Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Afya: Dalili nne za mtu mwenye huzuni na nini cha kufanya

Afya: Dalili nne za mtu mwenye huzuni na nini cha kufanya

w

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Huzuni ni jambo la asili pindi mtu akipoteza kitu ambacho anahisi kuwa na uhusiano nacho. Mfano kifo au kuvunjika kwa uhusiano. Kupoteza kiungo cha mwili kwa kukatwa. Huzuni ni jambo la kiasili na ni la kawaida. Ni njia ya kisaikolojia ya kupambana na mshtuko unaoletwa na hasara.

Nguvu ya majibu kutokana na huzuni hutofautiana kulingana na mambo kadhaa, kama vile uhusiano wako na mtu aliyekufa. Kwa mfano, vifo vya kikatili au kufiwa na mtoto, husababisha maumivu makali zaidi kuliko kifo cha mtu mzee.

Dalili za huzuni

Dalili za kawaida za huzuni zinaweza kugawanywa katika vipimo vinne.

Dalili za kimwili: Hizi huathiri kazi za kibiolojia za mwili wa binadamu. Zinaweza kujumuisha mabadiliko katika tabia ya kula, kama vile kula kupita kiasi au kupoteza hamu ya kula. Pia, mfumo wako wa kinga unaweza kudhoofika, ikimaanisha kuwa utapata mgonjwa kwa urahisi.

Dalili za kiakili: Hizi huathiri mwelekeo wa utambuzi. Kupunguwa umakinifu, kama vile kurudia-rudia kufanya kazi hiyo hiyo. Kuchanganyikiwa pia kunaweza kutokea, na ugumu wa kukumbuka mambo fulani, kama vile majina ya watoto au vyumba maalum ndani ya nyumba. Kufanya maamuzi na kujifunza mambo mapya kunaweza pia kuwa changamoto. Haya yanaweza kuchagiwa na wingi wa huzuni na kuleta athari kwenye ubongo.

Dalili za kijamii: Hizi ni pamoja na jinsi unavyohusiana na wengine. Baadhi ya watu wanaweza kujiondoa na kuacha shughuli wanazofurahia katika jamii. Wengine wanaweza kuonyesha mifadhaiko. Wanaweza kuwa tegemezi zaidi, na kuhitaji msaada wa wengine hata kwa maamuzi rahisi.

Dalili za kiroho: Hizi zinahusiana na imani na maadili ya kidini au ya kiroho. Huzuni inaweza kukufanya ujiulize Mungu wako alikuwa wapi wakati mpendwa wako alipokufa. Unaweza kutilia shaka uwezo wa Mungu au kutilia shaka ufanisi wa maombi yako.

Dalili za huzuni zinaweza kuwa na madhara iwapo zitadumu kwa muda mrefu kuliko kawaida (zaidi ya miezi 12) au kama zitaathiri utendakazi wako hadi kufikia hatua ambayo huwezi kufanya shughuli zako za kawaida za kila siku kwa urahisi.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ishara mbaya

Huzuni ya muda mrefu: Ingawa huzuni ni mchakato wa asili, kipindi kirefu cha huzuni itakulazimu upate usaidizi wa ziada. Ikiwa huzuni yako itaendelea zaidi ya miezi sita bila nafuu, kutafuta usaidizi wa kitaaluma kunaweza kuwa na manufaa.

Utendaji mbaya wa kila siku: Huzuni inaweza kuvuruga maisha ya kila siku, lakini ikiwa inathiri sana uwezo wako wa kufanya kazi, ni ishara kwamba msaada wa kitaalamu ni muhimu kwako. Unaweza pia kuhitaji usaidizi wa wenzako au watu wengine muhimu.

Dhiki ya kihisia inayoendelea: Hisia za upweke. Ikiwa hisia hizi zitakuelemea na kutatiza maisha yako ya kila siku mara kwa mara, ni wakati wa kufikiria kutafuta usaidizi wa kitaalamu. Washauri wanaweza kukusaidia kukabiliana na changamoto na kupata mbinu bora za kukabiliana na hali hiyo.

Mawazo mabaya: Katika hali nyingine, huzuni inaweza kusababisha mawazo ya kujidhuru au hamu ya kujiunga na marehemu na hisia za kukata tamaa. Ukikumbana na mawazo ya kujiua au mawazo mabovu, kama vile kutumia dawa za kulevya, wasiliana na mshauri au mtaalamu wa afya ya akili. Hii ni muhimu kwa usalama na ustawi wako.

Cha kufanya

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kutafuta msaada wa kitaalamu sio udhaifu. Badala yake, ushauri nasaha hutoa nafasi salama ya kueleza hisia zako, kupata maarifa muhimu na kujifunza mikakati ya kukabiliana na hali ambayo imekuja kulingana na mambo yaliyokukumba.

Zungumza kuhusu jinsi unavyohisi. Hii hukusaidia kueleza hisia ambazo unaweza kuwa umezizuia hapo awali. Pia hukusaidia kufikia mazungumzo chanya. Kuzungumza pia husaidia kukufikisha mahali ambapo unaweza kukubali hasara na kusonga mbele na maisha yako.

Uponyaji wa huzuni huchukua muda. Kutafuta msaada ni hatua ya ujasiri kuelekea kupata faraja na kurejesha ustawi wako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?