Kifo cha George Floyd: Wakili akiita 'mauaji yaliyopangwa'

Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji".
Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza.
"Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua," alisema
matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la Philadelphia.
Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja .
Ripoti ya Uchunguzi ya West Philadelphia, imesema kuwa magari ya polisi pia yalichomwa moto.
Miji kadhaa ya Marekani imeweka amri ya kutotoka nje.
Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter uliosema: Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka. Walete wanajeshi wetu waingilie kati ".
Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.
Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives Matters.
Katika video Bw. Chauvin alionekana akipiga goti kwenye shingo la Floyd kwa dakika kadhaa huku Floyd akisikika akisema kuwa hawezi kupumua.
Maafisa wengine watatu waliokuwepo wakati wa tukio hilo pia wamefutwa kazi.
"Kutokana na ukweli kwamba afisa wa polisi Chauvin aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo kwa takriban dakika tatu baada ya Floyd kupoteza fahamu hatuelewi kuwa hayo hayakuwa mauaji ya kiwango cha kwanza. Hatuelewi ni kwanini maafisa wote hawa hawajakamatwa ," wakili Crump alisema.
Maafisa wengine watatu waliokuwepo wakati wa tukio hilo wamefutwa kazi.
Kwa wengi ghadhabu ya kifo cha George Floyd pia inaonesha hasira juu ya kutokuwepo kwa usawa na kuwepo kwa ubaguzi katika masuala ya kijamii na kiuchumi, ambao haupo Minneapolis pekee.
Kikosi cha wanajeshi wa Ulinzi nchini Marekani- National Guard - cha wanajeshi wa akiba kinachoshughulikia hali za dharura ndani ya nchi -kimesema jana kuwa Wanajeshi wake 5,000 wamepelekwa katika majimbo 15 na Washington DC. Kiliongeza kuwa " polisi wa taifa bado wanasalia kuwajibika kwa usalama ".
Katika mahojiano na kituo cha habari cha CBS, wakili Benjamin Crump pia alisemakwamba "sasa tuna sauti kutoka kwa polisi na tunasikia ambapo polisi mmoja wao akisema 'hajatokwa na damu, labda tunaweza kumgeuza ', lakini afisa Chauvin anasema 'hapana, tutaendelea kumlaza hivi '. Hiyo inaonesha kuwa alfanya hivyo kwa makusudi.
"Na pia kwamba afisa Chauvin aliendelea kushindilia goti lake kwa karibu dakika tatu baada ya George Floyd kupoteza fahamu."
Wakili alisema pia kuwa Bwana Chauvin na Bwana Floyd walikuwa tayari wanafahamiana kabla ya kifo chake.
Alisema kuwa familia ya Floyd ili "fahamishwa kuhusu kifo chake na mmiliki wa kilabu ambacho kwamba Derek Chauvin alikuwa polisi ambaye alikuwa akilinda katika kilabu hicho wakati hayupo ambako pia George Floyd alikua mlinzi, kwa hiyo walikua wanapokezana".


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?