Virusi vya corona: Kwa miaka 20 nimekuwa nikijitayarisha kukabiliana na ugonjwa huu

Maana ya kukabiliana na hofu ya muda mrefu ya kupata viini kwa mwanahabari was Newsday Swahili wakati wa janga la virusi vya corona.
Tangu akiwa mtoto amekuwa akifahamu namna ya kuzingatia usafi na pia amekuwa na ujuzi wa kuzuia hofu yake isipundukie na kushidwa kuidhibiti.
''Nilikuwa nimeketi kwenye sakafu ya jikoni, nikitumia dawa ya kuua vijidudu nilipopata ufunuo: Nimetumia miaka 20 nikitekeleza yale yanayotekelezwa sasa hivi kukabiliana na janga la corona''.
Nilipokuwa na miaka 10 na kadhaa, niligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kushindwa kudhibiti mawazo na misukumo.
Kwa karibia theluthi mbili ya maisha yangu, nimekuwa na ghadhabu kali kwasababu ya virusi, kujua vile vinavyoweza kusambazwa na ninavyoweza kujikinga dhidi ya virusi hivyo. Na hilo limeniweka mstari wa mbele katika kukabiliana na virusi katika kile kinachohimizwa sasa hivi duniani.
Kutokaribiana unapokuwa nje ya nyumba yako. Kuosha mikono baada ya kila unachoshika ambacho kimeshikwa na wengine, kunyunyizia dawa nafaka baada ya kuzinunua kutoka duka la jumla la kufanyia manunuzi - hayo ni mambo ambayo nimekuwa nikiyafanya maishani mwangu.
Nimetambua mengi tu ambayo nimekuwa nikiyaendeleza katika utamaduni huu wa kukabiliana na virusi vya corona. Lakini kile ambacho nimekigundua zaidi, ni wasiwasi wa kwamba hakuna kipindi mtu anajiamini kuwa salama kutokana na maambukizi.
Maelfu au pengine mabilioni ya watu kote duniani kwa sasa hivi wanajiuliza:
"Je yule mtu niliyekutana naye dukani alinisongelea kwa karibu mno?"
"Je nimeosha mikono yangu kwa muda unaohitajika?"
"Je sabuni hii ninayoitumia itaua vijidudu vyote?"
Katikati ya karne ya 19, madaktari wa Ufaransa waliipatia hali hii jina na kuiita, 'wazimu wa kuwa na wasiwasi'.
Hayo ndio maelezo mazuri zaidi kuwahi kuyaona kipindi ambacho nimekuwa nikihisi kuwa katika hali mbaya zaidi. Na inaonekana watu wengi wanapitia hali kama hiyo wakati janga la virusi vya corona linapoendelea.
Tunaweza kuwa na uhakika kwamba kutokaribiana, kuosha mikono na kufuata kanuni za kusalia ndani kunaweza kutukinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona. Lakini huwezi kukosa kuwa na wasiwasi na mashaka.
Sio kwamba ni hisia mbaya tunazokuwa nazo. Ni baadhi ya yale ambayo yamekuwa yakitufanya kuwa makini.
Tatizo ni kwamba maambukizi yanaweza kuwa vigumu kudhibitiwa.
Ninavyofahamu ni kuwa, wasiwasi huanza pale unapohisi, "Je niko msafi inavyotakikana?"
Lakini hali inazidi kuwa mbaya pale unapoanza kujiuliza, "Je nitaweza kurejelea tena maisha ya kawaida?"
Nilikulia nchini Canada, ambapo nilikuwa na tatizo la kudhibiti uwoga na hofu tangu nikiwa mtoto - miaka mitano au hivi. Nikiwa na miaka 12, hisia hizo zilikuwa zimejikita sehemu moja hasa kwenye usafi na maambukizi: watu hurusha matone ya mate wanapozungumza, viini husambaa wanapokosa kuosha mikono vizuri baada ya kutoka chooni na bakteria zote hatari nilizokuwa naweza kuzifikiria zilikuwa zinanizunguka.
Hatimaye familia yangu ilibaini kwamba nilikuwa nakwepa kushika vitu kama kifundo cha mlango, kuzima taa na hata kusugua mikono yangu.
Nilikuwa na bahati kuwa na wazazi wenye kunipa usaidizi wote niliohitaji, walinisikiliza kila nilipokuwa nataka kuuliza au kuelewa jambo, walinisaidia kufahamu urasimu wa mfumo wa afya ya akili. Na nilianza kupata tiba na kupewa dawa ambazo nilihitajika kunywa kila siku.
Matibabu hayo na jinsi ya kudhibiti mawazo na msukumo, vilikuwa sehemu ya maisha yangu. Lakini vinitatiza maishani hasa nilipokuwa kijana mwanzoni mwa miaka yangu ya 20. Niliporejea nyumbani baada ya masomo yangu ya shule ya upili na chuo kikuu, nilikuwa natumia muda wangu mwigi kutafakari kuhusu usafi wa kujikinga dhidi ya viini kuliko masomo.
Kuna kipindi nilikuwa ninakesha kuosha nguo zangu tu au kuoga kwa mara ya pili au hata ya tatu kwasababu sikuhisi kuwa ni msafi inavyotakikana. Sikuwa na marafiki kwasababu nilihofia sana kuhusu kupata maambukizi - lakini pia niliogopa kwamba wangegundua kuwa mimi niko tofauti na wao.
Katika kipindi cha miaka mitano hivi iliyopita, nimeweza kudhibiti hali yangu kwa kiasi kikubwa kukabiliana na hofu yangu. Najitahidi sana kutenganisha hofu yenye tija na nyengineyo. Pia nimefaidika sana kuwa mwenza wangu muelewa na anayenisaidia kwa kila namna kila ninapomuhitaji.
Cha kutia moyo ni kwamba, watu ambao wamekuwa na tatizo la kuwa na wasiwasi au viini hapo kabla, wanasema kuwa sasa hivi hawana wasiwasi sana kwa janga la corona.
Pengine ni kwasababu watu wengine wamejiunga nao kimtazamo, na kuchukua tahadhari na pia kwa sasa hivi wanajifunza kukabiliana na msongo wa mawazo wa hali ya juu katika maisha yao ya kila siku.
Kwa kiasi fulani, huu ni ukweli. Lakini janga la corona pia nalo limeibua changamoto zingine kwangu. Onyo kutoka wizara ya afya imesisitizia ukweli wa kwamba viini vinaweza kusambazwa kwa urahisi kutoka mtu mmoja hadi mwengine hata tunapopishana mitaani.
Mwongozo wa kuosha mikono kumenifanya nianze kujiuliza ni mara ngapi nimekuwa nikiacha karai ya jikoni bila kuiosha vizuri.
Aidha, usafi wa nafaka umekuwa tatizo tena katika maisha yangu.
Hakuna kipya kwangu kwasababu ndio maisha ambayo nimekuwa nikishi.
Na siko peke yangu mwenye kupitia changamoto za afya ya akili.
Kote duniani, watu wamekuwa wakitafuta usaidizi kutoka kwa washauri tangu kutokea kwa janga la mlipuko wa virusi vya corona.
Nchini Marekani, baadhi ya wataalamu wameonya kwamba mfumo wa afya ya akili hauna uwezo wa kuhudumia idadi ya watu wanaondelea kutafuta tiba kila uchao.
Hilo ni sawa na kusema hakuna nchi yenye uwezo wa kijitosheleza katika kukabiliana na tatizo hili.
Wakati ambapo mazungumzo kuhusu janga la corona yanajikita katika ulegezaji wa masharti baada ya kanuni za kusalia ndani, kuwa na utulivu kunaweza kuwa jambo la msingi na gumu zaidi kuliko yote.
Haijalishi shule, maduka na ofisi zitafunguliwa lini, madhara ya Covid-19, hofu yote na wasiwasi vinavyoambatana na janga hili, ni mambo yatakayo shuhudiwa kwa miezi kadhaa ijayo.
Lakini kile ambacho nimejifunza kwa miaka kadhaa kuhusu kujitathmini na tiba ambayo nimekuwa nikipokea, kuwa na wasiwasi kunaweza kudhibitiwa.
Kwa tajriba yangu, hatua ambayo imekuwa ya msaada kwangu ni kuzungumza kuhusu hisia zangu kwa utulivu na uwazi na watu ninaowaamini, ama wawe ni wataalamu au watu wangu wa karibu.
Kwa watu wanaotimiza kanuni ya kusalia ndani, wasiwasi kunaweza kuwa tatizo la kiafya lenye kujumuisha mambo kadhaa kama vile ukosefu wa ajira, kujitenga na hata kukosa maisha ya raha ya kila siku waliozoea.
Kwa kubaini changamoto unazopitia, unaweza kuwa na mpango makhususi wa kukabiliana na nazo.
Ama ukatafuta ushauri kutoka kwa wataalam ambao wamesisitiza kuwa watu wengi zaidi wanaopata ugonjwa wa Covid -19, wana uwezo mkubwa wa kupona.
Pia unaweza kupata afueni kutokana na ushahdi wa kisayansi kwamba kuosha mikono mara kwa mara na sabuni kunatosha kujikinga dhidi ya viini na pia kuosha nguo zako kama kawaida tu kutaondoa virusi vilivyonasa kwenye nguo





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?