Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2022

​Ndege 4 za Urusi zaangushwa Ukraine huku baadhi ya wanajeshi wakikataa kutekeleza amri

Picha
Post update Baadhi ya wanajeshi wa Urusi wakataa amri , ndege  nne zaangushwa - vimesema vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine Wakati Ukraine ikielekea katika siku ya ishirini ya uvamizi wa Urusi katika ardhi yake, Maafisa wakuu wa jeshi la Ukraine wametoa taarifa yao kila alfajiri Vikosi vya Urusi vinasalia kushambulia maeneo kadhaa nchini Ukraine , na vimeshindwa kupiga hatua zaidi Hata hivyo wanajeshi wa Urusi wameendelea kufanya mashambulizi ya makombora na mabomu kwenye miundombinu muhimu  Wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakitumia vituo vya afya katika maeneo yanayokaliwa kuwatibu waliojeruhiwa Helikopta nne za Urusi ziliangushwa na vikosi vya Ukraine Vikosi vya Ukraine vimefanikiwa kuzuia majaribio ya Urusi ya kuuteka mji wa bandari wa kusini wa Mariupol uliokuwa na ushindani mkubwa na hakujawa na dalili zozote za kutua kwa jeshi la Urusi katika eneo la Bahari Nyeusi. Baadhi ya wanajeshi wa Urusi wanakataa kutekeleza amri. Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter

Vifo vya Ajali treni DRC vyafikia 75

Picha
Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya treni kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa imefikia 75 , hii ni kwa mujibu wa maafisa wa Shirika la reli na Wizara ya Mawaasiliano. Maafisa hao wanasema idadi ya majeruhi ni 125 wengi wao wakiwa ni akina mama na watoto. Idadi hii mpya imetangazwa na Mkurugenzi wa shirika la Reli Bwana Abien Mutomb, baada ya kutembelea eneo la ajali hiyo akandamana na timu maalum iliyoundwa kuchunguza mkasa huo. Siku ya Jumamosi maafisa wa shirika la reli walikuwa wamethibitisha kuwa idadi ya waliofariki ilikuwa watu 61 wakiwemo wanawake na watoto .Taarifa hiyo ya Jumamosi ilimnukuu Marc Manyonga Ndambo, Mkurugenzi wa miundo mbinu akizungumza na chombo cha Habari cha AFP kuwa watu 52 waliojeruhiwa waliokolewa. Vyombo vya Habari nchini humo vilimnukuu gavana wa jimbo hilo Fifi Mazuka akisema kwamba takriban watu 60 wamefariki. ‘’Ilikuwa treni ya mizigo iliokuwa ikibeba mamia ya watu waliokuwa wakisafiri kutoka eneo moja hadi jingine kwa njia

Urusi yatoa masharti ya kusitisha vita Ukrane.

Picha
Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni "wakati wowote" ikiwa Ukraine itatimiza masharti ya Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Ukraine lazima itambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama mataifa huru.  Mbali na hayo, Peskov anasema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote (kama vile Nato, kwa mfano).  Anaongeza kuwa Urusi itamaliza "kuondoa jeshi" kwa Ukraine, na ikiwa masharti haya yatatimizwa hatua za kijeshi za Urusi "zitakoma mara moja".  Msemaji wa Kremlin amesisitiza kuwa Urusi haitaki kutoa madai yoyote zaidi ya eneo nchini Ukraine. Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter

Aliyelipwa Fidia ya mamilioni ya fedha kimakosa akataa kurejesha fedha

Picha
Mfuko wa Marekani ambao ulijitwikwa jukumu la kuwalipa fidia waathiriwa wa shambulizi la kigaidi la 1998 jijini Nairobi umemshtaki mwanamke ambaye alipokea kimakosa mamilioni ya pesa ambayo inadaiwa alikataa kurejesha.  Mfuko huo umeomba Mahakama Kuu itoe amri ya kurejeshewa fedha alizopokea Mary Ngunyi Muiruri, kiasi cha dola za Marekani 65,683.50 (Sh milioni 7.4 za Kenya) mnamo Novemba mwaka 2020, Gazeti la Nation la Kenya limeripoti. Hazina hiyo ilinuia kumlipa Mary Njoki Muiruri pesa hizo, lakini mkanganyiko wa majina ya kati ulisababisha mtu ambaye hakukusudiwa akipokea pesa hizo.  Bi Ngunyi hajajibu madai hayo.  Mfuko huo wa fidia ulikuwa umeomba benki ya eneo hilo kurejesha pesa hizo. Benki ya Nairobi, hata hivyo, ilisema Bi Ngunyi alikataa kuridhia ombi hilo, hivyo kuwasilisha shauri la kisheria.  Benki hiyo inaongeza kuwa mawasiliano kati ya Mfuko wa Udhibiti wa Mabomu wa Ubalozi wa Marekani wa 1998 na Ngunyi yalionesha kuwa kulikuwa na mzozo kuhusu ni nani mpokeaji halisi wa

Siku ya Wanawake Duniani: Ina maana gani Afrika?

Picha
CHANZO CHA PICHA,  UN WOMEN/BENNIE KHANYIZIRA Kila mwaka Machi 08, Umoja wa Mataifa husheherekea haki zilizopatikana kwa bidii za wanawake- na kuangazia changamoto ambazo bado ziko mbele katika kukomesha ubaguzi wa kijinsia katika karibu nyanja zote za maisha. "Usawa wa kijinsia wa leo, kesho na endelevu" ndio kauli mbiu ambayo Umoja wa Mataifa umeichagua mwaka huu kuadhimisha kile kinachojulikana rasmi kama Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Kwa nini imechagua mada hii? Dkt Maxime Houinato, mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, aliiambia  kwamba "kukuza usawa wa kijinsia katika mazingira ya mzozo wa mabadiliko ya tabia nchi na upunguzaji wa hatari ya majanga ni mojawapo ya changamoto kubwa duniani kwa karne ya 21". "Wanawake na wasichana wanapitia athari kubwa zaidi za mabadiliko ya tabia nchi," aliongeza. MATANGAZO Kwa kweli, utafiti wa Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa wanawake na wasichana hufa kwa idadi kubwa