Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hezbollah yasema italipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya shambulio la vifaa vya mawasiliano


sdxz

CHANZO CHA PICHA,EPA

Kundi la Hezbollah la Lebanon limesema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba Katibu Mkuu wa kundi hilo, Hassan Nasrallah, atatoa hotuba siku ya Alhamisi, kufuatia milipuko ya vifaa vya mawasiliano kote Lebanon siku ya Jumanne.

Hezbollah imeahidi "kuendeleza operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel kwa kuunga mkono Ukanda wa Gaza" siku moja baada ya milipuko ya vifaa vya mawasiliano vya wanachama wake.

Chama hicho kilisema katika taarifa yake kwamba uungaji mkono kwa Gaza ni tofauti na kile ulichokitaja kuwa ni adhabu kali ijayo kwa adui mhalifu kwa mauaji ya siku ya Jumanne.

Hezbollah inaomboleza vifo vya wapiganaji wake wanane, akiwemo mtoto wa Mbunge wa Hezbollah, Ali Ammar.

Waziri wa Afya wa Lebanon, Firas Al-Abyad alisema idadi ya watu waliojeruhiwa kutokana na milipuko hii ni watu 2,750, pamoja na waliokufa tisa, akiwemo msichana wa miaka minane, akieleza kuwa takwimu hizi si za mwisho bado.

Waziri wa Lebanon alielezea wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba mejeraha mengi ni mabaya, akibainisha kuwa ni pamoja na majeraha ya uso, mikono, eneo la tumbo na macho, na kuongeza kuwa zaidi ya hospitali 100 nchini Lebanon zinapokea majeruhi.

Pia unaweza kusoma

Yaahidi kulipiza kisasi

SDX

CHANZO CHA PICHA,EPA

Hezbollah ya Lebanon ilitangaza kutokea kwa milipuko katika vifaa kadhaa vya kupokea ujumbe, ambavyo vinamilikiwa na idadi kubwa ya wafanyakazi katika vitengo na taasisi mbalimbali za Hezbollah.

Chama hicho kiliongeza katika taarifa yake kwamba, baada ya kuchunguza ukweli wote, data, na taarifa zilizopo, “tunamtaja adui Israel kuwa amehusika moja kwa moja kwa uhalifu huu uliolenga raia,” na kuahidi kulipiza kisasi kwa shambulio hilo.

Kwa upande wa serikali ya Lebanon imelaani kile ilichokitaja kama "uhalifu wa Israel, ambao unajumuisha ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya Lebanon na ni uhalifu kwa viwango vyote."

Baraza la Mawaziri lilisema "serikali ianza mara moja kufanya mawasiliano yote muhimu na nchi nyingine na Umoja wa Mataifa ili kuiwajibisha (Israel) kwa uhalifu huu unaoendelea."

Israel bado haijazungumzia shutuma hizo za Lebanon, lakini runinga ya Taifa ya Israel, imenukuu Baraza la Mawaziri kwamba limetoa "maagizo kwa mawaziri wote kutotoa matamshi yoyote."

Shirika la Usalama wa Ndani la Lebanon, limesema vifaa vya mawasiliano vililipuka katika maeneo kadhaa ya Lebanon, pamoja na vitongoji vya kusini, na kusababisha majeruhi.

DS

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Katika taarifa yake, shirika hilo limewataka wananchi kuondoka barabarani ili kurahisisha matibabu ya majeruhi na kuwapeleka hospitalini.

Afisa wa Hezbollah alisema kulipuliwa kwa vifaa vyao vya mawasiliano ndio "kuingiliwa kukubwa kwa usalama" wa kikundi hicho karibu mwaka mmoja tangu vita na Israel kuanza, kulingana na Reuters.

Mwandishi wa habari kutoka shirika hilo ambaye alikuwa katika kitongoji cha kusini aliona watu kumi wenye mafungamano na Hezbollah wakivuja damu.

Shirika la Habari la Iran, Mehr lilitangaza kuwa balozi wa Iran nchini Lebanon, Mojtaba Amani, alijeruhiwa kutokana na "mashambulizi ya mtandao" yaliyolenga Lebanon na Syria, bila kutoa maelezo ya ziada.

Kwa upande wake, ubalozi wa Iran nchini Lebanon ulithibitisha kuwa Balozi Amani alipata "jeraha dogo na yuko katika hali nzuri."

Hospitali zajaa

SDXC

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Mwandishi wa BBC alithibitisha kuuawa kwa mtoto wa mbunge wa Hezbollah, Ali Ammar katika shambulio hilo, na kujeruhiwa mtoto wa mbunge Hassan Fadlallah.

Hospitali kadhaa huko Beirut zilitangaza kujaa kutokana na idadi kubwa ya waliojeruhiwa. Wizara ya Afya ya Umma ilizitaka hospitali kuwa tayari na kuinua kiwango chao cha maandalizi.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon lilitangaza kutayarisha magari 50 ya ziada ya kubebea wagonjwa na watoa huduma za kwanza 300 ili kusaidia waathiriwa.

Wizara ya Afya ya Lebanon ilitoa wito wa dharura kwa wafanyakazi wote katika sekta ya afya kwenda mara moja katika maeneo yao ya kazi ili kukidhi mahitaji ya dharura ya kiafya.

Wizara iliwataka wananchi wote wanaomiliki vifaa vya mawasiliano vya aina hiyo wavitupe mara moja.

Mashambulizi nchini Syria

Mashambulizi ya aina hiyo pia yameripotiwa katika vitongoji vya kusini vya Bekaa, Nabatieh, Al-Hush, Bint Jbeil, Tyre, na kusini mwa Lebanon, pamoja na baadhi ya mikoa ya Syria, kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari vya Syria.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria pia lilitangaza kuwa watu 14 wanachama wa Hezbollah walijeruhiwa kutokana na milipuko ya vifaa vya mawasiliano ndani ya gari huko Kafr Sousse, Syria.

Vilevile, kumetokea milipuko mingine katika maeneo ya Sayyida Zeinab na Qalamoun Magharibi, na kuthibitisha kuwa ni milipuko kama ile iliyotokea katika maeneo kadhaa nchini Lebanon.

Shirika hilo lilisema idadi ya waliojeruhiwa ni watu 14, lakini haikufichua juu ya utaifa wao. Chanzo kutoka Hezbollah kiliithibitishia Agence France-Presse, wanachama wa kundi hilo walijeruhiwa na milipuko ya vifaa vya mawasiliano nchini Syria bila kutaja idadi yao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?