?

Wataalam bado hawana jibu la swali hilo.

Je, inawezakana kwamba kama jellyfish, kitu ndani yetu kinarudisha ujana, angalau kwa muda?

Iliyosomwa zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?