Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kisima kikubwa China kuwahi kutokea Duniani;


Kwa nini China inachimba kisima chenye kina cha kilomita 11 ardhini?

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kitakuwa kisima kirefu zaidi kilichotengenezwa na mwanadamu nchini Uchina

China imeanza kuchimba kisima chenye kina cha zaidi ya kilomita 11 (futi 11,100) ndani ya jangwa la Taklamakan katika mkoa wake wa kaskazini-magharibi wa Xinjiang.

Kazi ya mradi huu ilianza wiki iliyopita.

Kulingana na ripoti ya shirika rasmi la habari la China "Xin Wa", kisima hiki chenye kina kirefu kitafikia tabaka za kipindi cha zamani zaidi cha Cretaceous duniani.

Muda uliokadiriwa wa mradi ni siku 457 ambapo wanaofanya kazi hapa watakuwa na shughuli nyingi usiku na mchana na mashine nzito.

Mradi wa kipekee

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Tayari kuna kisima cha mafuta kilicho umbali wa kilomita tisa ndani ya jangwa la Taklamakan

Mradi huo unatajwa kuwa mradi mkubwa zaidi wa uchimbaji madini nchini China.

Hapo awali, kisima kirefu zaidi cha aina yake nchini China kilirekodiwa kuwa na mita 10,000.

Hata hivyo, kisima kinachochimbwa na Uchina hakitakuwa chenye kina kirefu zaidi lililotengenezwa na mwanadamu.

Rekodi hiyo inashikiliwa na kisima cha 'Kola' nchini Urusi, ambacho kilifikia mita 12,262 (zaidi ya kilomita 12) mnamo 1989 baada ya karibu miongo miwili ya shughuli ya uchimbaji, kabla ya kusimamishwa.

Tangazo la mradi huu mkubwa na China linakuja wakati nchi hiyo ikichukua hatua muhimu kuimarisha msimamo wake kama iliyo na nguvu kimataifa ya kiteknolojia na kisayansi.

Jambo la kupendeza ni kwamba, siku ileile ambayo kazi ya mradi huu mpya ilianza, China ilituma wanaanga wake watatu kwenye kituo cha anga cha juu.

Ikijaribu kufika kwenye mwezi kabla ya mwaka wa 2030.

Lakini swali ni je, kwa nini China inachimba kisima kikubwa sana kiasi hiki, ambalo kina chake ni zaidi ya urefu wote wa kilele cha mlima ulio juu zaidi duniani, Mlima Everest?

Mradi huo unaongozwa na shirika la serikali la petrochemical 'Sinopec'. Hivi majuzi, Sinopec imetangaza lengo lake la 'kupanua mipaka ya kina' katika uchunguzi wa kijiolojia.

Malengo ni mawili

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kampuni zinazomilikiwa na serikali ya China zitafanya kazi katika mradi huu

Mradi huo unaongozwa na shirika la serikali la petrochemical 'Sinopec'. Hivi majuzi, Sinopec imetangaza lengo lake la 'kupanua mipaka ya kina' katika uchunguzi wa kijiolojia.

Takriban miaka miwili iliyopita, Rais Xi Jinping wa China alihimiza jumuiya ya wanasayansi ya nchi hiyo kuongeza kasi ya kuchunguza rasilimali za ndani kabisa za dunia.

Na sasa mradi huo umezinduliwa karibu miaka miwili baada ya agizo la Rais wa China kwa jumuiya ya wanasayansi.

Liu Xiaogang, mwakilishi wa Shirika la Kitaifa la Petroli la China, kampuni kubwa zaidi ya nchi hiyo inayofanya kazi ya utafiti wa mafuta na gesi nchini China, alisema kuwa uchimbaji wa kisima hiki una malengo mawili: utafiti wa kisayansi na uchunguzi wa mafuta na gesi.

'Ikumbukwe kwamba 'Shirika la Kitaifa la Petroli la China' sio tu kampuni kubwa zaidi nchini China, lakini pia ni moja ya kampuni kubwa zaidi za mafuta na gesi ulimwenguni.

Katika ujumbe wa video akielezea mradi huo, Liu Xiaogang alihakikisha kuwa mradi huo ni sehemu ya juhudi za kuunganisha na kuimarisha uwezo wa kiufundi wa PetroChina (biashara inayodhibitiwa na Shirika la Kitaifa la Petroli la China na kusajiliwa kwenye Soko la Hisa la Hong Kong).

Aidha alisema mradi huo utasaidia katika uzalishaji wa mashine mpya na za kisasa za uchimbaji madini.

Akizungumzia umuhimu wa mradi huu, mwanajiolojia Cristian Farias aliambia BBC kwamba jumuiya ya wanasayansi duniani kwa kawaida hutumia tomografia ya tetemeko la ardhi na mbinu nyinginezo kuchunguza sehemu za kina kabisa za Dunia. ''Miradi ya aina hii ni muhimu sana kwani inatoa ushahidi halisi ili kusaidia utafiti.''

Cristian Farias, ambaye pia ni mkurugenzi wa Kazi za Ujenzi na Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Timoco, anasema mradi wa China utatoa fursa ya kupima vifaa vya hali ya juu zaidi na maendeleo ya kiteknolojia kuwahi kufanywa, na kuanzisha jambo jipya kwa ulimwengu.

Milango mpya itafunguliwa.

Mafuta na Gesi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jangwa la Taklamakan linachukuliwa kuwa eneo gumu kufanya kazi, huku nyuzijoto ikishuka hadi nyuzi 20 Celsius wakati wa baridi.

Shirika la Kitaifa la Petroli la China pia limedokeza kuwa mradi huo pia unalenga kupata hifadhi mpya ya mafuta na gesi yenye kina kirefu sana katika eneo hilo.

Madini ya hidrokaboni kwenye kina kirefu cha Dunia, kwa kawaida chini ya mita 5,000 (au kina cha kilomita tano), yako katika maeneo ya baharini, ambapo tabaka za miamba na mashapo ni nene, lakini wakati mwingine pia hupatikana katika maeneo ya nchi kavu.

Jangwa la Taklamakan linasemekana kuwa eneo ambalo hifadhi kubwa ya mafuta na gesi asilia inaweza kupatikana.

Hata hivyo, kulingana na wataalamu, muundo wa kijiolojia wa jangwa hili, kama vile joto kali na shinikizo la juu, inaweza kusababisha changamoto kubwa za kiufundi wakati wa kufanya kazi katika mradi huo.

Profesa Cristian Farias anasema kwamba 'kudumisha kuwepo kwa kisima hicho lenye kina kirefu pia ni changamoto kubwa.'

Ingawa Urusi iliweza kuchimba kina cha kilomita 12 miaka ya nyuma, wataalam wanasema kuwa kufikia kiwango cha chini cha ukoko wa Dunia bado kunaweza kuwa jambo gumu sana.

Sun Jinsheng, mwanasayansi katika Chuo cha Uhandisi cha China, aliliambia shirika la habari la serikali la Xinwa kwamba "ujenzi wa mradi huu wa kuchimba visima ni sawa na kuendesha lori kubwa kwenye waya mbili nyembamba za chuma (yaani, ni mradi mgumu sana).'

Kwa kuongezea, jangwa la Taklamakan linachukuliwa kuwa eneo gumu kufanya kazi, huku halijoto ikishuka hadi nyuzi 20 za Selsiasi wakati wa msimu wa baridi na kufikia nyuzi joto 40 wakati wa kiangazi.

Pia unaweza kusoma:

Iliyosomwa zaidi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?