Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MATUKIO YALIYOJIRI: Habarika na Newsday Swahili 🇹🇿


  1. Hofu yatanda baada ya mtu mmoja kujichoma moto Mombasa

    Mwanamume mmoja kwa sasa anaendelea kupata nafuu katika hospitali kuu ya Pwani mjini baada ya kujichoma moto eneo la Mwembe Tayari kaunti ya Mombasa.

    Katika video isiyo na tarehe iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi, mtu huyo ambaye hakutambulika alinaswa akijichoma moto akiwa amesimama juu ya jengo fulani huku watu wa karibu wakitazama.

    Hata hivyo polisi bado hawajazungumzia tukio hilo.

    Alionekana akijimiminia kitu kinachoshukiwa kuwa mafuta kabla ya kujiwasha moto.V

    ilio kutoka kwa watazamaji vilisikika huku wengine wakitazama tu kwa mshangao mtu huyo aliyekuwa akichomeka akianguka chini.

    Mtu mwingine alionekana akimkimbilia huku watu wakiwa wamekusanyika ili kuelewa kinachoendelea.

    Ripoti sasa zinaonyesha kuwa mwanamume huyo kwa sasa anapokea matibabu ya majeraha yake.

    Kufuatia kisa hicho, baadhi ya Wakenya mtandaoni wameibuka na nadharia kadhaa ili kujaribu kueleza sababu ya vitendo vya mwanamume huyo.

    Idadi kubwa imedai kuwa mwanamume huyo alikuwa mwanafunzi wa uhandisi aliyejichoma akipinga changamoto kali za kiuchumi zinazowakabili mamilioni ya Wakenya.

  2. Moto wa Maui: Mkuu wa idara ya dharura aacha kazi baada ya kukosolewa

    Wakazi

    Mkuu idara ya kushughulikia matukio ya dharura ya Maui amejiuzulu siku moja baada ya kutetea kushindwa kwa wakala wake kuwasha mfumo wake wa kengele katika ajali mbaya ya moto ya mwituni wiki iliyopita.

    Herman Andaya, ambaye hakuwa na uzoefu wa awali katika usimamizi wa dharura, alitaja "sababu za kiafya" za kujiuzulu.

    Wakazi wa kisiwa cha Hawaii wameiambia BBC muitikio wa haraka wa dharura ungeweza kuokoa maisha zaidi.

    Takribani watu 111 wameripotiwa kufariki. Mamia bado hawajulikani walipo.

    Mfumo wa kisasa wa Maui, unaojumuisha ving'ora 80 kuzunguka kisiwa hicho, hujaribiwa siku ya kwanza ya kila mwezi, sauti yake ya sekunde 60 ni sehemu ya kawaida ya maisha huko Lahaina.

    Lakini siku ya moto walikaa kimya. Mnamo Jumatano, mkuu wa Shirika la Usimamizi wa Dharura la Maui Bw Andaya alisisitiza kuwa hajutii uamuzi huo.

    Alisema alihofia ving'ora - ambavyo mara nyingi vinasikika kwa ajili ya tsunami - vingepelekea baadhi ya watu huko Lahaina kukimbia hadi sehemu ya juu, pengine kwenye njia ya moto unaoendelea kwa kasi.

    Lakini huko Lahaina siku ya Alhamisi, hakuna hata mmoja wa wakazi waliozungumza na BBC aliyekubali maelezo haya, wakisema king'ora hicho kingetoa onyo muhimu kuhusu hatari inayokaribia.

  3. Shambulio la ndege isiyo na rubani lapiga jengo katikati mwa Moscow

    Jiji la Moscow

    Shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine limepiga jengo moja mjini Moscow, na kusababisha mlipuko uliosikika katika eneo la biashara la mji huo, maafisa wa Urusi wamesema.

    Meya Sergei Sobyanin alisema ulinzi wa anga uliidungua ndege hiyo isiyo na rubani huku vifusi vyake vikiangukia kwenye Kituo cha Maonesho cha jiji hilo.

    Ni alama ya hivi punde katika mfululizo wa mashambulizi hayo kwenye mji mkuu wa Urusi.

    Picha ambazo hazijathibitishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionekana kuonyesha moshi mzito wa kijivu ukipanda angani usiku juu ya jiji la Moscow.

  4. Habari na karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?