Virusi vya Corona: Vitu gani tunaweza kujifunza kwa nchi ambazo zimepambana mapema na corona?

Mlipuko wa pili wa maambukizi ya virusi vya corona sio tena suala la ikiwa linaweza kutokea badala yake ni lini litatokea na athari yake itakuwaje," amesema mwanabaolojia Dkt. Jennifer Rohn, ambaye amekuwa akifuatilia vile janga hili linavyoedelea Asia na kusambaa kote duniani.
Shirika la Afya Dunia (WHO) limesema maambukizi mapya huenda yakaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu na kutahitaji juhudi za pamoja ili kuudhibiti.
Hata nchi zenye mikakati inayofanyakazi kwa ufasaha kukabiliana na jaga hili kupitia upimaji, kutafuta walioathirika na hatua za kusalia ndani - kama vile Korea Kusii na Japani huko Asia, lakini pia Ujerumani na Ulaya - zimeshuhudia mlipuko wa pili wa maambukizi punde tu baada ya kulegezwa kwa masharti.
Wiki hii, timu ya Umoja wa Ulaya yenye kupambana na ugonjwa wa Covid-19 ilipedekeza kwamba Ulaya inastahili kujiandaa kwa mlipuko wa pili - na swali lililopo ni lini utatokea na athari zake zitakuwa na ukubwa gani, amesema mkurugenzi wa timu hiyo Andrea Ammon, kulingana na taarifa ya gazeti la The Guardian.
Serikali kote duniani kwa sasa hivi zinahitajika kujiandaa kwa uwezekano wa kutokea kwa wimbi la pili la virusi vya corona huku macho yao yakiangazia eneo la Asia mashariki.
Je ni kipi tunaweza kujifunza kutoka kwa nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kwanza na kwa sasa hivi ziko mbele katika suala la kukabiliana na vugonjwa wa Covid-19?

Kila aliyeambukizwa, kila aliyetangamana nae

Cha msingi tunachoweza kujifunza kwa eneo la Asia mashariki ikilinganishwa na kwengine duniani, kulingana na wataalamu wa afya wa WHO wanaofuatilia eneo hilo, ni kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwapata, kuwatenga, kupima na kufuatilia kila mwathirika, na kuwafuatilia na kuwaweka karantini kila mmoja atakayekuwa na ametangamana na mwathirika," amesema mkuu wa WHO Tedros Adhanom.
Dkt. Rohn, mtaalamu wa virusi na magonjwa ya kuambukiza kutoka chuo cha London, anakubaliana na hilo: " Kuzingatia data kutoka Asia, tumeona kwamba namna pekee ya kudhibiti wimbi la pili la maambukizi ni kupitia upimaji wa kasi kwa raia, kuwatafuta na kisha kuwaweka karantini."
Kwa mfano, Korea Kusini wakati fulani ilikuwa kitovu cha ugonjwa Covid-19 lakini serikali ikachukua hatua mapema na kuanza kupima watu huku ikitegemea mfumo unaotumia programu za kwenye simu na ule wa kupokea habari kutoka kwa setilaiti (GPS) kutafuta walioathirika.
Mfumo huu uliwaruhusu kuweka mifumo ya tahadhari na hata kama ugonjwa huo unadhibitiwa lakini kukatokea kuwa na eneo jengine linalopata maambukizi kwa wingi, linaweza kufungiwa," ameongeza Dkt. Rohn.
Ufanisi wa hatua hiyo ulithibitishwa pale maambukizi mapya - yaliporekodiwa mapema Mei, baada ya wiki kadhaa ambapo hakuwa kumerekodiwa maambukizi yoyote - yakafuatilia na kuhusishwa na maeneo maalum katika mji ambao ni maarufu kwa vilabu vya usiku. Na kulihusisha kufuatilia watu wengi zaidi kama 11,000.
Uchakataji wa takwimu
Tunachoweza kujifunza cha pili, wataalamu wanasema, ni kwamba kuna umuhimu wa kuchukua taarifa na kuzifasiri na kutafiti kutoka maeneo kama vile China, Japani na Korea Kusini kuelewa vile kirusi hicho kinavyoendeleza uwepo wake.
"Kwa sasa hivi tunataarifa kidogo kuhusu muda wa kuanzia kwa maambukizi hadi uponaji lakini bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu muda wa maambukizi wakati wa kutangamana," amesema Profesa Alistair McGuire, mwenyekiti wa masuala ya afya katika Idara ya sera ya afya, chuo cha London School of Economics.
Hiki ni kirusi kipya ambacho kina tabia ya kubadika badilika ikilinganishwa na magonjwa mengine ya virusi ambayo yalijitokeza hivi karibuni kama vile ugonjwa wa SARS huko Asia, au Ebola barani Afrika - kwa hiyo mikusanyiko na taarifa kujaza maeneo mengi ambayo bado yanazua maswali ni jambo la msingi.
Cha tatu, ni kufahamu vile kirusi hiki kitakavyobadilika baada ya kulegezwa kwa masharti: "Tusiwe na matumaini sana," ameonya Profesa McGuire akiangazia kilichotokea bara la Asia.
Kufanikiwa kutekeleza hatua ya kusalia ndani hakumaanishi kwamba eneo fulani halitapata maambukizi ya virusi. Eneo la Hokkaido nchini Japani, lilikuwa la kwanza kutekeleza hatua hiyo mwishoni mwa Februari.
Kufikia katikati ya Machi, idadi ya maambukizi mapya ilikuwa imepungua hadi kwa mtu mmoja au wawili kwa siku. Mafanikio ya hatua hiyo ni kwamba ile hali ya hatari iliondolewa na kufikia Aprili, shule zilikuwa zimefunguliwa. Lakini chini ya mwezi mmoja, hali ya hatari iliwekwa tena kwasababu eneo hilo la kisiwani lilikuwa linapitia wakati mgumu kupambana na wimbi la pili la maambukizi.
Hilo kwa sasa hivi sio jambo la ajabu kutokea, amesema Dkt. Rohn, "Hata kwa nchi zinazoonekana kwamba mlipuko huo umedhibitiwa, kwasababu masharti yamelegezwa maambukizi yanaanza kuongezeka. Hili ni jambo ambalo litatokea kote duniani".

Kupima - sio mara moja bali mara mbili

Kuna ujumbe unaotolewa na wataalamu wa afya kila wakati: "Cha msingi ambacho tumejifunza kutoka kwa Asia ni kwamba kupima ni hatua ya msingi," amesema Dkt. Rohn.
Moja ya sababu Korea Kusini ilipata ufanisi mkubwa katika kudhibiti virusi ni kwasababu ya hatua ya upimaji kwa watu wengi, kuwatafuta na kuwaweka karantini,"mtaalamu huyo aliongeza.
Mara ya kwanza, idadi ya walioathirika Korea Kusini iliongezeka. Lakini nchi hiyo ilivumbua mfumo wa kupima takribani watu 10,000 kwa siku bila malipo kuanzia Februari, kwa kuzingatia kile ambacho walikuwa wamepitia na taarifa walizokusanya wakati wa mlipuko wa 2015, wa ugonjwa wa Matatizo ya Kupumua Mashariki ya Kati (MERS).
"Vile walivyoimarisha mfumo wao na kuanza kupima watu ni jambo la kupigiwa mfano," Ooi Eng Eong, profesa wa magonjwa ya kuambukiza katika chuo kikuu cha Taifa cha Singapore, alizungumza na BBC mwezi Machi.
Nchi za magharibi ambazo zilifuata mfumo wa upimaji wa Asia Mashariki - kwa mfano Ujerumani, - ilifanikiwa kuhakikisha idadi ya wanaokufa ni ya chini ikilinganishwa na nchi za Ulaya ambazo hazikufuata mfumo huo - kama vile Uingereza na Uhispania.
Lakini siyo hilo pekee: vile Asia ilivyosimamia takwimu zake pia kunaonesha umuhimu wa kupima zaidi ya mara moja.
"Sio kwamba tunahitaji tu kujua wale waliopata maambukizi, ambako unaweza kufahamu kupitia vipimo vya kwenye mdomo, pia unahitaji kupima kupitia kinga ya mwili ili kufahamu ni nani aliyetangamana nae," amesema Profesa McGuire.
Taiwan na Japani, kwa mfano, wale ambao vipimo vilionesha wamepata maambukizi - na wale ambao walikuwa wametangamana nao - walifuatiliwa, wakatafutwa na kuwekwa karantini, na hivyo basi takwimu zikawa zinaonesha ni nani aliyeambukizwa na yuko wapi na vile ambavyo maambukizi yamesambaa kwa haraka.
"Wanaobaini corona" Singapore kuligonga vichwa vya habari kote duniani, wakati ambapo wanawatafuta na kuwasiliaa na maelfu ya watu kwa kutumia picha za video kwenye CCTV na njia zengine na kutaka watu wajitenge hadi pale majibu yatakapotoka. Wale waliojitenga walipigiwa simu mara kadhaa kwa siku na wakati mwengine hata kuhitajika kutuma picha za kuthibitisha pale walipo.
Hong Kong ilianzisha mfumo usio wa kawaida unaotumia bangili za kielektroniki kwa wale wanaoingia nchini humo kutoka mataifa ya nje.
Nchi ambazo hazijatekeleza hatua ya kupima na kutafuta ambao huenda walipata maambukizi wanakosa takwimu muhimu linapokuja suala la kudhibiti mawimbi kadhaa, wataalamu wanasema.
"Tunajua kwamba hili ni la kweli, ugonjwa wa kuambukizwa hasa," Profesa McGuire ameongeza, "Unachohitaji kuangalia ni kile kilichotokea Korea Kusini, nchi yenye sera bora … baada ya kulegeza masharti, mtu mmoja alifanikiwa kuambukiza watu zaidi ya 100 kwa wikendi moja tu."
Na nchi hiyo inajianda kwa uwezekano wa kutokea kwa mlipuko mwengine, baada ya kutokea kwa maambukizi mapya ya Covid-19 Mei 19 katika hospitali moja kubwa mjini Seoul.
Kwasababu wamekuwa wakifuatilia na kukusanya takwimu zao kila wakati, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Korea (KCDC) kimefanikiwa kubaini chanzo cha maambukizi mapya tisa punde tu baada ya kutokea kulingana na Shirika la Habari la Yonhap.

Mabadiliko katika sekta ya afya ya umma

Pia ni muhimu kuangazia kile sekta ya huduma za afya za umma inaweza kujifunza kutokana na tajriba yao wenyewe, amesema Profesa Judit Vall, ambaye amekuwa akifuatilia vile mfumo unavyokabiliana na virusi vya corona kutoka chuo cha School of Economics at Universitat de Barcelona.
"Katika janga hili, sekta ya afya imethibitisha inaweza kufanya mabadiliko ya haraka," anasema
.China ilijenga hospitali ya vitanda 1,000 mjini Wuhan - kitovu cha ugonjwa wa Covid-19 kwa siku nane pekee na kuongoza katika kuonesha namna ya kujipanga na kuwa na hospitali ya hali ya dharura.
"Hospitali na vituo vya kutoa huduma zingine za msingi duniani wamejifunza mengi kutoka kwa wengine lakini pia kutoka kwao wenyewe," amesema Profesa Vall, "na watakuwa katika nafasi nzuri zaidi kukabiliana na wimbi jingine litakapotokea."
Pia kuna ushauri mwengine muhimu wakati ambapo janga hili linaonekana kuwa la muda mrefu, amesema Profesa Vall: "Kuangalia madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya afya ya akili kwa wafanyakazi wako."
"Kuna utafiti Asia unaoonesha vile kupitia hali kama hizi, wahudumu wa afya wanaweza kupata matatizo yanayosababishwa na mfadhaiko," anasema.
"Kwa kurejelelea takwimu zilizotangulia, tuligundua kwamba hata baada ya miaka mitatu ugonjwa wa mlipuko wa SARS mapema miaka ya 2000, asilimia 10 ya wahudumu wa afya wakati huo bado walikuwa na dalili za mfadhaiko wa akili."
Wimbi la ugonjwa...kwa kipindi cha miezi mingi
Kama wataalam wa magonjwa wanaofuatilia mwenendo wa janga kwa wakati wote tayari wamegundua kwamba kirusi hutembea "katika hali ya mawimbi".
''Lakini ni katika hali ya wimbi pekee tunafunga shughuli na kukata uwezekano wa kuenea kwa ugonjwa,'' anasema Dokta Rohn. ''Vinginevyo tungeshuhudia madhara mabaya sana kwa kiasi kikubwa.''
maambukizi huja wakati wa kuondoa vizuizi. Hiki ndicho kinachofanyika unapokuwa na virusi vipya na hakuna kinga miongoni mwa watu,'' aliongeza.
Milipuko ya pili ni kawaida katika mazingira ya majanga ya magonjwa, kama historia inavyoeleza- na Shirika la Afya duniani, WHO linasema kuwa "wimbi huenea kwa miezi kadhaa'', hivyo kulegeza masharti haraka kunaweza kuwa ishara ya mapema kabisa.
Si tu tunachoweza kujifunza kutoka nchi nyingine, lakini ni tunaweza kujifunza nini kutokana na matukio yaliyopita,'' anasema Dokta Laia Maynou, kutoka idara ya sera ya afya,'' na hasa kilichotokea wakati wa mafua ya Uhispania mwaka 1918, ambacho ni uzoefu tulionao ambao unaweza kufananishwa na janga la sasa.''
''Wakati huo Data za kina zilikusanywa namna gani masharti ya kutotoka nje yalilegezwa. Tafiti mpya zinazotegemea takwimu za mani zinatupa taarifa muhimu kuhusu namna wimbi la pili la ugonjwa linavyoshambulia watu,'' anasema Dokta Maynou.
''Mwaka 1918, kulikuwa na wimbi baada ya wimbi la maambukizi duniani kota, kutegemea na namna sera madhubuti zilizokuwa zimewekwa,'' aliongeza Dokta Rohn.
Tuna matumaini kwa asili ... lakini hivi sasa serikali zinahitaji kusimamia matarajio ya watu."
Na kama tulivyoona huko Asia, "uwezekano mkubwa kuwa ni" kutazama, kusubiri na kuchukua hatua ", na tunaweza kujikuta katika hali hii hadi mwaka 2022," anasema Dokta Rohn.

Kusubiri

Lakini labda somo kubwa hapa la kulichukua ni kuwa ''hakuna njia moja ambayo imefanikiwa'' pekee, anasema Dokta Naoko Ishikawa, Mkurugenzi wa idara ya kupambana na janga la Covid -19 katika shirika la WHO nayesimamia nchi za ukanda wa Magharibi mwa Pasifiki.
''Si vipimo pekee na kuepuka kuchangamana pekee. Nchi nyingi na maeneo mengi katika ukanda huu zimefanya sana hatua hizi'', aliongeza.
Uwezo wa kupambana na wimbi la pili la majanga unaonekana kutegemea muunganiko wa hatua zinazochukuliwa kwa pamoja , pia data zinazotumika kutathimini na kuchukua hatua kutokana na tathimini hizo.
''Njia nyingi zinazochukuliwa sasa ni funzo ambalo lilipatikana wakati wa mlipuko wa homa ya SARS ya mwaka 2003,'' anasema bwana Ishikawa.
WHO imeonya dhidi ya kukisia kuhusu lini virusi vitakwisha kabisa.
''Mpaka pale tutakapokuwa na chanjo, sisi sote tuko kwenye hatari.''
Habari njema pekee ni kuwa ''Sote tuko kwenye njia moja. Dunia imeungana kwa namna ambayo haikutarajiwa, na nina matumaini kuwa sayansi itatoa majibu ya tatizo hili,'' anasema Dokta Rohn.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?